Mwingira wa EFATHA awaita Viongozi ya Serikali ni washenzi

ina maana huyu mwizi katutukana na sisi,, maana kama serikali ni washenzi na wanaongozwa lazima wawe washenzi wanaokubaliana na ushenzi unaofanywa na washenzi......... Mshenzi yeye na yeyote anakubaliana naye..
 
ndugu issue si imani uliyozaliwa nayo, bali imani sahihi yenye kufuata amri za mungu ndani ya biblia takatifu na imani ya yesu pekee.
Kumb. Mzazi hata beba dhambi ya mtoto wala mtoto dhambi ya mzazi. Take it mr/mis/ms

duuuu!!!.....kwahiyo kwenda kwa mwingira ndo kufata dini sahihi?......... Hujui biblia wewe..... Kweli watu wake mnaangamia kwa kukosa maarifa...
 

HAHAHAHAHAHAHAHA...... Hapo kwa RED....... Hivi jamani Biblia mnazibeba urembo au? Someni Biblia muijue kweli na kuamka kiroho.....

 
Mmmmmmh! huyu Mwingira sasa anautani na serikali hiyi ya Kidharimu kwani wamemfanyia nn tena au mashamba yake yamedhulumiwa kisha akaanza kuiona serikali ni mbaya????? mwache ataipata dawa yake!
 

Vipi ulisha mpeleka mkeo au dadaako nn? hayo yoote hayana ushahidi, kakobe enzi yake walimzushia saana ooh kuna joka kubwa ofcn kwake, anarubuni watu, yako waapi he is still there to date, remeber No right to condemn unless u have a proof, if u have it put it on the table.
 
Kakobe alishinda kwa kuwa anasimamia kweli ya neno na yale anayoyahubili anayatenda .Sasa Mwingira ni zipu kwa mbele!!!.
Unatakiwa uongeze nguvu kumutetea mtu kama Mwingira.
 
Hebu tupeleke taratibu,kwani Mwingira anataka kuipindua serikali na kusimika ufalme ulio juu mpaka serikali imfanyie ujasusi? tuambie msingi wa shutuma zake kwa serikali,nadhani itakuwa jambo rahisi kwake kwasababu ameshaoneshwa filam nzima!

Huyo Mwingira anatakiwa aisaidie polisi ktk upelelezi. Itakuwa ameshaoneshwa nani aliua, nani alirusha bomu, katumwa na nani, saa ngapi, mpango ulipangwa wapi na kwa lengo gani. Tunaoteshwa tu kwenye mambo ya kuwadanganya waumisni but inapokuja kwenye majanga makubwa hamna anayeoteshwa tena ili atuambie ukweli.
 
wonders shall never end
 
Kakobe alishinda kwa kuwa anasimamia kweli ya neno na yale anayoyahubili anayatenda .Sasa Mwingira ni zipu kwa mbele!!!.
Unatakiwa uongeze nguvu kumutetea mtu kama Mwingira.
 
jamaa wanafanya dini biznes sasas hizo ni promotion
HAHAHAHAHAHAHAHA...... Hapo kwa RED....... Hivi jamani Biblia mnazibeba urembo au? Someni Biblia muijue kweli na kuamka kiroho.....

 
mshenzi mwenyewe na mwingira na na viongozi wenyewe
ina maana huyu mwizi katutukana na sisi,, maana kama serikali ni washenzi na wanaongozwa lazima wawe washenzi wanaokubaliana na ushenzi unaofanywa na washenzi......... Mshenzi yeye na yeyote anakubaliana naye..
 
 

ww ni mmbeya tu, huna maana yawezekana ni ww ndo umetumwa na umeambiwa ww ndo mshenzi
 
ww ni mmbeya tu, huna maana yawezekana ni ww ndo umetumwa na umeambiwa ww ndo mshenzi

Mali za Nabii Mwingira zachafua hali ya hewa

Toleo la 2575 Sep 2012
















  • Wanakijiji wadai kukatwa masikio, ‘kubabuliwa' mwili kwa vyuma vya moto
  • Ni shamba alilonunua kwa mamilioni ya shilingi





