Mwizi aliyekuja kuiba saa tisa usiku

Mwizi aliyekuja kuiba saa tisa usiku

Sijacheka hivi siku nyingi tye tye tye tye
 
Usiku wa kuamkia leo kibaka aliingia ndani na akafanikiwa kuchomoka na decoder ya Dstv, uzuri tukashtuka tukaanza kupiga kelele za mwizi huku tukimfukuza.

Tukiwa tunaendelea kumfukuza mwizi wetu, tukasikia tena kelele zikitokea kwenye nyumba jirani, mwizi huyo anaruka kaiba simu!!!! Majirani wakaunga tela kufukuza mwizi wa simu.

Wale wezi wakawa wamekimbilia njia moja, huku kelele zikiendelea, mwiziii huyoooo, kaiba dekodaaaaa. Kundi lingine, mwizi huuyooooo kaiba simuuuuu.

Baada ya dakika kadhaa mwizi mmoja kapiga kelele, wote tusimame, naye akasimama, tukawa kwenye bumbuwazi.
Mwizi wa dekoda akasema, mbona kundi kubwa linaniandama?

Mnaofukuza mwizi wa simu kaeni upande wa kushoto.

Mnaofukuza mwizi simu kaeni kulia.

Jamaa wakaenda kulia. Mwizi akasema kila mtu afukuze mwizi wake.

Akaanza Tena kutoka mbio ili tuanze tena kumfukuza🤣😂😅
Mitano tena
 
Weeehh...!!!

Wanazifanyia nini sasa wanaoziiba...!???

Au ndo mitumba, ile ya reo reo ya reo reo ya reo mali mpya imeingia mpende mkeo kifuli mia mia [emoji28][emoji28][emoji28]
Kuna vitu unavipenda mno!
 
Huyu kibaka wa Dar na si mwizi, hata wafukuzaji wa Dar pia, nilishudia anapigwa mmoja zipu ikafunguka jamaa wakaacha kupiga wakamwambia "mshikaji funga basi zipu yako hapo chini" [emoji15][emoji15][emoji15]. Yaani kibaka anawapangia jinsi ya kumkimbiza!! [emoji3][emoji3][emoji3]
Zipu ikafungukaje yenyewe?
 
Back
Top Bottom