Mwili wa Daktari Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu waokotwa maeneo ya Malolo, Tabora

Mwili wa Daktari Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu waokotwa maeneo ya Malolo, Tabora

Tusikimbilie kusingizia vyombo vya usalama wala fidiemu. Wengine waliiba wake za watu labda
akiiba mke wa mtu mwenye jukumu la kumlinda afikishwe kwenye vyombo vya sheria ni nani

basi vyombo vya ulinzi viondolewe tufanye kuhukumiana wenyewe huku mtaani
 
Wewe jamaa umenikumbusha mbali sana.Tulikua tunapaita Mkwakwani pale pembeni kidogo ni Isungu Honey pot.Mwaka 1960 kabla ya uhuru wa Tanganyika. 🤔

Ebu kausha mazee...
Tupo Oxygen tunaomboleza taratibu na...🍻
Poleni sana mkuu, kumbe unafaidi zizini uhazili na oxygen! Vipi Orion Tabora hotel bado pananoga sasa au pamepoa?

Isungu pale kwa akina Fundikira na Mgalula opposite na geti kubwa la zizini.
 
Exactly.

Sms fake ya kutengenezwa yenye nia ovu ya kutaka kuwaghiribu watu ili wasijue kiini halisi Cha Mauaji hayo.
Just a spinning Propaganda.

Hali mbaya kabisa Kama Hii inanikumbusha wakati ule wa nyakati za mwisho mwisho kabisa kabla ya kuanguka kwa Utawala dhalimu wa Dikteta Mobutu Sesseseko aliyekuwa Rais wa zamani wa Zaire (Sasa Congo DR), Watu wengi sana walikuwa wakitekwa na kuuawa katika Mazingira ya kutatanisha Sana kama hivi inavyotokea hivi sasa hapa Tanzania. Maiti za Watu wakosoaji wa Utawala wake zilitakapaa mitaani, kila siku Wananchi walikuwa wanaokota miili ya Watu mitaani.
Aidha, kila siku (hususani nyakati za usiku) ndege na helikopta za Jeshi zilikuwa zinatua nyumbani kwa Rais Mobutu kijijini kwake Gbadolite zikiwaleta 'Mateka' waliokusanywa kutoka katika miji na mikoa mbalimbali iliyopo kwenye nchi hiyo ya Zaire ili wàweze kuteswa mbele ya Rais Mobutu mwenyewe akishuhudia kwa macho yake na mwishowe mateka hao waliuliwa kikatili sana. But all in all, mwisho wa dhahama yote hiyo, Dikteta Mobutu aliishia kumteka hata Mkuu wake wa Majeshi (CDF) General Mahele na kumuua kikatili kama nguruwe pori, na hapo ndipo Utawala wake wa kidikteta ulipofika mwisho wake.

Watanzania tuzidishe sala na maombi kwani kunakaribia kukucha, Wakimaliza kututeka sisi Wananchi basi watageukiana wao kwa wao, kama ilivyofanyika nchini Zaire kwa Rais Mobutu.
General Mahele alikuwa Waziri wa Ulinzi na wala hakuuliwa na Mobutu mwenyewe bali mtoto wa Mobutu ambaye alikuwa anaona nchi ni shamba la familia yao. Of course ni yaleyale pipa na mfuniko.

Alikuwa Kanali jeshi likashindwa ulinzi akakasirika akatafuta wanaofanya mazungumzo na waasi wa Kabila, maana jeshi lilijaza vilaza kupigana hawawezi. Mobutu alikuwa na machawa tu. Siku mbili baadae baba yake akakimbia nchi.

Ikifika hatua ya mamlaka kuwa desperate, hata akina Mafwele utasikia wameuwawa. Kawaida kabisa hasa former Socialist countries
 
Serikali ifanyie kazi haya matukio,hali sio nzuri,tungesema ni siasa lkn wangine hawana uhusiano na siasa wanakufa, haya mambo hayaleti afya kwa serikali yetu,kila mtu ameshaingia hofu hatujui kesho anaondoka nani.Nina mashaka hata watu wenye visasi wanautumia huu mwanya wa serikali kukaa kimya kufanya yao kwa maadui zao...
 
Duuh na maCDF wanatekwa? Hakuna aliye salama
Baada ya waasi kulishinda nguvu jeshi uchwara la Dikteta Mobutu, jeshi lililozoea kuua na kuteka ila kupigana halijui kitu. Basi Jenerali Mahele aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na vigogo wauaji wengine wakamwambia Mobutu hawawezi kuulinda mji mkuu Kinshasa.

Mobutu kwa kujiona mungu mtu aligoma kwanza, wakasisitiza hawawezi kuulinda mji maana stronghold yao iliishaanguka kwa mauaji ya mamia ya watu siku chache kabla. Sasa Mobutu alikuwa na kikosi maalumu cha vilaza ila ndio mzee, wao hawajui kutumia akili na kukubali amri. Ikabidi Jenerali Mahele aende kuwaeleza hawa vilaza kuwa wasipigane uwezo hawana vita serikali imeishashindwa.

Kule akakuta mtoto wa Mobutu, Kongulu Mobutu. Huyo ndio Mafwele wa kule, akakasirika kuona hawa wanaleta uhalisia kuwa baba yake nchi imemshinda soon anaangushwa. Akatumia machawa wake kumteka Mahele na kumuua.

Muosha uoshwa.
 
Back
Top Bottom