Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Ivi tunafaidika na nn kama nchi?
 
Tanzania kamwe haiwezi kuwa dhaifu kwa Rwanda.

DrC ni mission tofauti sio vita kamili baina ya Tanzania na Rwanda.
 
Sidhani hizo stori zina ukweli, huko insta kuna stori ya M23 kupukutishwa Goma na video ya mrundikano wa silaha zao huku kamanda wa DRC akisifu operesheni yao. Mwizi anakimbizwa kimya kimya kelele ni za waasi wenye nchi yao wanafanya actions tu. Muda si mrefu DRC itarudisha kila sentimita inayokaliwa na waasi.

Propaganda ni kubwa kuwakuza M23 kuliko uhalisia wa mambo, kwani wale madereva wa tz waliokwama Goma kwenye mapigano si wote walitoka salama kupitia operesheni ya JWTZ? Hao M23 walikuwa wapi kuzuia JWTZ?

Tuache kusifia wajinga kakikundi cha M23 hawana uwezo wowote tukikumbuka 2013 walivyofekwa, ni vile tu JWTZ hawajaamua tu kuingia vitani, JWTZ wakiamua kuwashughulikia siku moja haitaisha M23 watakufa wote na stori yao itaishia hapo.

Angekuwa Rais mkwere muda huu tayari M23 washarudishwa kwao Rwanda sababu utawala wao kule Goma ni janga kwa uchumi wa tz sijui Maza anawaacha kwanini. Wakiachwa wajijenge na kutanua mipaka ya Rwanda kwa kuongezea Goma kuna siku watavamia TZ na tutakuwa tumechelewa.
 
ni vile tu JWTZ hawajaamua tu kuingia vitani, wakiamua siku moja haitaisha M23 watakufa wote na stori itaishia hapo.

Vita ni rahisi hivyo? 😂😂🚮
 
Wapiganaji wa vita ya Uganda 1978-79 walitoka majeshi yote ya ulinzi na usalama ya Tanzania: JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, TISS, na Mgambo.

JWTZ walikuwa na majukumu ya uongozi; kukusanya wapiganaji toka nje ya jeshi hasa mgambo vijijini, kushughulikia mahitaji, kuandaa na kupanga mwenendo wa vita, kuongoza vikosi, kutoa mafunzo na mazoezi ya kivita (crash training), ku-operate mitambo na silaha kubwa (vifaru, APC, mizinga na magari yake, jet fighters, n.k.).

Vile vile raia wengi wa kawaida walichukuliwa hasa kwa ajili ya kushughulikia ukusanyaji na usafirishaji wa mahitaji (supplies), udereva wa magari ya mizigo na abiria, wapishi, n.k.

Ni vita iliyoshirikisha Watanzania wengi sana ndani na nje ya JWTZ. Wote walikuwa na combat uniform moja na silaha zinazofanana. Mtu asiyehusika asingeweza kutofautisha yupi ni JWTZ, JKT, polisi, magereza , mgambo …. Viongozi wote walikuwa na rank za JWTZ bila kujali ni wa jeshi lipi.

Neno uzalendo lilipata maana kubwa sana wakati ule. Sijui kama kuna maandiko yanayoonyesha hali halisi ya vita ile. Mitandaoni Siku hizi zimejaa simulizi za kipropaganda zisizoakisi hali halisi ya ile vita.
 
