Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Tambua tu hili:
Mafunzo yao wamepata US,hata mtoto wa namba moja alienda fundishwa huko juzi kati,kuna msemo mmoja ulitolewa na mzee Mandela”ukiona majirani wanapigana jua moja ya nchi ametembelewa na US”. Congo madini yake ni adimu duniani sawa na Ukraine ndio maana vita zao kl mtu anamgombea.
NB
Somalia…Madini,mafuta and gas
Sudan :: mafuta,gas and madini
Congo ..madini
Mashariki ya kati….gas,Madini and mafuta
Venezuela….mafuta and gas
Ukiona ppt kuna vita ujue kuna utajiri and mabeberu wanayataka hayo hivyo mnavurugwa
Mbona hata sisi tunayo na tena kwa wingi zaidi lakini kitu kama hiki sisi hatuna? Kumbuka kuwa baada ya tukio la ugaidi KWENYE balozi mbili ZILIzOPO Dar na Nairobi mnamo August 1998, BAADA YA pale US Alijenga HAPA ubalozi MKUBWA ZAIDI KULIKO BALOZI ZAKE zOTE zilizokuwepo DUNIANI kwa WAKATI huo. WAKATI UBALOZI WA Dar unajengwa, ULIKUWA NI ubalozi MKUBWA ZAIDI kuzidi Balozi ZOTE ZA US zilizokuwepo DUNIANI kwa wakati huo

US HUWA ANACHAFULIWA TU ILI WENYE TAMAA WAPATE MWANYA WA KUIBA. US ANGEKUWA HIVYO HATA SISI HAPA TUSINGEKUWA SALAMA UKIZINGATIA KUWA TAYARI ANA BASE YAKE KUBWA SANA HAPA KWETU.

KAMA ANAVYOENENDA NA MAMA, MUNGU AENDE PIA NA RAIS TRUMP KWA KISHINDO KIKUU
 
Waiguse TZ mara ngapi wakati wameua na kujeruhi askari wetu?
Mleta mada ni mpumbavu mmoja asiyejua taratibu zozote za kijeshi na diplomasia,Tanzania haikwenda kupigana Congo,hao M23 unaowahofia wanatambua vzur sana jambo litakalowapata wakiigusa Tz,huyo Kagame sio tahira hivyo,anaangalia na sehem za kugusa
 
Mama yao kabaki kumpiga kofi mtoto halafu anambembeleleza
 
Jeshi siyo uwezo wa kupiga kwata, gwaride, kusafisha barabara wapinzani wakitaka kufanya maandamano, kuonea raia eti wagalagale chini pindi wakitresspass maeneo ya jeshi.

Jeshi ni AKILI. Kama huna watu wenye IQ kubwa kwenye kamandi mtapigwa tu, hata muwe na zana nzuri kivipi!
 
Ata ivyo mmezoea kuaminishwa ujinga
Sku moja niliwai kusikia msemaji wa JWTZ akisema jeshi letu ni namba 3 kwa ubora
Nkabakia nashangaa iv uyu anazani anaongea na watz wa miaka ya 60 ajui kua dunia ya leo kila kitu kiko wazi
 
Juzi nimeshangaa eti kwenye mafunzo yao ya RTS Kihangaiko wanafundishwa kutulizwa waandamanaji. Nikasema yaaani Jeshi letu nalo limeingia kwenye siasa mfu za kukilinda Chama cha Mapinduzi badala ya kushughulika na mambo makubwa makubwa?

Acha tu tule matokeo ya Jeshi letu kuwa kikaragosi cha Wanasiasa wajinga wa CCM. Na bado.
Hawa MAKADA WA CCM watavuna walichopanda
 
Kanchi kadogo ka Rwanda kanazichezesha singeli Nchi zote za Maziwa Makuu na ukanda wa SADC aibu kubwa hii.
Mkuu; Tukuombe tu uwe mtulivu halafu baada ya muda sio mrefu utajionea na kushuhudia Heshima ya JWTZ ikirudi mahali pake kwa kasi ya 5G.
 
Najua habari hii imewauma sana makamanda ninawafahamu wa JWTZ!

Najua habari hii imemuua sana kamanda Luteni Generali Mstaafu Mwakibolwa. Najua habari hii imemsononesha sana General Mstaafu Davis Mwamunyange. Najua habari hii haijamlaza vizuri mwamba Luteni General Abdulrhman Shimbo.

