Haya wameyataka wenyewe.
Tumekuwa tukishauri Sana hapa mtandaoni kwamba Wanajeshi wa nchi yetu warudi nyumbani ili waje kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi yetu hii, lakini inavyoonekana Watawala wa nchi hawataki kusikia ushauri wetu huo. Matokeo yake ndio haya sasa.
Maandiko Matakatifu yanasema kwamba "Aonywaye Mara nyingi naye hushupaza shingo, huvunjika ghafla na hakuna dawa tena."
(Mithali 29: 1)
Kama ni suala la Kulinda Amani, basi Jeshi linapaswa kupeleka Wanajeshi wake katika nchi za mbali, lakini siyo kwenda kulinda amani katika nchi ambazo ni majirani zetu. Hii ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa nchi. Wanajeshi Wapiganaji wa Vikosi vya Kulinda amani vinapaswa kupelekwa katika nchi za mbali huko Kama vile kwa mfano Pakistan, Lebanon, Mynmar, Haiti, n.k.
All in all, Wanajeshi wetu wanapaswa kupelekwa kwenda kulinda amani katika nchi zingine lakini muda wote kabisa wanapaswa wasimame katika Upande wa HAKI. Wasiende huko ili kwenda kuwatetea au kuungana na Watawala wa huko ambao ni Wadhalimu. Ujumbe wa Kulinda Amani usititumwe ili kwenda kusaidia au kuungana na upande wa Wadhalimu.
Daima Tukumbuke kwamba 'ukiungana na Wadhalimu basi Wapenda HAKI hawatakuwa upande wako.'