Mwili wa Mtu aliyefungwa kwenye Kiroba wapatikana ukielea kwenye Mtaro Jangwani

Mwili wa Mtu aliyefungwa kwenye Kiroba wapatikana ukielea kwenye Mtaro Jangwani

JITU BANDIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2023
Posts
4,368
Reaction score
9,937
Taharuki imezuka maeneo ya Jangwani, Dar es Salaam baada ya mwili wa Mtu kupatikana ukiwa umefungwa kwenye kiroba ukiwa unaelea katika mtaro.
===============
Mwili wa mtu mmoja umeonekana asubuhi ukielea majini kwenye mtaro uliopo Jangwani, jirani na kilipokuwa kituo cha mabasi ya mwendokasi.

Katika eneo hilo kwa sasa unaendelea ujenzi wa barabara mbadala kabla ya kubomolewa ya awali kupisha ujenzi wa daraja la juu litakalounganishwa eneo la Fire na Magomeni.

Mwili huo wa mtu mzima umeonekana leo Jumatano Agosti 27, 2025, hivyo kuzua taharuki kwa wananchi waliotumia Barabara ya Morogoro lililoko eneo la Jangwani.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (SACF), Peter Mabusi amesema walipata taarifa ya kuwepo kwa mwili huo saa 3:30 asubuhi, hivyo walituma timu kufuatilia.

Amesema timu hiyo ilikuta mwili wa mtu mzima aliyetambuliwa kwa jina la Swalehe Shukurani, ukiwa chini ya daraja lenye maji.

Amesema mwili huo uliopolewa na umekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 
Back
Top Bottom