What we use to know as Tanzania Pride iliyokuwa inabebwa na Jeshi letu la Wananchi (Tanzania People's Defence Forces) imefikia tamati baada ya wanajeshi wetu kudhalilishwa huko Rwanda kwa kusubilishwa kwa masaa mpakani na Wanajeshi (Mamlaka za Rwanda).

Wanajeshi wetu waliosubilishwa mpakani ni sehemu ya majeruhi wa vikosi vya SADC waliopokea kichapo kutoka kwa Wanajeshi wa Rwanda na Washirika wao M23.

Inasemwa pia Wanajeshi wetu kama sehemu ya wanajeshi wa SADC wamenyang'anywa silaha zao na wanamgambo wa M23 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Hawawezi fanya chochote bila ruhusa ya M23.

Itakumbukwa hadi miili ya Wanajeshi wetu waliouwawa bado haijarudishwa na inawezekana jamaa wanatuwekea ngumu ili tuendelee kuwalamba miguu na ili watuoneshe kuwa sasa wao ndo mabwana zetu kivita.

Naumia sana Nchi yangu kufikia hapa. Naumia sana Jeshi langu JWTZ kufikia kudhalilishwa hivi.

Kuna haja ya kujitafakari na kuanza upya. CCM ni janga.
View attachment 3249000

=======

Takriban wanajeshi 200 wanaohitaji wakihitajihuduma ya matibabu wakiwemo wale wa Afrika Kusini, Malawi na Tanzania walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC waliondoka Goma na kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kuelekea Kigali kwaajili ya kupata ndege za kuwarejesha makwao.

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza wikendiiliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.

Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda,ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwayamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.

g

Walifika mpakani Jumatatu saa sita mchana, na waliondoka mpakani baada ya saa kumi na mbili jioni, Donatien anasema.

Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani.

Vyombo vya habari vya Goma - jiji linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.
Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.
Tanzania iliingia DRC kama sehemu ya SAMIDRC. Huwezi kwenda kulinda Amani halafu unabadili kuwa Offensive. FARDC ndio wafanye offensive. Kama wanakimbia kama watoto basi hakuna haja JW kupendelea kuwepo DRC.
Tanzania haijawahi kuwaza kufanya offensive DRC. JW ndio jeshi pekee lililowahi kishinda vita kamili hapa SADC na EAC.
 
Tanzania iliingia DRC kama sehemu ya SAMIDRC. Huwezi kwenda kulinda Amani halafu unabadili kuwa Offensive. FARDC ndio wafanye offensive. Kama wanakimbia kama watoto basi hakuna haja JW kupendelea kuwepo DRC.
Tanzania haijawahi kuwaza kufanya offensive DRC. JW ndio jeshi pekee lililowahi kishinda vita kamili hapa SADC na EAC.
Usiongelee historia. Ongelea yaliyopo.
 
Wakati tunavunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel 1973, Israel ilitukosea nini direct?

Tulipata faida gani?

Dunia ishaachana na mambo ya kununua ugomvi usiokuhusu. Nyerere alitumia nguvu nyingi kusaidia nchi za Afrika na harakati za kugombania uhuru ila hatujaambulia kitu, Nyerere mwenyewe wamemsahau wanawakumbuka Nkurumah na Mandela tu who did absolutely nothing for them.

Kama TZ itajiingiza kwenye huo mgogoro kwa namna yeyote ile inabidi iweke maslahi yake mbele yani iwe imeingia kupata faida na kulinda interest za nchi sio kutafuta sifa za kijinga. Congo imekua kubwa jinga toka ipate uhuru haijui amani ni nini kila siku inapigana tu hatuwezi kuwa saviors kusaidia wasioweza kujisaidia wenyewe.
 
Mimi ni mzalendo lakini nahisi kama kwa sasa hata tukizichapa na Uganda tunachapika mbaya,
Wale watu wanabajeti kubwa kwenye majeshi yao
 
Usiongelee historia. Ongelea yaliyopo.
1.Huwezi kuacha historia unapotaka kuongelea sasa.
2.Vita vya sasa ni vya kiuchumi. Siyo vita vya ukombozi wala pride.
3. Tuna maslahi ya kibiashara na DRC na sio political economy interests. We can do business na DRC under any regime. It is not necessary to impose a regime in DRC so to do business with.
4. Mkakati wa kujenga na kuboresha barabara na reli kuelekea DRC unatosha kwa sasa. Hii haihitaji vijana wetu kufa kwa ajili hiyo.
5. Kunachotakiwa kufuata ni kupeleka huduma na uwekezaji wetu DRC under any regime so to influence economics and business. Tupeleke mabenki, Ofisi za bandari, Ofisi za Reli, Wamiliki wetu wa malori washawishiwe na wawezeshwe kuingia soko la DRC.
 
