Mwingine Auawa; Jeshi la Polisi Fanyeni Uchunguzi na Mtupe Taarifa.

Mwingine Auawa; Jeshi la Polisi Fanyeni Uchunguzi na Mtupe Taarifa.

Kama walihitaji Namba ya siri kutoka kwa Mama, bila shaka huyo ni Jakobo.
 
Atakuja kusema "KIFO NI KIFO TU"

Anyway, RIP kwake Mwamba.
 
Kuna michezo mkishaianzisha basi mtegemee na mtakuwa mmewafumbua wengine macho kwa kuona inawezekana kumbe kufanya abcd.

Tukiendeleza hizi style Kwa kuona zinatusaidia kwenye ugali wetu na umaarufu wetu basi tutambue tunadhidi kuwapa watu ujasiri na mbinu, tutafika mahala watu wataanza hata kukodi wauwaji wa kimataifa kuanzia snipers, wapiga visu, wazee wa sumu nk
 
View attachment 3101087
Pichani ni kijana aitwaye Aziz Alumini Njombi wa huko wilaya Nanyumbu.

Huyu kijana hajihusishi na siasa wala mambo ya uanaharakati na kazi yake ni afisa usafirishaji a.k.a bodaboda.

Mnamo tarehe ya jana yaani 19/9/2024 alitekwa na mtu aliyembeba kama abilia ila inasemekana hakuwa abilia bali mtekaji.

Baadaye usiku wa kuamkia leo watekaji walipiga simu kwa mke wake wakitaka password ya simu ya mumewe.

Ila baadaye hao watekaji walimuua na leo maiti yake imeokotwa.

NB. Jeshi la polisi nchini, kutokana na kadhia hii ya utekaji raia ovyo hata vibaka, majambazi, wezi na kila muarifu wanatumia mbinu ya kuteja na kuua.

Kwa sababu inaonekana tayari ni njia iliyohararishwa wkt si kweli, ikiwa nyie ndiyo wenye jukumu la kuwalinda raia kisheria basi tunaomba ulinzi.

Vinginevyo mruhusu sasa raia wajilinde katika hali yoyote.

CC. Nawasilisha.
 
Attachments

  • 5828116-3deca1cd82eed06379e0266b4db1399a.mp4
    25.6 MB
Vijana tunaangamia na kuacha familia zinazotutegemea zikiwa zinateseka, ewe kijana lolote unalolifanya angalia kwanza wanaokutegemea. NI HAYO TUU KWA LEO..
 
vibaka,majambazi na waporaji ni wazi sasa wanatumia upepo wa kutekana kufanya matukio yao
Hao #1 wenyewe ndiyo watekaji,waporaji wakuu
Kwanini wengine wasipite na upepo wao maana wameona sasa imehalalishwa
Watekaji wana kinga kutoka juu
Wanajua hata upelelezi hautofanyika

Ova
 
“Polisi ni jamii na jamii ni polisi.” tushirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa taarifa na tushirikiane kufichua uovu unaoendelea.
Tutabaki tunailaumu polisi kila siku kwani wao ni wapiga ramli kua fulani leo atauwawa?
Kama n hapana bhasi sisi ndio wenye taarifa na hawa watenda maovu ni wana jamii wenzetu
Inayoharibika ni Tanzania
Sahv hakuna ushirikiano wa polisi na jamii,jamii yenyewe haina imani nao
Wao watajuwa wanajilindaje

Ova
 
Usafiri wa bodaboda na bajaj upigwe marufuku turudie usafiri wa baiskeli, teksi, hiace na daladala.

Nchi za kusini mwa Afrika wameweza kujizuia kufanya pikipiki au bajaj (vespa) kuwa chombo cha usafiri wa umma na maisha yanaendelea, kwanini Tanzania tunashindwa kuwa kama nchi za Kusini mwa Afrika.
Kwa nchi yako kuzuia ni ngumu sana, moja wamesha halarisha pili hii njia ya kuruhusu hayo madude ni sehemu ya kuwafanya vijana kuwa busy na kusahau mambo ya msingi.
 
Wahalifu wanajuwa utekaji umeruhusiwa na wao wnapita
Mule mule

Ova
 
View attachment 3101087
Pichani ni kijana aitwaye Aziz Alumini Njombi wa huko wilaya Nanyumbu.

Huyu kijana hajihusishi na siasa wala mambo ya uanaharakati na kazi yake ni afisa usafirishaji a.k.a bodaboda.

Mnamo tarehe ya jana yaani 19/9/2024 alitekwa na mtu aliyembeba kama abilia ila inasemekana hakuwa abilia bali mtekaji.

Baadaye usiku wa kuamkia leo watekaji walipiga simu kwa mke wake wakitaka password ya simu ya mumewe.

Ila baadaye hao watekaji walimuua na leo maiti yake imeokotwa.

NB. Jeshi la polisi nchini, kutokana na kadhia hii ya utekaji raia ovyo hata vibaka, majambazi, wezi na kila muarifu wanatumia mbinu ya kuteja na kuua.

Kwa sababu inaonekana tayari ni njia iliyohararishwa wkt si kweli, ikiwa nyie ndiyo wenye jukumu la kuwalinda raia kisheria basi tunaomba ulinzi.

Vinginevyo mruhusu sasa raia wajilinde katika hali yoyote.

CC. Nawasilisha.
CC chiembe
 
Back
Top Bottom