Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Mkuu, kila kitu ni udhibiti, halafu hakuna mtu anakuja tu puup ajenge kiwanda, watakuja watauza watakapoona soko ni zuri kuna watakaoshawishika kujenga viwanda ila lazima wafanye biashara kwanza, watengeneze soko. Maendeleo ni hatua.Wachina unawajua au wawasikia?
Wale wanatakiwa waje Tz kujenga viwanda na si vinginevyo
Mchina akileta bidhaa kutoka china akaziuza hapa kwa jumla ni nafuu kwa mfanyabiashara wa kitanzania kuliko akiufata mzigo china. Hata bei zitakuwa za kiushindani na kupelekea unafuu kwa mtumiaji wa mwisho. Hatuwezi jifungia watanganyika tu milele, lazima tufunguke halafu tuweke mifumo ya udhibiti. Kuna tofauti kubwa ya Dar na Moshi au Iringa sababu watu wa dar waliruhusu wageni, leo dar kila mtanganyika anataka kwenda.
Imagine bidhaa zinazohitaji vifungashio bora kama utavipata kiwepesi hapa badala ya kuviagiza China itakavyoboost wenye viwanda vidogo vidogo huko mikoani. Sasa hivi mmakonde kapambana kafungua kakiwanda kake ka kupaki unga kilo moja moja huko umakondeni vifungashio mpaka aagize China na hiyo exposure hana.