HALI si swari kwa wanavijiji vya jirani na Shamba la Mifugo la DAFCO-Malonje, mkoani Rukwa lililouzwa kwa Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha, uchunguzi wa Raia Mwema, umebaini.
Baadhi ya wanavijiji hao wanadai wamedhalilishwa na kutendewa vitendo vya kikatili. Kati ya vitendo hivyo ni pamoja na baadhi yao kukatwa masikino na kuunguzwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kutumia vyuma vya moto.
Shamba hilo ambalo liliuzwa kwa Nabii Mwingira kwa zaidi ya shilingi milioni 600 likitajwa kuwa na ukubwa wa hekta 15,000, mbali na Kijiji cha Malonje linazungukwa na vijiji vingine vya Ulinji, Sandulula na Sikaungu, ambavyo vipo Kata ya Molo, Manispaa ya Sumbawanga.
Taarifa za kiuchunguzi zinabainisha kuwa wanaofanyiwa vitendo vya kikatili ni wanavijiji ambao wamekuwa wakipita ndani ya shamba hilo na hata wengine wanaoendesha shughuli za kilimo.
Uchunguzi wa timu ya waandishi wetu umebaini kuwa mtu yeyote hufanyiwa vitendo hivyo bila kujali umri wake wala jinsi. Tayari mwanakijiji mmoja amekwishakatwa masikio na wengine kuadhibiwa kwa kuchaniwa nguo na baadhi kutandikwa viboko.
Katika mlolongo wa adhabu hizo, wamo pia wanaodaiwa kukatwa mapanga, kuunguzwa kwa kutumia vyuma vya moto mwilini. Kasoro iliyojitokeza baada ya uchunguzi wa waandishi wetu kuhusu matukio hayo ni kwamba, sehemu kubwa ya waathirika wa matukio hayo hawakuwa tayari kuripoti katika vyombo vya dola kwa hofu ya kuogopa kuteswa zaidi na baadhi ya walinzi wa shamba hilo.
Mmoja wa wananchi hao ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Malonje, Nuru Togwa (30), amemweleza mwandishi wetu kwamba yeye ni mlemavu kwa sasa, baada ya kukatwa masikio yote mawili kwa wakati mmoja kutokana na kudaiwa kupita ndani ya shamba hilo.

"Kwa sasa ni zaidi ya miaka mitano tangu nilipokutana na ukatili huo ambao sitokuja kuusahau maishani mwangu. Nilikuwa nikitoka Ziwa Rukwa wakati wa asubuhi nikiwa nimebeba kikapu chenye samaki wabichi kuelekea mjini Sumbawanga.

"Sumbawanga ndiko kwenye soko la samaki, lakini nikiwa njiani ghafla watu watano wakanisimamisha na kuniamuru nikae chini. Wakanitaka nitoe maelezo ya kwa nini nimepita kwenye njia zilizoko shambani humo ili hali tayari kuna zuio?

"Lakini kabla hata ya kuanza kujieleza nilianza kupata kipigo kutoka kwa hao walinzi ambao walikuwa na silaha za jadi. Wakanichukua hadi kwenye kambi yao na kuendelea kunipiga na baadaye walinifunga kamba miguuni," anaeleza Nuru Togwa.
Kwa mujibu wa maelezo yake, baada ya kumpiga na kumfunga kamba walinzi hao walimkata sikio kwa kutumia panga. Anadai walimkata sikio moja baada ya jingine kwa panga, naye kubaki katika maumivu makali na alivunja damu nyingi hadi kupoteza fahamu.

"Baada ya hapo naelezwa kwamba nilifikishwa polisi na kisha hospitali ya mkoa kwa matibabu. Baada ya kutoka hospitali niliwekwa rumande kwa kosa la kuiba ngano magunia 40 na siku iliyofuata nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo mjini Sumbawanga.
"Kesi hiyo iliahirishwa kwa zaidi ya mara tisa mahakamani na kisha nami kuachiwa huru kutokana na upande wa walalamikaji kutohudhuria mahakamani kwa muda wote huo wa kesi,"anasema.
Anasema baada ya hapo, hakujua namna gani anaweza kusaidiwa kudai haki yake lakini baada ya siku chache alishauriwa kuwatafuta watumishi wa Kitengo cha Haki za Binadamu mkoani Rukwa na kuwaeleza kile kilichomsibu, lakini hata hivyo, walishindwa kumsaidia kama alivyotarajia.
"Mchumba wangu aliyetarajia kunioa (anamtaja jina), alinikataa na hadi sasa sijawahi kupata mchumba mwingine. Nahisi kuwa mnyonge nisiye na thamani tena ndani ya jamii," anaeleza kwa masikitiko.
Kikongwe naye akumbana na madhila
Si Nuru Togwa pekee katika kadhia hiyo, bali pia wamo wengine akiwamo kikongwe Alesi Maarifa (77) ambaye mwishoni mwa mwaka 2010, alikamatwa na walinzi wa shamba hilo, akatandikwa bakora.

Huyu anasema alikamatwa wakati akipita kandokando ya shamba hilo. Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu, bibi huyo anakumbuka maumivu makali aliyopata akisisitiza "yalikuwa makali sana" kwa kuwa hakuwahi kupigwa kwa muda mrefu katika utu uzima wake.

Kutokana na kutofahamu Kiswahili vyema,katika mazungumzo yake na mwandishi wetu bibi huyo akiwa na mkalimani maalumu anasema; "Nilipigwa na kitu kizito kichwani na kuanguka chini na kubebwa hadi kwenye kambi ya walinzi. Huko wakachukua panga lililopashwa moto kwa muda mrefu, wakanichoma kwenye mapaja, mgongoni na sehemu mbalimbali za mwili wangu.

"Hadi leo nimeachwa na makovu ya kudumu mwilini mwangu kutokana na vidonda vilivyosababishwa na mateso hayo" anasema bibi huyo na kuongeza: "Nilishindwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kutokana na kutokuwa na uelewa wowote wa masuala hayo. Ilibidi nijitibu mwenyewe vidonda kwa kutumia dawa za asili hadi nikapona.

