Tuombe tu vita isije upande wetu tena tukakutana na watu wanaotumia teknolojia kupambana.Russia haina precision weapons nyingi kwani zina gharama kubwa, kitu chochote kikishakuwa cha gharama kubwa usitarajie Urusi ikipendelee. Wala precision missiles zake sio better, Israel ndio nchi inapenda zaidi na inajua vizuri precision.
Russia ina silaha kadhaa nzuri ila namba zinakataa. Su-35 hazifiki 200, kwa US multirole yake mpya F-35 zipo zaidi ya 400. Hapo hatutaji F-16 ambazo ni nyingi zaidi na ni level za Su-35.
Russia kwenye drones hawazidi US, China, Israel wala Turkey. Hao wanne ndio wanaanza na hakuna mpinzani wao soon, wanafuata kina Russia na Iran na wengineo.
Rwanda wanajipanga kwenye precision weapons na silaha za kisasa ukilinganisha na bajeti yao, population na ukubwa wa ardhi yao jeshi lao linajitahidi. Tanzania iko kivyake inaishi
Tumebakiwa na jina/sifa ila utendaji sidhani, mishahara/malipo na siasa yameondoa ufanisi.