Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Kilichonishangaza humu ni watu kushangaa machinga kumiliki pass ya kusafiria kweli ccm mbele kwa mbele.
 
Amechukuliwa usiku wa manane na watu waliojitambulisha kwamba ni askari ambao walikataa kutoa vitambulisho, sasa kwa nini wanafamilia walisubiri siku nne? Kwanini hawakuanza kufuatilia usiku huo huo? Siku hizi kuna simu za mkononi Je, walianza hizo pilika pilika na kuuliza?

Post ya Zito inaonyesha kwamba TISS wanahusika, Je, anao ushahidi?
Hina maana hakusindikizwa na mke wake au hata mtoto wake mmoja
 
Tatizo ni kwamba wanateka wanajulikana na bado wanatamba mitaani

Solution ni kudeal na ndugu zao
Uyo ajatekwa watu wakija nyumbani kwako wakikuchukua ni kutekwa?
 
Kuna sheikh alichukuliwa msikitini huko miaka kadhaa iliyopita wakamtesa hadi kumtia upofu
Huu uwendawazimu wa kuteka na kuumiza watu kwenye awamu hii hauna tofauti na nyakati za Maliyamungu wa Uganda, Ni aibu kubwa sana haya mambo ya kinyama na uonevu.

FREE MWINYI KATUNDU
 
..hili suala hata Mzee Mwanakijiji aliwahi kulitahadharisha jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.

..kumezuka tabia ya Polisi kuvaa nguo za kiraia, kubeba silaha za kivita, na kutekeleza majukumu ya jeshi la Polisi.

..Utaratibu huo mpya ndiyo unaotoa mwanya wa kufanyika hayo yaliyomtokea mhusika anayedaiwa na Zitto kuwa ametekwa na wanausalama.

..Itafika mahali wananchi watashindwa kutofautisha kati ya Polisi na majambazi.
Kwanini unam reference Mzee Mwanakijiji ? Wewe unadhani anapinga uonevu wa raia? Acha hizo na wewe nilikuwa nikikuheshimu.
 
Na kuna watu wamechinjwa huko juzjuzi tu ila zito haku tweet, ila huyo machinga na passport yake katweet, sasa mmoja ana faida kuliko wengi, au hao waliowachinja hao anawajua?
Zito is a disgrace.
 
Machinga hana uwezo wa kunua? Hastahili kununua Mali anayo taka na kuimiliki? Je ndg zake hawa ruhusiwi kumsaidia? Kumnunulia ? Kumjengea? Ukiwa machinga hutakiwi kufanya maendeleo?
Rudia kusoma uliyoandika na palipoandikwa haruhusiwi ktk niliyoandika. We si shahidi wa huyu ana kitambulisho cha machinga cha 20,000/= yaani hana uwezo wa kulipia kodi ya biashara yake bali uwezo wa kulipia kodi ya moko wake na uwezo wa kusafiri ughaibuni😂😂
 
Hii siyo sawa, ni uonevu wa wazi
Jeshi la polisi siyo jeshi la Utekaji na kupoteza watu ni jeshi la kulinda watu

Usalama wa Taifa ni pamoja na usalama wa wananchi

Free Mwinyi Katundu
 
Kuna MTU anamjua huyu Mwinyi Mkuu atupe Japo maelezo yake kdg hapo mtaani ?

Yaani historia fupi khs yy
 
Back
Top Bottom