Mwandishi wetu pia alizungumza na Diwani wa Kata ambayo shamba hilo lipo, Festo Mwananjela, ambaye katika maelezo yake licha ya kukiri wananchi wake kuteswa, anasema; "Wananchi hawakushirikishwa kwenye mchakato wa kuuzwa kwa shamba hili, baada ya mwekezaji kukabidhiwa alikuta kuna mazao ya wananchi, lakini aliyaharibu bila ya kuwalipa fidia.
"Njia ambazo awali zilikuwa zikiunganisha kijiji kimoja na kingine kupitia shamba hilo zikafungwa na yeyote anayepita katika njia hiyo ya awali anakamatwa na walinzi na kisha kuteswa."
Taasisi ya Haki za Binadamu
Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Mkoa wa Rukwa, Dk. John Masiya, anazungumzia suala hilo kwa kukiri kufikiwa na malalamiko ya wanakijiji hao kuhusu mgogoro huo wa ardhi.
Kwa mujibu wa Dk. Masiya, katika malalamiko yao wanakijiji hao wanadai kukatazwa kulima kwenye mashamba yao ya awali yaliyopo ndani ya shamba la DAFCO na walimwandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga wakati huo, Meja (mstaafu) Bahati Matala.
"Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilishauri suala hilo lishughulikiwe na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, lakini sikuwahi kupokea malalamiko kuhusu watu kupigwa, kuchomwa moto na wengine kukatwa masikio," alisema Dk. Masiya.
Kauli ya Naibu Waziri Mwanri
Serikali, kupitia kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, hivi karibuni iliagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kushughulikia kero zote zinazowahusu wananchi wa vijiji hivyo ndani ya mwezi mmoja.
Kati ya hatua zilizopendekezwa na Mwanri ni pamoja na na kupitiwa upya mkataba wa mauziano ya shamba hilo la mifugo la DAFCO ili kubaini ukiukwaji wowote wa mkataba baina ya pande mbili husika.
Mwanri akiwa ziarani mkoani Rukwa hivi karibuni alidai agizo la kupitiwa upya kwa mkataba huo linazingatia ukweli kwamba mwekezaji aliyenunua shamba hilo amebadili matumizi ya eneo hilo. Kwa mujibu wa Mwanri, badala ya kuendesha shughuli za ufugaji sasa mwekezaji huyo analima mazao mbalimbali kinyume cha mkataba.
Mwanri anasema; "Serikali haiwezi kuvumilia kuona wawekezaji ambao wamekuwa wakiidanganya. Kuna haja ya kupitiwa upya kwa mkataba huo vinginevyo kama atakuwa ameshindwa kutimiza masharti mkataba huo usitishwe mara moja".
Hata hivyo, tayari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya ameunda tume kwa ajili ya kushughulikia kero hizo baina ya wananchi wa vijiji hivyo na mwekezaji huyo, lakini ni zaidi ya miezi miwili sasa imepita huku majibu ya tume hiyo yakiendelea kusubiriwa kwa hamu na wananchi ili hatimaye kuhimitisha mgogoro huo uliodumu kwa miaka kadhaa sasa.
Msimamo wa Efatha Ministry
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mkoa wa Rukwa wa Efatha Ministry, Mchungaji Michael Meela, alimweleza mwandishi wetu kwa njia ya simu kwamba, hafahamu kuhusu watu kufanyiwa udhalimu wa aina yoyote.
Mchungaji huo anasema anachokijua yeye ni kwamba walinzi wake katika shamba hilo wamekuwa wakipigwa na wanakijiji na zaidi ya hapo, kesi za kupigwa walinzi zimekuwa zikiripotiwa Polisi. Hata hivyo, hakufafanua kuhusu idadi ya kesi ambazo zimeripotiwa.
"Suala la kero zinazodaiwa kuwapo katika vijiji vinavyolizunguka shamba hilo ni masuala ya kisiasa ambayo hayana tija yoyote kwa Efatha," alisema mchungaji huyo.
Msimamo wa polisi Rukwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, amemweleza mwandishi wetu kwamba taarifa zilizoripotiwa kwake hivi karibuni zinahusu walinzi wa shamba hilo kuporwa silaha na baadhi ya wanakijiji pamoja na wizi wa ng'ombe wawili wa mwekezaji huyo. Anasema uchunguzi kuhusu matukio hayo unaendelea.
"Jambo jingine ninalofahamu ni kuibuka kwa uhasama mkubwa kati wananchi wa vijiji vinavyozunguka shamba hilo na walinzi wa DAFCO, lakini hakuna taarifa ya watu kalalamika kuhusu kupigwa wala kufanyiwa vitendo vyovyote vya kikatili na kumsababishia ulemavu wa maisha.
"Polisi wapo kwa ajili ya kusikiliza watu wote hivyo kama kuna vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi na kufanyiwa unyama wa aina yoyote ile, wajitokeze na kutoa taarifa ili vyombo vya dola viweze kushughulikia na hatimaye sheria kuchukua mkondo wake," anasema Kamanda Mwaruanda.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…