Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua


Kaanza kutupiga taratibu!
 
Hapana. , Musa alikufa na roho yake iko hapo ikingojea ufufuo au ikingojea siku ya ufufuo.

Mbinguni yupo Bwana Yesu kwenye Bustani kubwa akingojea siku ambayo hata yeye haijui, Mungu Baba atakapomtuma kuja duniani kwa mara ya pili na kuondoka na Musa na Sie Watakatifu wengine.

Upande wa pili Yupo Mungu mwenyewe, mji ambao nguzo zake ni dhahabu hakuna giza, hakuna mchana wala usiku.

Tunaomwamini Mungu hivi vitu tunaoneshwa tukiwa na mwili huu huu.

Mpe Salaam zangu Mwalimu Mwakasege.
 
(Ufunuo 7:13-14)

13:Akamjibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu Hawa waliovikwa mavazi mweupe ni akina nani? Na wametoka wapi?

14: Nikamwambia , Bwana wangu wajua wewe. Akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki Ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi Yao na kuyafanya mweupe katika Damu ya mwana- kondoo.

... Mwisho wa kunukuu....

Neno linasema, wapo wataookolewa baada ya Unyakuo katika dhiki kuu,

Si Rahisi kuokolewa wakati huo kama sasa, ni Rahisi sana kuliko kusubiri mito yote na Ziwa na bahari vikauke pasiwepo maji, jua lisogezwe, mimea yote ikauke, uweze kuvumilia mateso hayo.

Mungu atusaidie.
 
Yesu akiwa na wanafunzi mlimani wakiomba,

Musa na Elia waliwatokea wakiwa katika miili ya kiroho.

Husomi maandiko?
 
Naungana na haya uliyo yaeleza hapa.

Watu watakwambiaje huyo Yesu ulijuaje ndo Yesu.


Maelezo haya yanajitosheleza sana.
 
Naungana na haya uliyo yaeleza hapa.

Watu watakwambiaje huyo Yesu ulijuaje ndo Yesu.


Maelezo haya yanajitosheleza sana.
Yesu akikutokea,

Utamwona Kwa kutumia macho ya Roho Si ya MWILI maana Yesu ni Mungu,

Na utajua huyu ni Yesu bila hata kutambulishwa, na utasujudu bila kuambiwa,

Ni automatically.
 
Kwani walipowatokea uliambiwa walitoka Mbinguni ?
Nawe aliyekwambia walitoka kaburini ni nani?

Hakuna nabii wa Mungu afaya na kusubiri kaburini.

Utakuwa mchanga kiroho ndugu yangu.

Kaburini inakaa Mizimu, wafu waliokufa katika dhambi, mapepo , wachawi, misukule nk nk.

Ikiwa Huwa unaenda kaburini ukiamini wapendwa wako waliokufa zamani wamo humo unajidanganya, na ukipiga magoti kuomba kaburini ndio kabisa unafanya Ibada ya wafu.
 
Unajua mnatuchanganya sana kwani anaekufa then anakaa kaburini ni nani?
Mwili wa aliyekuwa ndio unakaa kaburini.

Lakini mtu ni ROHO, tendo la kifo linapotokea, mwili hujitenga na Roho.

Roho ndio mtu halisi, ikiwa ulikufa katika Kristo Yesu, siku ya kufa, Malaika wa Nuru watakuijia na kukupeleka Mbinguni juu,

Ikiwa hukumwamini Yesu, ukifa katika dhambi, Roho Yako ambayo ndio wewe halisi watakuja Malaika wa Giza na kukushika na kukupeleka kuzimu ya moto, chini.

Umeelewa?
 
Kweli Tanzania tuna bahati

Mfalme Zumaridi amewahi kwenda mbinguni

Nabii Mkuu GeoDavid naye amewahi kwenda mbinguni

Mzee wa Upako naye amewahi kwenda mbinguni

Sasa mchungaji Mwakasege naye ameenda na kurudi

Ajabu huu ni Mwaka wa 2025 tunamsubiri Yesu arudi wakati hao wenzetu wameenda na kurudi Kwa kipindi kifupi tu πŸ™Œ

Maajabu hayawezi kuisha πŸ€—
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…Ule Uchawi wa Rakims umetufikisha huku?

Mimi nasemaga hapa tz hakuna Injili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…