Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Najua habari hii imewauma sana makamanda ninawafahamu wa JWTZ!

Najua habari hii imemuua sana kamanda Luteni Generali Mstaafu Mwakibolwa. Najua habari hii imemsononesha sana General Mstaafu Davis Mwamunyange. Najua habari hii haijamlaza vizuri mwamba Luteni General Abdulrhman Shimbo.

What we use to know as Tanzania Pride iliyokuwa inabebwa na Jeshi letu la Wananchi (Tanzania People's Defence Forces) imefikia tamati baada ya wanajeshi wetu kudhalilishwa huko Rwanda kwa kusubilishwa kwa masaa mpakani na Wanajeshi (Mamlaka za Rwanda).

Wanajeshi wetu waliosubilishwa mpakani ni sehemu ya majeruhi wa vikosi vya SADC waliopokea kichapo kutoka kwa Wanajeshi wa Rwanda na Washirika wao M23.

Inasemwa pia Wanajeshi wetu kama sehemu ya wanajeshi wa SADC wamenyang'anywa silaha zao na wanamgambo wa M23 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Hawawezi fanya chochote bila ruhusa ya M23.

Itakumbukwa hadi miili ya Wanajeshi wetu waliouwawa bado haijarudishwa na inawezekana jamaa wanatuwekea ngumu ili tuendelee kuwalamba miguu na ili watuoneshe kuwa sasa wao ndo mabwana zetu kivita.

Naumia sana Nchi yangu kufikia hapa. Naumia sana Jeshi langu JWTZ kufikia kudhalilishwa hivi.

Kuna haja ya kujitafakari na kuanza upya. CCM ni janga.
Screenshot_20250225_110330_Facebook.jpg

=======

Takriban wanajeshi 200 wanaohitaji wakihitajihuduma ya matibabu wakiwemo wale wa Afrika Kusini, Malawi na Tanzania walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC waliondoka Goma na kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kuelekea Kigali kwaajili ya kupata ndege za kuwarejesha makwao.

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza wikendiiliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.

Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda,ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwayamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.

g

Walifika mpakani Jumatatu saa sita mchana, na waliondoka mpakani baada ya saa kumi na mbili jioni, Donatien anasema.

Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani.

Vyombo vya habari vya Goma - jiji linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.
Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.
 
Hawa waasi wanatubipu.
Wamewarejesha wanajeshi wetu wa JWTZ nyumbani kupitia Rwanda bila silaha.

Walipoulizwa kwanini wanawafanyia hivyo, wakajibu Sila zote walizokuwa wanatumia Goma ni za Umoja wa Mataifa sio za Tanzania.
Cha ajabu wao hutumia silaha hizo kuteka maeneo mashariki mwa Congo.

Je wanajeshi wetu hawakubeba hata silaha zetu chache wakati wakitoka huku kwenda Congo?

Source: BBC Swahili news.
 
Picha iko wapi
 
Tetesi : umbea , habari zisizo na uhakika, kujitungia story za vijiweni?
 
Hawa waasi wanatubipu.
Wamewarejesha wanajeshi wetu wa JWTZ nyumbani kupitia Rwanda bila silaha.

Walipoulizwa kwanini wanawafanyia hivyo, wakajibu Sila zote walizokuwa wanatumia Goma ni za Umoja wa Mataifa sio za Tanzania.
Cha ajabu wao hutumia silaha hizo kuteka maeneo mashariki mwa Congo.

Je wanajeshi wetu hawakubeba hata silaha zetu chache wakati wakitoka huku kwenda Congo?

Source: BBC Swahili news.
Hilo haliwezekani maana huwezi kuwafanyia wanajeshi walio chini ya umoja wa mataifa kitu kama hicho hutakuwa hujipendi kabisa..

Alafu thread yako inaonyesha uelewa wako wa mambo baro upo chini.
 
Hilo haliwezekani maana huwezi kuwafanyia wanajeshi walio chini ya umoja wa mataifa kitu kama hicho hutakuwa hujipendi kabisa..

Alafu thread yako inaonyesha uelewa wako wa mambo baro upo chini.
Kwenye vita unazungumzia Wanajeshi wa umoja wa kimataifa wewe Mzee mwenye uelewa mkubwa inakuaje wanajeshi wa Umoja wa mataifa wanauawa na wengine wanarudishwa na majeruhi wanaenda kutibiwa SA wengine Tanzania wewe mwenye uelewa Mkubwa kwa nini hao wanajeshi wanakua na siraha nao huko vitani?
 
Hawa waasi wanatubipu.
Wamewarejesha wanajeshi wetu wa JWTZ nyumbani kupitia Rwanda bila silaha.

Walipoulizwa kwanini wanawafanyia hivyo, wakajibu Sila zote walizokuwa wanatumia Goma ni za Umoja wa Mataifa sio za Tanzania.
Cha ajabu wao hutumia silaha hizo kuteka maeneo mashariki mwa Congo.

Je wanajeshi wetu hawakubeba hata silaha zetu chache wakati wakitoka huku kwenda Congo?

Source: BBC Swahili news.
Jeshi letu inabidi lijitafakari. Kama ni kweli limeingiliwa na wanasiasa wa CCM hadi kulifanya lishindwe ku focus kwenye masuala ya msingi hadi kufikia linadharirika hivi basi kuna haja ya kufanya yale aliyofanya General Sani Abacha kule Nigeria mwaka 1993
 
Back
Top Bottom