Pre GE2025 Mwishooni kabisa mwa hizi sarakasi za Siasa CCM ya Mzee Kikwete, Kinana, Makamba, Nape itaibuka kidedea na washindi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Kwa yoyote alobarikiwa kua na Uwezo wa kukisia mambo Fulani Fulani ya nyakati zijazo.

Kuna Makosa yalifanyika 2015-2020 , Ufalme akaanguka, Licha ya Ufalme kufanya mambo makubwa yaliyoonekana.
Makosa yaleyale yanajirudia 2022-2025, safari hii yanajirudia kukiwa na mambo yanayopigiwa kelele sana, DP World , Ngorongoro ya wamasaai , n.k.

Makosa yenyewe Wala hata hayahitaji nguvu kuachana nayo, VIFO VYA KISIASA , UKANDAMIZAJI WA SIASA PINZANI , DHURUMA KWA WANANCHI KUKOSA FURSA YA KUONGOZWA NA VIONGOZI WANAOWATAKA( TAMISEMI 2020 ).

Naam , na ni katika huu mtifuano wa masuala ya Dp World, Masuala ya Abdul , Masuala ya Lissu na Mbowe, NDIPO HAPO CCM YA KAMANDA JK ITASHINDA.

Mfalme anapozungukwa na Washauri wabaya, Haki na Kuinuka Kwa Taifa, Hupotea .... Mzee kikwete anaposema, ukitaka mambo yako yanyooke, Kaa vizuri na Wazee , anamaanisha kwelikweli.

Yule Adui "UJINGA" hatunae.
 
Makosa yaliyofanywa na utawala wa awamu ya tano waliopo wanayarudia tena yaleyale wanajiona wamekamata kila eneo na kudhibiti kila kitu,wanajiona hakuna wa kuwafanya chochote!
Katika dunia hii hakuna kitu kibaya kama kuwafanyia watu dhuluma na bado mkawaona wale watu ni maboya tu na hawana cha kuwafanya,Wacha tuone.
 
Kila mtu apambane na hali yake
Utakula ulipo peleka mboga
 
Unachekesha hahaha πŸ€ͺ !
Hakuna kitu kama hicho !
 
Sijui hapo katikati mambo yaharibike saaaaaana, ......habari njema ni kwamba KATIKATI ishafika, na mambo yameharibika saaaana.

Mzee wa msoga kazi kwako.
 
kwa mujibu wa Katiba iliyopo Mkuu wa Nchi hawajibiki kwa Wazee wala Vikongwe !😳
Awamu ile ya Mzee Kikwete Wapo Wazee wengi walidhalilishwa pia !
Kila mtu atulize boli !
Katiba bado ni ile ile na sheria ni zile zile na madaraka ni yale yale kwa mujibu wa Katiba !
Sina mashaka kila mtu anajua hivyo !
Locuta causa finita πŸ˜…πŸ˜€πŸ™ !
Wakae kwa kutulia !
 
Kiuhalisia nanusa kama wewe. Hili suala nilikuwa naliongea Jana na mwanangu mmoja wa falsafa na sayansi za siasa. Kuna uwezekano huko upande A kuna fukuto la ndani kuliko hili tunaloliona kule upande B. Muda ni muamuzi mzuri.
 
Ngorongoro kuna nini baya? Huduma zipo na wanaohama kwa hiari wanapewa utajiri wa ardhi na nyumba Msomera. Ni vile Watanzania wengi tunafikiria leo, ila wale waliopewa ardhi Handeni watakuwa sawa na waliopewa Geza, Kibugumo...Kigamboni enzi za Nyerere. Kelele za Ngorongoro ni za Human Rights Watch, Amnesty International na Green peace hakuna shida yoyote.

Hayo mengine ndo hata siyaelewi points zake. Tumwache Mhe. Rais Samia aongoze kwa vision yake na ya nchi.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mpaka sasa.
CCM 3 - 0 Chadema.

Na bado Samia katengewa penalty ili afunge goli lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…