Mwili wa Daktari Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu waokotwa maeneo ya Malolo, Tabora

Mwili wa Daktari Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu waokotwa maeneo ya Malolo, Tabora

Kuna uwezekano pakawa na changamoto kubwa ndani ya vyombo vyetu vya usalama, je tuna uhakika hawa wanaopoteza maisha hawajawahi kujihusisha na chombo chochote cha usalama?

Vipi kama kuna tatizo limetokea hivyo wanaondolewa waliokua sehemu ya hilo tatizo, maana siamini kuwa huyu Daktari ameponzwa na yaleyale tunayodhania.
 
Wazungu wanasema no loose end.wote waliokuwepo kweye mission wanafutwa .
 
Mwili wa Dr. Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu, Tabora umeokotwa maeneo ya Malolo, Tabora asubuhi ya leo. Dr.Chami aliondoka nyumbani (Kaliua) Jumatano ya September 4 na kumuaga mkewe kuwa anakwenda mjini Tabora kikazi na angerejea kesho yake. Hata hivyo hakurejea na simu zake hazikupatikana

Familia ilimtafuta kwa wiki nzima bila kujua alipo, lakini ilipofika Jumatano ya September 11 simu zake zilipatikana. Hata hivyo alipopigiwa hakupokea. Baadae alituma sms kwa mke wake iliyosomeka "Nisamehe sana, baada ya dakika chache sitakuwa nanyi duniani. Simamia kila kitu nilichokiacha. Pesa zote zipo CRDB bank, simamia watoto wasome. Kwaheri"

Baada ya kutuma sms hiyo, simu yake ilizimwa na hakupatikana tena. Polisi kwa kushirikiana na familia waliendelea kumtafuta bila mafanikio. Hatimaye leo mwili wake umeokotwa maeneo ya Malolo, ukiwa umechomwa sindano. Pembeni ya mwili huo kuna madawa mbalimbali ya hospitali ambayo inadaiwa yalitumika kujidunga/kudungwa.

Bado haieleweki kama amejiua mwenyewe kwa kujidunga madawa au ameuawa na watu waliomdunga madawa hayo. Haijafahamika pia kama sms aliyotuma kwa mkewe alituma kwa utashi wake au alikuwa chini ya shinikizo. Polisi wamesema wanachunguza chanzo cha kifo chake kujua kama kimetokana na migogoro ya kifamilia, Msongo wa mawazo, madeni, ugomvi binafsi au sababu nyinginezo. Rest easy Dr. Chami.!

Credit: Malisa GJ, X Page

Kijana mdogo sana. Sijui nini kinaendelea sasa hivi
 
Nchi hii kwasasa hali si shwari yani tunapoendea tutaanza kuogopana sisi kwa sisi.Kile kisiwa cha amani kimekuwa kisiwa chenye hofu kubwa.

E Mungu tesaidie.
 
Mkiambiwa mzungu fulani alianza kwenye store (garage) ya wazazi wake kwao na sasa ni millionaire tunakenua na kuona linawezekana
Lakini kwa sisi mtu akisema nilianza kuuza dagaa na leo namiliki meli mnaguna
Kila mmoja apambane kivyake
Anaweza akawa hivi, kafanya vile
Hayatuhusu 😄
 
Back
Top Bottom