TZ peke yake haikuwa na uwezo kupigana na Iddi amini sema kweli mulipata msaada toka nje ya nchi na uungaji mkono mkubwa wa silaha lengo ni choko choko za julius nyerere kumuondoa kiongozi wa kiislam Iddi amini Uganda na Africa mashariki. leo mnajidai na kujimwagia sifa ilihali ukweli unajulikana
Msaada toka nje? Toka wapi?

Jeshi la Uganda lilikuwa na uwezo gani? Lilipigana vita gani kabla ya ile ya Kagera? Zaidi ya kuonea, kutisha, kunyanyasa, kutesa na kuua raia lilikuwa likifanya kazi gani ya maana ya kijeshi?

Uislamu unaingiaje hapa?

Hata kama zilikuwa choko choko za Nyerere, Tanzania ilikuwa vizuri sana kijeshi miaka ile. Ilikuwa tishio sana Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika.

Kwa taarifa yako, baada ya kipigo kikali eneo la Lukaya (Uganda) kabla kabisa ya Kampala, jeshi la Idi Amin lilianza kusambaratika na kukimbia mapigano. Kama sio changamoto za logistics, jeshi letu lingemaliza vita mapema zaidi. Sehemu nyingi hasa baada ya Kampala ilikuwa ni walk-over tu; hakukuwa na upinzani wa maana.

Jeshi lolote linaloishi kwa kutishia, kunyanyasa na kufanyia ugaidi raia wake huwa halina uwezo wala ujasiri wa kukabiliana na adui wa nje vitani. Jeshi la Mobutu lilipotea kama moto wa mabua mbele ya wapiganaji wa kina Laurent Kabila.
 
TZ peke yake haikuwa na uwezo kupigana na Iddi amini sema kweli mulipata msaada toka nje ya nchi na uungaji mkono mkubwa wa silaha lengo ni choko choko za julius nyerere kumuondoa kiongozi wa kiislam Iddi amini Uganda na Africa mashariki. leo mnajidai na kujimwagia sifa ilihali ukweli unajulikana
Hakuna vita ambayo haina support. Cha muhimu ushawishi wako wa kupata support. Hata USA huombaga support ya Washirika wake na Five Eyes au AngloSuxons.
 
Kama ni kweli basi lawana zote ziende kwa Amiri jeshi wa nchi dhaifu
Hii ni zaidi ya fedhea!
 
Alyeleta udini ni baba yako nyerere, hakuwa na haja ya kumpiga vita iddi amini ila alitaka kusimika kanisa, ww hujuwi lolote uliza wazazi wako ni kwanini Tz ilimpiga vita iddi amini, usubiri itekewe kagera, Malawi tu wamepora ziwa lenu lile lake nyasa siju lake tanganyika mmeshindwa kufanya chochote,

Mombasa Kenya ni sehemu ya Zanzibar na Tanzania mbona mmeshindwa kuikomboa. nyinyi subirini uchaguzi mpige wananchi mabomu tu ndio mnayojua kwenye vita vya nchi na nchi hama kitu, M23 inawarejesha kwenye masanduku
Mimi najua HISTORIA ya nchi yangu. Ndiyo maana nimekwambia Nyerere kazaliwa kayakuata makanisa .Sasa Sasa unasemaje alisimika kanisa. wewe Utalopoka sana tu kwa kutokujua lolote sifia au mabwana zako na huo udini wako wa kipumbavu. Lakini iddi amini alileta za kuleta kapewa za huo za jeshi tiifu kabisa JWTZ. m23 yako hiyo haiwezi kufanya chochote kwa Tanzania hii. Mtapigwa Kama ngoma. Sasa ffu toka waliwatoa mbio mapoli ya kigoma na Kagera mkarudi Rwanda mbio sembuse JWTZ.
 
Kagera haikuwa Tz
Jitekenye tu.mbona rahisi tu mwambieni mme wenu mwingine museveni aungane na m23 na pk wenu mje muichukue Kagera Kama mlivyoichukia goma. Si umesema Kagera siyo Tanzania na imepakana na Uganda na Rwanda saaa kama nyinyi na wanaume sogezeni kwato zenu utaijua vizuri Tanzania maana mnavipele vinawawasha sisi atukuni tunapasua tu
 
Kazi kuonea raia wakikutana na wazee wa kazi wanasanda
 
Back
Top Bottom