Mwili wa Khalid, Askari aliyeuawa Pemba Oktoba 28 wapatikana

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Mwili wa askari wa KVZ aliyejulikana kwa jina la Khalid umepatikana baada ya kuuawa siku ya uchaguzi

=====

Pemba. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limefanikiwa kuupata mwili wa aliyekuwa askari wa kikosi cha KVZ Khalfan Junedi aliyedaiwa kuuawa wiki tatu zilizopita eneo la Ngwachani Wilaya ya Mkoani.

Pamoja na mwili huo jeshi hilo pia limefanikiwa kuipata bunduki aina ya AK47 katika eneo la Ngwachani Novemba 12 majira ya saa 2:00 usiku huku magazine yake ikiwa na risasi 21.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Khamis Makarani amesema mwili huo ulipatika katika kijiji cha Chonga kwenye bonde la Kisitu mbwa.

Alisema kuwa, Novemba 15 walifanikiwa kuupata mwili wa askari huyo baada ya kumkamata mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Ussi Foum Machano mkazi wa Ngwachani, ambaye aliwapeleka kwenye eneo alilofukiwa.

“Novemba 12 tulimkamata Ussi, maeneo ya Chake Chake, tulimhoji na ndipo akatuambia mahala ilipo bunduki na baadaye kwenda kutuonyesha eneo alipowekwa marehemu huyo”, amesema Kamanda Makarani.

Ameeleza kuwa, baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi, walibaini kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa na majeraha ya kupigwa huku akiwa amekatwa baadhi ya viungo vya mwili wake.

“Taratibu zote za kiuchunguzi kuhusiana na mwili zimefanywa, mwili umesafirishwa kwenda Unguja kwa ajili ya mazishi”, amesema.

Alisema kuwa, upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika na kusema kuwa wanaamini watawakamata watu wengine waliohusika na tukio hilo.

Amesema kuwa, Oktoba 28 mwa huu askari huyo pamoja na wengine walikuwa kwenye doria za kawaida, ambapo askari huyo alipotea majira ya saa 2:00 usiku akiwa na bunduki AK47.

Aidha, kamanda Makarani amewataka wananchi wa Ngwachani kurudi katika maeneo yao ya kuishi, ili waendelee na shughuli zao za maisha, kwani amani na utulivu imerejea.

“Waliokuwapo maporini warudi na waliokuwa nje ya Pemba warudi, sisi kimsingi tunawatafuta watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusika na mauaji ya huyo askari na sio wananchi wa kawaida”, amesema.

RPC Kusini Pemba azungumza na Wanahabari kupatikana kwa Bunduki ya AK47 pamoja na mwili wa marehemu askari wa vikosi wa SMZ​

1605587729274.png

WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini taarifa ya mauwaji ya askari wa vikosi vya SMZ, iliyotolewa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Makaran (hayupo pichani)ofisini kwake Madungu Polisi.
1605587747828.png

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Makaran, akiwaonyesha waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Kisiwani Pemba, bunduki iliyopatikana aina ya AK47 na magazine yake, bunduki ambayo ilitoweka pamoja na marehemu askari wa vikosi
1605587766175.png

MKUU wa Upelelezi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Tadei Mchomvu, akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupatikana kwa bunduki aina ya AK47 iliyopatikana pamoja na mwili wa marehemu askari wa Vikosi vya SMZ aliyekua ameuawa
1605587779223.png

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Khamis makarani, akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kupatikana kwa bunduki iliyokua imepotea aina ya AK47 na mwili wa marehemu askari wa vikosi vya SMZ aliekua ameuawa
 
Mwili wa askari wa kvz aliyejulikana kwa jina la Khalid umepatikana baada ya kuuwa siku ya uchaguzi

Habari zaidi zitakujia

Source
Mwananchi
Wanaanza kutengeneza matukio baada ya kusikia kuna ICC??? Waambie wamechelewa sana. Hakuna askari aliyeuwawa Pemba, hayo ni matukio wanayatengeneza.

Pemba majeshi ndo yaliuwa wananchi. Majeshi ya Tanzania ambayo wakuu wake ni Diwani Athumani, SIMON Sirro na Venance Mabeyo, huku amiri jeshi mkuu wao ni John Pombe Magufuli
 
Mkuu,

Wewe majibu yako kwenye uzi au mada unazoanzisha inathibitisha pasipo shaka kwamba unachuki binafsi inayofungamana na itikadi yako una chuki iliyo ya wa zi kwa hawa:
1. Diwani Athumani,
2. SIMON Sirro
3. Venance Mabeyo,
4. Amiri jeshi mkuu wao ni John Pombe Magufuli

Sijui kama una kifua cha kupambana nao kwa kutumia hiyo ICC isiyo na mamlaka na tuhuma zako hizo. Tambua wewe sio Roboti unapotumia hicho kibodi cha kinakirishi wakati utambulisho wako wote umeuweka wazi

Kumbuka
1. Hakuna uhuru bila mipaka
2. Hakuna haki bila wajibu
3. Hakuna utu bila uwepo wa watu
4. Hakuna maendeleo bila kufanya kazi kwa bidii na maarifa

Pia Tambua

1. Ukituhumu unawajibika kuthibitisha kwa ushahidi unaokubalika kisheria na katika mamlaka yenye uwezo wa kutoa suluhisho
2. Uksimtendee mtu mwingine jambo ambalo wewe au utaratibu uliowekwa unakataza kutendewa
3. Ukiheshimu mamlaka ya nchi na kiongozi wake unampa wajibu wa kukutendea vivyo hivyo bila kujali nafasi yako katika jamii
 
Umeandika vizuri mno,kwa kifupi with authoritative tone!!Naamini uliyekuwa unamjibu amekuelewa vizuri.
Tunaoingia humu hii ni warning tosha.
Umetuzindua wengi!!
 
