Mwisho wa CCM umefika na hata 2025 Rais Samia hatokuwa Mgombea wa CCM

Hapo kwenye kusema eti Mungu ameweka mkono wake, ni uongo.
 
Hilo liko wazi, akishamaliza kazi yao ataenda, na hatokaa TZ atapewa kazi UN au World Bank, lkn mpaka hiyo siku ifike tayari tanesco itakuwa imeshagawiwa bure kwa foreigners, Migodi yote ya Cobalt, Gas etc …
 
Utaratibu wa CCM ni kuwa raisi atatoka bara alafu Makamu atatoka Zanzibar
Huu ndio utaratibu wa CCM, na unaheshimiwa sana
 
Tamaa mbele mauti nyuma! Kama alishindwa Bosi wake, hata yeye atashindwa tu. Siku zote muda ni rafiki mzuri sana.
 
Mkuu, CCM itashindwa 2025 kwa upinzani upi imara?

Au una maana CCM original itashindwa na itayokuwa CCM mpya baada ya kuparaganyika?
 
Kwa sababu wanakupa kula eti?!

Watanzania tulivyo ji-tune hata asipokuwepo kiongozi yeyote ngazi za juu tuta-survive shida ni kwenu nyie mliochomekwa chomekwa kwenye vitengo na baba zenu makada kuona bila hili dubwana CCM hakuna maisha.
Siku hizi watu wanajitaftia rizki hawajali mapato wala matumizi,wakope,wasikope shauri yao,na kwa kifupi tayari watu wamejianda kujitegemea,angalia uchaguzi watu hawajitokezi wanapambana na hali zao za kipato
 
Muda utaongea......ngoja tuendelee kula mtori nyama ziko chini
 

 
Kazi IPO !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…