Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Habari ni ya kweli yenye lengo maalumu. Kwanza, aliyeleta ni ''jirani'' yetu
Pili, kama mnakumbuka JokaKuu aliweka habari ya misiba na vilio Kigali.

Tatu, inatangazwa Askari wamepanda ndege Rwanda ili kuonyesha kwamba Rwanda haina tatizo na DRC

Nne, Askari walikabidihiwa na M23 kwa Rwanda bila kuwadhuru kwa maana ni majeruhi, inaonyesha ''coordination' kati ya M23 na Kigali, kwamba , M23 hawana tatizo na mataifa mengine ni watu ''wema''

Tano, tangu kikao cha Dar kilichoagiza Wakuu wa Majeshi wa Nchi 5 wakutane hakuna taarifa zaidi.

Sita, M23 wanazidi kusonga mbele bila kujua hiyo ni mbinu ya ''ku stretch'

Subirini mtasikia
Seems M23 na Rwanda wana ubinadamu kwa kuwarudisha mateka waliokamatwa nyumbani kwao bila kuwadhuru au kudai chochote, ingekuwa lile jeshi lako la Congo na interahamwe hao wote wangeliwa mshikaki
 
Sijui kwanini Walinunuliwa Yutongs full viyoyozi... Kuna mtu nia yake sio nzuri yakufanya jeshi lowe comfortable na Relaxed...wakifika Congo ni mwendo wa Bedfords vunja kiuono wanaomba warudi kambini Tanzania tu wakale asali maziwa na mkate.
 
..Na alipokuja Dsm kwenye mkutano wa Sadc-Eac tukampokea kwa heshima za kijeshi, maturumbeta, na wakata viuno.
Mtu kaua na kujeruhi wanajeshi wenu alafu mnampokea kwa parade!! Ningekuwa mimi soldier pale yangetokea yaliyompata Anwar Saddat.
 
Sijui kwanini Walinunuliwa Yutongs full viyoyozi... Kuna mtu nia yake sio nzuri yakufanya jeshi lowe comfortable na Relaxed...wakifika Congo ni mwendo wa Bedfords vunja kiuono wanaomba warudi kambini Tanzania tu wakale asali maziwa na mkate.
Juzi nimeshangaa eti kwenye mafunzo yao ya RTS Kihangaiko wanafundishwa kutulizwa waandamanaji. Nikasema yaaani Jeshi letu nalo limeingia kwenye siasa mfu za kukilinda Chama cha Mapinduzi badala ya kushughulika na mambo makubwa makubwa?

Acha tu tule matokeo ya Jeshi letu kuwa kikaragosi cha Wanasiasa wajinga wa CCM. Na bado.
 
Juzi nimeshangaa eti kwenye mafunzo yao ya RTS Kihangaiko wanafundishwa kutulizwa waandamanaji. Nikasema yaaani Jeshi letu nalo limeingia kwenye siasa mfu za kukilinda Chama cha Mapinduzi badala ya kushughulika na mambo makubwa makubwa?

Acha tu tule matokeo ya Jeshi letu kuwa kikaragosi cha Wanasiasa wajinga wa CCM. Na bado.

Maarifa hutangulia kila kitu. Jeshi siyo msuli wa mwili, wala mavyumavyuma yaitwayo zana. Jeshi cha kwanza kabisa cha maana ni msuli wa ubongo, na inaonekana Kagame ana msuli imara sana wa ubongo kichwani mwake!
 
Hayo majibu waliyopewa ni ya kweli.
Ukiwa kwenye mkataba wa ulinzi wa amani, silaha na vifaa vya kijeshi hulipiwa na UN.
Halafu mikataba ya kiulinzi ya UN hauruhusiwi kurusha risasi hata uchokozwe.
Kule kugumu Mana UN hao hao wanakuambia Huruhusiwi kumuua Mwana harakati ( M23 )
Kumbe M vingt trois Ni Wana harakati na Sio waasi Wala jeshi.
 
Lengo lako ni kuitaja CCM Wala sio wanajeshi,na hizo habari ulizoleta na bandiko BBC ni vitu viwili tofauti.
 
😀😀😀 kumbe shughuli ya mwakibolwa unaijua..?

Afande shimbo ni opportunist 😁😁 refeer issue ya kule kisiwani, mzee shimbo bana 😂😂🙌
 
Chopa ya kivita si inadunguliwa mazee itatua wapi wakati maeneo yote M 23 wameyazingira na kumbuka hata jeshi la DRC wamejiunga M 23 na polisi wao kwa kuhahidiwa mshahara mkubwa kuliko wa Serikali ambao ni mdogo na walikua hawapewi kwa wakati..
Nilimaanisha mara baada ya M 23 kuruhusu Wanajeshi kurudishwa Rwanda.
Baada ya M 23 kuruhusu, ilitakiwa iende chopa kuwatoa DRC mpaka Bongo na si kupitia Rwanda. Nadhani kulikuwa na makubaliano kati ya M 23 SADC na MUNUSCO jinsi ya kuwaondoa wanajeshi.
 
