Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Kati ya vitu vya kijinga serikali inaenda kufanya kwa watu wake ni kuua soko la Kariakoo kwa kuruhusu gulio la Wachina Kurasini ili wauze bidhaa zao bila kodi na kodi ikusanywe pale tu bidhaa inapotoka.

Hizi akili itakuwa kazitoa Mwigulu lakini ikitokea hili limefanikiwa basi Kariakoo haitakuwa na watu tena. Wachina tunawajua wanauza mpaka miwa wale na bei yao hutaweza kushindana nao kwa sababu wanapewa backup kubwa na Serikali yao.

Tuwe tunafikiria kwa kutumia kichwa.
 
Kati ya vitu vya kijinga serikali inaenda kufanya kwa watu wake ni kuua soko la kariakoo kwa kuruhusu gulio la wachina kurasini ili wauze bidhaa zao bila kodi na kodi ikusanywe pale tu bidhaa inapotoka...
Sisi wananchi tunachotaka ni bidhaa kwa bei ya chini nyie madalali mtajijua dunia ni soko huria, Kariakoo walijaa Wachagga wezi wezi tu kuibia WATU wasiojua bei acha wachina wawavunde tena Serikali iwahi haraka

USSR
 
Kati ya vitu vya kijinga serikali inaenda kufanya kwa watu wake ni kuua soko la Kariakoo kwa kuruhusu gulio la Wachina Kurasini ili wauze bidhaa zao bila kodi na kodi ikusanywe pale tu bidhaa inapotoka...
Ni vema iwe hivyo ili kiwake zaidi moto uwe mkali wamesema wana agano na Mungu hawatatoka
 
Wanaibia wanunuzi na serikali kwa ujumla kwa tamaa ya faida kubwa isiyoendana na huduma (bidhaa). Mfano kiatu anauza 50,000 apate faida ya 15,000 nje ya kodi. Kiatu hichohicho nikiagiza china kinagharimu 30,000 kila kitu hadi nakivaa
Nadhani hujawahi kuwa mfanyabiashara. Maelezo yako hapo yanatosha kujua kuwa pengine hujawahi kuuza hata pipi.
 
Back
Top Bottom