Mkuu,

Wewe majibu yako kwenye uzi au mada unazoanzisha inathibitisha pasipo shaka kwamba unachuki binafsi inayofungamana na itikadi yako una chuki iliyo ya wa zi kwa hawa:
1. Diwani Athumani,
2. SIMON Sirro
3. Venance Mabeyo,
4. Amiri jeshi mkuu wao ni John Pombe Magufuli

Sijui kama una kifua cha kupambana nao kwa kutumia hiyo ICC isiyo na mamlaka na tuhuma zako hizo. Tambua wewe sio Roboti unapotumia hicho kibodi cha kinakirishi wakati utambulisho wako wote umeuweka wazi

Kumbuka
1. Hakuna uhuru bila mipaka
2. Hakuna haki bila wajibu
3. Hakuna utu bila uwepo wa watu
4. Hakuna maendeleo bila kufanya kazi kwa bidii na maarifa

Pia Tambua

1. Ukituhumu unawajibika kuthibitisha kwa ushahidi unaokubalika kisheria na katika mamlaka yenye uwezo wa kutoa suluhisho
2. Uksimtendee mtu mwingine jambo ambalo wewe au utaratibu uliowekwa unakataza kutendewa
3. Ukiheshimu mamlaka ya nchi na kiongozi wake unampa wajibu wa kukutendea vivyo hivyo bila kujali nafasi yako katika jamii
The Hague haiepukiki jiandaeni kisaikolojia
 
The ICC haiwezi kuhusu hao uliowataja:-
(a). Wapi walishika silaha na kufyatulia watu na kuwaua?
(b). Lini waliamrisha askari kuua?
(c). ICC watapata ushahidi kwa nani hapa nchini ukiachilia mbali viongozi wa vyama vya siasa?

Nionavyo:-
= CP Diwani Athumani mnamuonea bure kwa sababu ya ukimya wake,
= IGP Simon Sirro mnamtwika zigo lisilomuhusu,
= General Mabeyo mnamulaumu bure, na
= Rais Dkt Magufuli mnamuorodhesha ktk orodha kinafki huku mkijua hakuna alilotenda sababu nae alikuwa mgombea sawa na TL, Rungwe, Lipumba nk
 
Basi na wewe una mahaba nao kulingana na itikadi yako.
 
Wanatengeneza tukio. Ni usanii. Hakuna askari aliyeuawa. Wameoana mambo ynawaendelea kombo hivyo wanajaribu kujinasua. Ondoa ujinga wako hapo. Rudisha kwa huyo mjinga aliyekutuma
 
The ICC haiwezi kuhusu hao uliowataja:-
(a). Wapi walishika silaha na kufyatulia watu na kuwaua?
(b). Lini waliamrisha askari kuua?
(c). ICC watapata ushahidi kwa nani hapa nchini ukiachilia mbali viongozi wa vyama vya siasa?

Nionavyo:-
= CP Diwani Athumani mnamuonea bure kwa sababu ya ukimya wake,
= IGP Simon Sirro mnamtwika zigo lisilomuhusu,
= General Mabeyo mnamulaumu bure, na
= Rais Dkt Magufuli mnamuorodhesha ktk orodha kinafki huku mkijua hakuna alilotenda sababu nae alikuwa mgombea sawa na TL, Rungwe, Lipumba nk
Umeandika unafiki. Vyombo vinajihamuru vyenyewe ?!
 
Mkuu,

Wewe majibu yako kwenye uzi au mada unazoanzisha inathibitisha pasipo shaka kwamba unachuki binafsi inayofungamana na itikadi yako una chuki iliyo ya wa zi kwa hawa:
1. Diwani Athumani,
2. SIMON Sirro
3. Venance Mabeyo,
4. Amiri jeshi mkuu wao ni John Pombe Magufuli

Sijui kama una kifua cha kupambana nao kwa kutumia hiyo ICC isiyo na mamlaka na tuhuma zako hizo. Tambua wewe sio Roboti unapotumia hicho kibodi cha kinakirishi wakati utambulisho wako wote umeuweka wazi

Kumbuka
1. Hakuna uhuru bila mipaka
2. Hakuna haki bila wajibu
3. Hakuna utu bila uwepo wa watu
4. Hakuna maendeleo bila kufanya kazi kwa bidii na maarifa

Pia Tambua

1. Ukituhumu unawajibika kuthibitisha kwa ushahidi unaokubalika kisheria na katika mamlaka yenye uwezo wa kutoa suluhisho
2. Uksimtendee mtu mwingine jambo ambalo wewe au utaratibu uliowekwa unakataza kutendewa
3. Ukiheshimu mamlaka ya nchi na kiongozi wake unampa wajibu wa kukutendea vivyo hivyo bila kujali nafasi yako katika jamii
Jamaa umempa mkwara mzito kweli kweli.Nafikiri hatarudia tena
 
Umeandika unafiki. Vyombo vinajihamuru vyenyewe ?!
Rejea kesi ya ASP Baganda, kwa nini IGP Mahita hakushitakiwa kwa kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini pale Mabwepande?

Kabla ya kufanya jambo lolote askari mwenyewe lazima ufahamu madhara ya matumizi ya nguvu ktk ground - sasa wapi kati ya hao tuliowataja walipoamrisha askari kufyatua risasi, kupiga watu nk?
 
Back
Top Bottom