Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Tunacho fail? Kwamba na mimi nimo? Ahahah mkuu hapo unanionea... Lakini pia tukirudi kwenye mada, kuna vitu vingine hivi vyombo haviwezi kuingiliana kwa sababu za kiusalama zaidi..
Hahahahaha!!! Ni kweli lakini kwa awamu hii matukio hayo yamekuwa mengi sana!! Halafu inachotia shaka, ni baada ya wanaharakati, wanasiasa, kuwa wanatekwa, ovyo ovyo!! Kweli dunia nzima haya mamboyapo, lakini hapa kwetu yanafanywa kishamba sana!!
 
Inshu hapo sio kuwa na passport, au huwa ana kwenda wapi, mnacho fail, ni kitu kidogo tu, njia za ukamataji, kwani ukiwatuma polisi wakaenda mchana tu, na kumkamata, na taratibu nyingine zikafuata, kuna tatizo? Kwani serikali zote huko nyuma hakukuwa na watu kama hawa?lakini approach haikuwa hii!! Ilani njia moja ya serikali zile zinazotisha wananchi!! Halafu unasikia viongozi wa dini wanatoa mapambio ya kusifia tu ili mambo yao yanyooke tu!! Bora yeriko nyerere anayeabudu mizimu ya mababu.
Si umesikia mchana anakuwa kwenye kazi zake,ndo maana wanaenda usiku
 
Majibu ya serikali ni ya jumla kwamba mpaka wahusika yani watekwaji, wapoteaji watakapofika wenyewe ktk vituo vya polisi na kufungua kesi ndio jeshi liingie kazini yani kuwatafuta watekaji ama wapotezaji. Umemuelewa Siroo mkuu?
Shame shame sana kwa yanayoendelea nchini now.

Hivi pamoja na doa la kupotea Ben Saanane na Azory Gwanda bado haya mambo yanaendelea na hakuna majibu ya serikali?
 
Si umesikia mchana anakuwa kwenye kazi zake,ndo maana wanaenda usiku
Hata kama ni usiku, si wanakwenda polisi, na kuwaambia ndugu, kesho njooni kituo fulani cha polisi, sasa polisi, hawajui nao!!
 
Wait a minute, yaani machinga ana hati ya kusafiria ?? ( Passport)?? kuna harufu ya jambo hapa.
acha ujuha kwani mmachinga hana haki ya kupata hati ya kusafiria? nyie watu mna matatzo sana,
 
Machinga ana hati ya kusafiria..! I wish ningeishika hiyo hati niangalie mihuri... Then ndio tutajua machinga kweli au lah na ana la kueleza au lah..
Acha kukremu mkuu.
Kwani passport inachagua mtu?Passport ni haki ya kila mtanzania.
 
Nchi hii si salama kabisa, ajabu kuna" viongozi" wa dini wamejiunga na wanasiasa kuimba kusifu na kuabudu, yaani huyu yale mauaji yaliyotokea mpakani na msumbiji yatamuhusu, utaambiwa amevaa kanzu na ana mzuzu huyu ni gaidi...TZ pole sana nchi yangu.
 
Wait a minute, yaani machinga ana hati ya kusafiria ?? ( Passport)?? kuna harufu ya jambo hapa.

Katika maisha ya binadamu kubadilisha kazi mpaka mara saba katika uhai wako ni jambo la kawaida
Kama alikuwa na maisha mazuri zaidi hapo mwanzo
Kuwa na passport ni jambo la kawaida sana hata mtoto wangu wa miaka miwili anayo
 
Kwa akili za haraka haraka uko sahihi Mkuu
Hamna cha akili za haraka haraka.

Kama ana makosa, zipo taratibu za kuwakamata watu na wanakamatwa na Polisi.

Cha msingi kwa sasahivi polisi ichukue jukumu la kumtafuta kwa kushirikiana na familia yake.Wasiishie tu kusema,"Sisi hatujamkamata".
 
Hamna cha akili za haraka haraka.

Kama ana makosa, zipo taratibu za kuwakamata watu na wanakamatwa na Polisi.

Cha msingi kwa sasahivi polisi ichukue jukumu la kumtafuta kwa kushirikiana na familia yake.Wasiishie tu kusema,"Sisi hatujamkamata".
Uko very far na kujua jinsi mambo yanavyoenda... Jiongeze Mkuu!
 
Amechukuliwa usiku wa manane na watu waliojitambulisha kwamba ni askari ambao walikataa kutoa vitambulisho, sasa kwa nini wanafamilia walisubiri siku nne? Kwanini hawakuanza kufuatilia usiku huo huo? Siku hizi kuna simu za mkononi Je, walianza hizo pilika pilika na kuuliza?

Post ya Zito inaonyesha kwamba TISS wanahusika, Je, anao ushahidi?
Kwani amewataja Tiss?
 
Hivi kwa nini polisi wasijitokeze hadharani na kuukana huu utaratibu wa kuvizia watu usiku wa manane kwenye nguo za kiraia.

Kwa nini isiwe kama zamani polisi wakija kukamata mtu lazima uongozi wa mtaa husika uambatane nao maana hapajitikezi hata majibizano ya risasi kwenye hizi kamatakamata.

Kama polisi hawahusiki basi wanailea hii tabia.

Hata ukioneshwa kitambulisho cha polisi utajuaje kama ni valid? Wangapi mmewahi hata kuviona hivyo vitambulisho before?
 
Back
Top Bottom