Najua habari hii imewauma sana makamanda ninawafahamu wa JWTZ!

Najua habari hii imemuua sana kamanda Luteni Generali Mstaafu Mwakibolwa. Najua habari hii imemsononesha sana General Mstaafu Davis Mwamunyange. Najua habari hii haijamlaza vizuri mwamba Luteni General Abdulrhman Shimbo.

What we use to know as Tanzania Pride iliyokuwa inabebwa na Jeshi letu la Wananchi (Tanzania People's Defence Forces) imefikia tamati baada ya wanajeshi wetu kudhalilishwa huko Rwanda kwa kusubilishwa kwa masaa mpakani na Wanajeshi (Mamlaka za Rwanda).

Wanajeshi wetu waliosubilishwa mpakani ni sehemu ya majeruhi wa vikosi vya SADC waliopokea kichapo kutoka kwa Wanajeshi wa Rwanda na Washirika wao M23.

Inasemwa pia Wanajeshi wetu kama sehemu ya wanajeshi wa SADC wamenyang'anywa silaha zao na wanamgambo wa M23 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Hawawezi fanya chochote bila ruhusa ya M23.

Itakumbukwa hadi miili ya Wanajeshi wetu waliouwawa bado haijarudishwa na inawezekana jamaa wanatuwekea ngumu ili tuendelee kuwalamba miguu na ili watuoneshe kuwa sasa wao ndo mabwana zetu kivita.

Naumia sana Nchi yangu kufikia hapa. Naumia sana Jeshi langu JWTZ kufikia kudhalilishwa hivi.

Kuna haja ya kujitafakari na kuanza upya. CCM ni janga.
View attachment 3249000

=======

Takriban wanajeshi 200 wanaohitaji wakihitajihuduma ya matibabu wakiwemo wale wa Afrika Kusini, Malawi na Tanzania walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC waliondoka Goma na kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kuelekea Kigali kwaajili ya kupata ndege za kuwarejesha makwao.

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza wikendiiliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.

Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda,ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwayamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.

g

Walifika mpakani Jumatatu saa sita mchana, na waliondoka mpakani baada ya saa kumi na mbili jioni, Donatien anasema.

Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani.

Vyombo vya habari vya Goma - jiji linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.
Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.
Kichapo gani unachosema hapo sijakuelewa,maana vikosi vile vinatekeleza viko pale kwa article 6 na unajua kazi yao ni nini? siyo kupigana ni kulinda amani! Kikosi cha akina Mwakibolwa kilikua [ale kwa artocle 7 ya umoja wa mataifa na ndiyo maana waliwatindika hao wajinga unao wasifia. Sasa kichapo sijui ni kichapo gani zaidi ya misifia ya kijinga ya Wanywaranda. Congo mnainnea kwa sababu hawana jeshi imara hebu acheni ujinga wenu huo!
 
Jeshi letu inabidi lijitafakari. Kama ni kweli limeingiliwa na wanasiasa wa CCM hadi kulifanya lishindwe ku focus kwenye masuala ya msingi hadi kufikia linadharirika hivi basi kuna haja ya kufanya yale aliyofanya General Sani Abacha kule Nigeria mwaka 1993
Hii kitu haina uhusiano wowote na unachosema! nimegundua kwenye mitandao kuna watu wengine uelewa wenu ni mdogo sana! mnatamani vita mandhania ni vizuri,huo ujinga hatuutaki hapa.
 
Kichapo gani unachosema hapo sijakuelewa,maana vikosi vile vinatekeleza viko pale kwa article 6 na unajua kazi yao ni nini? siyo kupigana ni kulinda amani! Kikosi cha akina Mwakibolwa kilikua [ale kwa artocle 7 ya umoja wa mataifa na ndiyo maana waliwatindika hao wajinga unao wasifia. Sasa kichapo sijui ni kichapo gani zaidi ya misifia ya kijinga ya Wanywaranda. Congo mnainnea kwa sababu hawana jeshi imara hebu acheni ujinga wenu huo!
Kikosi cha SADC kina jukumu gani?
 
Rwanda Huwa wanaidogosha tu lakini ni Nchi ambayo inajeshi Bora na la kisasa.Mfano mwaka 2013/2014 alipotaka kutuchapa watanzania alikuwa anasilaha za kisasa kama ndege zisizo na rubani na silaha za balistiki ambazo zinaweza kufyatuliwa kutoka Kigali Hadi feri magogoni Dar es salaam
Naona unaongea kupita matakho?
 
Back
Top Bottom