Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Wachina wapewe wajenge Bandari Kavu pale Tunduma Mbeya na Isaka Shinyanga Ili Wacongo, wamalawi, Zambia, zimbabwe, burundi, Rwanda,sudan, Uganda, Central Afrika,Nk waache Kwenda China. Bidhaa zote wanunue Tunduma au Isaka. Hii itachochea Sana uchumi.
Matajiri wetu hawa wa ndagu hawana ubunifu wowote wa kubuni miradi mikubwa ya kimkakati. Wao wanachojua ni kutoa kafara tu na sio kubuni megaproject.
Huwezi ukawa mshirikina then uwe na akili ya kubuni.
Hakuna matajiri nchi wote hawa ni madalali wajanja wa janja, utajiri wa manyoka, thus hawana akili ya kucheza na fursa tele nchini wakashindana na Wachina. Ndumba upunguza uwezo wa kufikiri.
 
Safi sana kama China imehamia kwetu maana na hela za kigeni zitaongezeka

Tena wapewe ekari 10,000 kabisa wajenge mji wao kabisa liwe soko kubwa Africa, na wanunuzi waje tu

Ni akili kubwa kwa wenye uelewa
Miji mingi US ina china town...hadi new york kuna Chinatown
 
Sasa ka mall kama hako ndio kaue Kariakooo?
Kkoo itakua kwa sababu kutakua na bidhaa nyingi zinapatikana kiurahisi hapa nilipo pana Mall za Wachina zaidi ya Sita ndio zinafanya mzunguko mkubwa wa fedha hapo Bree Street na hapo hapo pia pana maduka makubwa ambayo walanguzi wanaita Chimbo chochote atakachohitaji mteja anakimbilia Chimbo..Kadeti ya ukweli inauzwa rand 100 huko chimbo kama 14,000 Tzh au Jean ni rand 100 mpaka 200 nzuri kabisa...
 
Miji mingi US ina china town...hadi new york kuna Chinatown
China town ni tofauti na ninachoongelea
China town hata London ipo na ninapita sana
China town ni wao na biashara zao na communities zao kwa ujumla

Mimi naongelea bidhaa zinazotulenga sisi waafrika na sio vyakula vyao
Kuwa na viwanda
 
Back
Top Bottom