Hivi we ulikua haujui km Jeshi ni la CCM sio Jeshi la Wananchi? Nikwambie mara uelewe kwamba Jeshi lipo chini ya CCM na Wanajeshi walio wengi ni Wana CCM sio wao tu hata ndugu na Wazazi wao ni CCM hakuna Mwanajeshi ambae hatokei kwenye Chimbuko la CCM, Wanajeshi wooote unaowaona ni Wana CCM

Ongea kingine nikusikilize
 
Neno uzalendo lilipata maana kubwa sana wakati ule. Sijui kama kuna maandiko yanayoonyesha hali halisi ya vita ile. Mitandaoni Siku hizi zimejaa simulizi za kipropaganda zisizoakisi hali halisi ya ile vita.
Jeshi limekaa kisiasa zaidi sasa hivi sio tena Jeshi la kupigana Vita, Jeshi lipo zaidi kuwalinda Viongozi wa kisiasa wabakie madarakani na sio vinginevyo tukichokonolewa nahisi hata na hao vibaka wa M23 tutachezea kichapo vibaya ngoja waivamie Kigoma kule Lake Tanganyika ndio utaona tuna Jeshi la aina gani, Jeshi lililobakia ni Jeshi la kuilinda CCM ibakie Madakani kwa namna yoyote

No election No reform huna Jeshi wenzio CCM wana Jeshi lao unategemea nini? Ukifanya fyoko wanakutembezea kichapo sababu wanailinda CCM kwa namna yoyote
 
Ivi tunafaidika na nn kama nchi?
Serikali inalipwa na Wanajeshi wanalipwa Mjeshi anaaenda huko kuna Maokoto anapata akirudi salama na sio haba ni pesa nzuri, Wanajeshi wote wanailinda CCM iendelee na ibakie Madarakani hakuna Mwanajeshi wa Chama Pinzani hata mmoja
 
Kwani SADC wanaenda kulinda Amani au kupigana vita na M23?
Watalindaje bila kupigana, hata mlinzi wa nyumba inamlazimu kupigana kama nyumba inashambuliwa. Unalinda hali ikiwa shwari na unapigana kulinda pale unachokilinda kinashambuliwa. Wakati wa vita kazi ya mlinzi ni kupigana, mlinzi(mjeda) si sawa na masanamu yanayowekwa kwenye mashamba ya mpunga.
 
We waache tu. Wanalifdharau jeshi halafu wakishughulikiwa wanaolalamika eti jeshi limetumia nguvu kubwa! Kwani maana ya Jeshi ni nini?
Mbona linashindwa kutumia nguvu kujilinda lisidhalilishwe na wanamgambo wa M23? Madogo hawa wanaoajiriwa kwa vimemo ndiyo wakapigane na watu wenye experience ya vita? Vita havipiganwi kwa maneno ya mdomoni, on the battlefield is where you show what you got.
 
Sijui ni ujinga umetuingia kama WaTz ama tumekuwa na raia wengi mamluki. Kila siku humu ni kumesifia Kagame na M23.

Watu bila uelewa wanajaribu kulinganisha operation ya sasa na ile 2013-2014. Operation ya sasa JWTZ ni washiriki siyo jeshi kiongozi, hivyo JWTZ kwasasa wanatoa nguvu kazi na utaalamu tu, lakini maamuzi ya operation iweje siyo yao. Operation ya 2013-2014 JWTZ ndilo lilikuwa jeshi kiongozi, likiongozwa na Mwakibolwa. Ukijua kutofautisha hapo hauwezi kuilaumu JWTZ na matokeo ya huko GOMA na KIVU.

Jeshi hili hili tunalolidharau na kuliona limekaa kisiasa Juzi tu limewafurusha waasi hapo Mtwara na linaendesha operations mbali mbali kwenye maeneo mbali mbali kwa mafanikio makubwa kabisa
 
Huyu Amiri Jeshi wa sasa anatudhalilisha.Hivi lile Jeshi la JKN liliichukua kampala na kupigana kote huko kusini mwa Africa liko wapi?Soon kwa mwendo huu tunaweza sumbuliwa na waasi wa Mtwara toka msumbiji tusipokuwa makini 🤔
Jeshi shupavu la enzi za JKN halipo tena, wote walishastaafu. Hawa watoto walioingizwa jeshini kwa connection na vimemo hawana discipline wala uzalendo na viongozi wameingiza u-CCM jeshi limekuwa la kulinda chama tawala kisitoke madarani, these goons can't do anything on the battleground.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…