Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Yule mzungu wa Afrika Kusini alisema "Mwafrika bado sana kujitawala" aliona mbali. Ukimpa mtu kazi kubwa kama uwaziri anaanza na kupiga madili tena ya kijinga!.
 
Kati ya vitu vya kijinga serikali inaenda kufanya kwa watu wake ni kuua soko la Kariakoo kwa kuruhusu gulio la Wachina Kurasini ili wauze bidhaa zao bila kodi na kodi ikusanywe pale tu bidhaa inapotoka.

Hizi akili itakuwa kazitoa Mwigulu lakini ikitokea hili limefanikiwa basi Kariakoo haitakua na watu tena. Wachina tunawajua wanauza mpaka miwa wale na bei yao hutaweza kushindana nao kwa sababu wanapewa backup kubwa na Serikali yao.

Tuwe tunafikiria kwa kutumia kichwa.
Kichwa kipi sasa tutumie kufikiri?

Kama jambo hilo litatekelezwa mimi nipo fifty fifty kwa uhalisi wa hoja yako!

Wachina wakimwaga ma fake yao hapo, machinga si ndiyo wataenda kuhemea na bei itakuwa ni ya kutupwa?

Kama serikali itakusanyia kodi zake hapo, nadhani wameshajipanga namna ya kudhibiti makusanyo yao, tatizo liko wapi?

Ninaelewa kuwa mkiwa na vitu vingi vya aina moja, mfano wa hayo masoko, kuwe na Kariakoo 5 ama zaidi za namna hiyo katika jiji la Dsm, si kutakuwa na ushindani wa maana sana na kupunguza msongamano usio na tija na ndiyo maendeleo hayo.

Wewe umesikia la Kurasini, mimi nimesikia la stand ya zamani ya Ubungo, embu ongelea na hilo sasa!
 
Siyo ujinga. Monopoly ni mbaya kwa mteja na competition ni nzuri.

Kama Wachina watauza kwa bei ya chini bidhaa zile zile ni heri kwa mteja. Na hilo ni jambo jema...

Turuhusu competition ya watoa huduma na makampuni. Ndivyo mambo yalivyo huko nchi za wenzetu. Monopoly ni adui!
Ni kweli, vitu vitashuka bei kiasi. Advantage kwa mlaji
 
Consumer hatuna wasiwasi ila seller.
Anyway ngoja tuone
 
Kati ya vitu vya kijinga serikali inaenda kufanya kwa watu wake ni kuua soko la Kariakoo kwa kuruhusu gulio la Wachina Kurasini ili wauze bidhaa zao bila kodi na kodi ikusanywe pale tu bidhaa inapotoka.

Hizi akili itakuwa kazitoa Mwigulu lakini ikitokea hili limefanikiwa basi Kariakoo haitakuwa na watu tena. Wachina tunawajua wanauza mpaka miwa wale na bei yao hutaweza kushindana nao kwa sababu wanapewa backup kubwa na Serikali yao.

Tuwe tunafikiria kwa kutumia kichwa.
Hakuna kitakachoua kariakoo, uko kote unakokutaja hapako connected kama kariakoo
 
Lile soko lililotakiwa kujengwa pale Ubungo kituo cha zamani cha mabasi limefika wapi?
Washa anza kujenga, sio soko la kawaida wanaita east Africa trade and logistics centre, ukipita pale utaona wameanza kuchimba na wamezungusha mabango ya mradi utakavyokuwa ukikamilika
 
Tuache mihemko, Duniani kote kwenye nchi zilizoendelea magulio yapo kila kitongoji.

Tusikariri maisha kwamba lazima watu wote wajazane Kkoo..

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Hasa ukizingatia kwa sasa kariakoo ina kila sababu ya kubaki juu. Iko centre usafiri wote unaenda kariakoo toka kila sehemu ya mji, biashara ipo tayari, na soko ndio kwanza linaendelea kujengwa upya kwa ukubwa zaidi
 
Sijajua kwanini watanganyika tunaogopa sana ugeni. Wachina wakija na bidhaa zikawa bei nafuu wateja hawatakuja kutoka mikoani tu, hata nchi jirani wanaweza kuja kwa wingi. Mikoani pia biashara zitachangamka.

Cha msingi soko liwe na ukuta, kuingia bure ukitoka na mzigo clearance ifanyike serikali ipate. Huduma ziwe ni kwa jumla, serikali ya soko iwe na database ya maduka yote humo ndani na bidhaa inazouza.
N tena hao wachina watakuwa wanauza kwa bulk kubwa zaidi, itafanya zile safari za China kupungua, watu hao wa Kariakoo pia watanunua mzigo kurasini
 
Nilipokua mdogo Niliwahi kujiuliza hivi, pale kariakoo kuna maduka zaidi ya mia na yote yanauza nguo za aina moja, wanapataje faida? Wakanijibu wakasema wasingekua wanapata faida wangeshafunga. Wateja hawaishi. Na mimi najibu leo, wateja hawaishi. Sisi tunataka unafuu
 
Nguo tunazouziwa toka china kwa 25-30k huko china zinauzwa si zaidi ya buku tatu pesa ya kitanzania
Sehemu gani ya China mkuu niende huko?
Nafanya biashara ya kuuza nguo kwa takribani miaka 18 sasa, na ninaenda China mara kadhaa, please nielekeze hilo chimbo.
 
Nguo ya elfu 10 wanakwambia sh elfu 35

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Nadhani huijui biashara.
Nguo nyingi zinazouzwa soko la kkoo huwezi kuzikuta kwenye masoko ya China, uagizwa kwa oda maalumu kwenye viwanda vidogo vilivyopo huko Xintang China. Wafanyabiashara wa nguo wa jumla faida yao ni kati ya tsh 400-3000 kwa pisi moja ya nguo
 
Back
Top Bottom