Mwisho wa CCM umefika na hata 2025 Rais Samia hatokuwa Mgombea wa CCM

Mwisho wa CCM umefika na hata 2025 Rais Samia hatokuwa Mgombea wa CCM

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Yanayoendelea ndani ya CCM ni mapigo ya mwenyezi Mungu kwa CCM na viongozi wake. Wataendelea kuvurugana na mwisho wa siku chama kitapasuka mapende kadhaa.

Mama hatoweza kuihimili na hata dola haitafua dafu kutuliza yatayotokea ndani ya CCM kuelekea 2025.Mama atalazimika kuachia ngazi 2025 katika harakati za kutuliza mivitano ndani ya chama chake ili kuokoa chama ingawa haitosaidia.

Yote haya ni matokeo ya uovu wa miak nenda miaka rudi na sasa Mungu kasema basi imetosha.

Tutaendelea kuona watu wakijiuzulu na wengine kulazimishwa kujiuzulu kuanzia sasa na kuendelea.

Ndugai kaafungua tu pazia la league ya watu kujiuzulu.

NB: Mama akibahatika kupenya, basi CCM itakwenda kufanya vibaya sana katika uchaguzi wa 2025 kuliko wakati wowote ule.

Time will tell.
 
Samia ameonesha tamaa kubwa sana na Urais wa 2025, ameshanogewa na ikulu, na yote anayofanya sasa ikiwemo kule "kumsuta" Ndugai alikuwa anajitengenezea njia yeye japo akatumia kivuli cha "najenga nchi" ili kuwadanganya wajinga.

Hata hiyo timu ya mawaziri aliyosena anataka aende nayo sio kwa ajili ya kujenga nchi kama anavyodai, ni kuteua wanaomuogopa ili awe huru kuelekea 2025.

Kwa level ya kiwango cha tamaa alichoonesha ikiwemo kuanza kuwapanga wanawake wenzake, huku akiwafunga midomo wapinzani wake kwa njia mbalimbali ikiwemo "kuwachamba" ikulu, sitegemei aachie hiyo nafasi kirahisi.

Simply anajijua ni dhaifu na anayeogopa ushindani asie na mbinu zozote kisiasa, ndio maana anatishia kuwatumbua anaowahisi kuutaka urais wa 2025, au atawatumbua kabisa, kusudi abaki peke yake kama mgombea pekee akiwa amezungukwa na kundi la wanaomuunga mkono, huyu nae ni dikteta tu.
 
Wakuifikisha hiyo ccm mwisho ni nani? Hawa hawa wanaoshangilia Hangaya kumchamba spika baada ya kutoa maoni yake kuhusu mikopo?
 
Yanayoendelea ndani ya CCM ni mapigo ya mwenyezi Mungu kwa CCM na viongozi wake. Wataendelea kuvurugana na mwisho wa siku chama kitapasuka mapende kadhaa.

Mama hatoweza kuihimili na hata dola haitafua dafu kutuliza yatayotokea ndani ya CCM kuelekea 2025.Mama atalazimika kuachia ngazi 2025 katika harakati za kutuliza mivitano ndani ya chama chake ili kuokoa chama ingawa haitosaidia.

Yote haya ni matokeo ya uovu wa miak nenda miaka rudi na sasa Mungu kasema basi imetosha.

Tutaendelea kuona watu wakijiuzulu na wengine kulazimishwa kujiuzulu kuanzia sasa na kuendelea.

Ndugai kaafungua tu pazia la league ya watu kujiuzulu.

Time will tell.
Matope!!! Kuna makundi kama kipindi cha jk? Kalale huko ukue
 
Samia ameonesha tamaa kubwa sana na Urais wa 2025, ameshanogewa na ikulu, na yote anayofanya sasa ikiwemo kule kumchamba Ndugai alikuwa anajitengenezea njia yeye japo akatumia kivuli cha "najenga nchi" ili kuwadanganya wajinga.

Hata hiyo timu ya mawaziri aliyosena anataka aende nayo sio kwa ajili ya kujenga nchi, ni kuteua wanaomuogopa ili awe huru kuelekea 2025.

Simply anaogopa ushindani ndio maana anawatishia kuwatumbua wanaoonesha dalili za kuutaka urais wa 2025, au atawatumbua kabisa kusudi abaki peke yake kama mgombea akiwa amezungukwa na kundi la wanaomuunga mkono.
Ulitaka afanyaje sasa? Awaaache waendelee kumharibia njia yake? Siasa ni ulevi kama ulivyo ulevi mwingine once unapoingia hutaman kutoka! Hata angesema atumikie miaka hii mitano bado msingekosa la kusema?! Mama safisha njia kanyaga twende 2025 tuko na wewe !!
 
Back
Top Bottom