Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Kwani Mussa na Eliya walipomtokea Kristo Yesu, Biblia ilitoa ufafanuzi timilifu wa namna miili yao ilivyokuwa?
Au ilisema tu Mussa na Eliya walitokea na Petro akasema wajenge vibanda vitatu au?
Petro alipowaona, aliwatambua kwamba huyu ni Musa, na huyu ni Eliya.

Na walionekana na utukufu wenye kung'aa, wenye miili Bora mfano wa Malaika ndio sababu Petro akashawishika kumwambia Yesu vijengwe vibanda Kwa ajili ya Ibada na kumbukumbu.
 
Petro alipowaona, aliwatambua kwamba huyu ni Musa, na huyu ni Eliya.

Na walionekana na utukufu wenye kung'aa, wenye miili Bora mfano wa Malaika ndio sababu Petro akashawishika kumwambia Yesu vijengwe vibanda Kwa ajili ya Ibada na kumbukumbu.
Sawa sasa inakuwaje Biblia kusema watu wakifufuliwa wanapewa miili mipya wakati kumbe ukifa tu na kuingia mbinguni unapewa mwili mpya?
 
Namba 1 nakubaliana na wewe japo ni katika nadharia ila naiamini nadharia hiyo.

Namba 2 sikubaliani na wewe, kama watakatifu wakifa hawakai kaburini wanaenda mbinguni moja kwa moja, then inakuwa vipi kwenye biblia kitabu cha ufunuo wa Yohana nadhani kama nna kumbu kumbu vizuri.
Kuna mstari unasema kwamba "parapanda itakapolia wafu walio makaburini watafufuliwa kwanza, alafu ndiyo wahukumiwe kila mtu kwa matendo yake".

Sasa huoni kuwa hii inapingana na mtazamo wako wa "watakatifu wakifa hakai makaburini wanaenda mbinguni moja kwa moja" ?


Namba 3 nakubaliana na wewe upande mmoja wa "Mungu ni mmoja", lakini unaposema Mungu huyo ndiyo Yesu hapo umeni- confuse.

Kwa sababu kwa jinsi nilivyo isoma biblia (japo ina mafumbo mengi) na kila mtu anafasiri kwa namna anavyoelewa yeye, ila mimi nilivyo ielewa Biblia Yesu siyo Mungu na wala yeye hakuwahi kujiita Mungu (japo baadhi ya mitume kama yohana walikuja kuandika kana kwamba Yesu alikuwa Mungu, ingawa yeye mhusika hakuwahi kujiita Mungu).

Swali la msingi ni je, Yesu yeye alisema yeye ni nani ? Kwa mujibu wa biblia (hasa vitabu vinne vya injili), Yesu alipo ishi duniani siku zote alikuwa akijitambulisha kuwa "yeye ni mwana wa Mungu, aliyetumwa na babaye (Mungu) kwa ajili ya kufanya kile Mungu amemtuma".

Na kuna mda hata alikuwa anaomba na kusali kwa Mungu wake (baba yake).

Sasa how come tukisema Yesu ni Mungu ? Mungu anaweza kujiomba ? Kujisalia ? Kufa je ?

What I noticed kwenye biblia ni kwamba "Yesu alikaimishwa majukumu ya kimungu na Mungu lakini siyo kwamba ndiyo alikuwa Mungu".
Hiyo inadhihirishwa na mistari kadhaa ya kwenye biblia kama "Huyu ndiye mwanangu mpendwa ninaye pendezwa nae,msikilizeni yeye"

"Na mimi nawatangulia naenda mbinguni kwa baba kuwaandalia makao na nitarudi nije niwachukue ili nilipo mimi nanyi muwepo"

"Mimi ndimi njia ya kweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi"

Hakuna mahali kwenye biblia Yesu amewahi kujiita Mungu au kujitambulisha yeye ni Mungu, ila kuna confussion zilizoletwa na baadhi ya mitume ambao walikuja kuandika kuhusu Yesu baada yeye Yesu kuwa amesharudi mbinguni tayari.

Mfano wa mitume has ni yohana aliyekuja kuandika kwamba "Hapo mwanzo kulikuwako neno,naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu" sijui huyo neno akakaa kwetu akafanyika mwili n.k.

Huu ni mojawapo wa mstari kwenye biblia unaoleta confussion sana na watu kuanza kuona kana kwamba "Yesu ndiye Mungu mwenyewe aliye hama kutoka kwenye makao yake mbinguni na kuja kuishi duniani kimwili kitu ambacho kwa mujibu wa biblia naona si sahihi".

Kama nitachukua mtazamo kama wako ya kwamba "Yesu ni Mungu mwenyewe original aliye amua kuuvaa mwili na kuja duniani(siyo mwana wa Mungu)" then nikuache na swali hili hapa chini πŸ‘‡

Je, huko mbinguni kwenye makao ya kiroho wakishafika watakatifu, watamwona Mungu, Yesu na malaika au watamwona Mungu, na malaika au watamwona Yesu na malaika pekee ?

Nitaomba unijibu hilo swali kwa ufasaha kabisa.

Na nimeuliza hivo kwa sababu, kama Yesu ni mwana wa Mungu kama alivyo jitambulisha yeye kipindi anaishi duniani, basi nna hakika na Mbinguni tutamkuta yeye Yesu,Mungu pamoja na malaika.

Ila kama nitachukua mtazamo wako wa kwamba Yesu ni Mungu mwenyewe aliye uvaa mwili na kuja duniani, basi huko mbinguni kuna kimojawapo hatutakikuta kati ya Mungu na Yesu, maana kilijibadilisha kuwa kitu kingine na muda huo kitakuwa kimerudi kwenye form yake ya uhalisia siyo mwili tena.

Ila kama mbinguni tutawakuta Mungu na Yesu katika utofauti (Baba na mwana) basi kauli yako ya Yesu ni Mungu haitakuwa sahihi.
 
Petro hakuwahi kumwona Musa Wala Elia before,

Lakini walipomtokea Yesu, aliwatambua vizuri.

Ndipo ujue, Roho hujua yote, Ukiwa na macho ya Roho, ukamwona Yesu, utajua bila kutambulishwa kuwa huyu ni Yesu.
 
Sawa sasa inakuwaje Biblia kusema watu wakifufuliwa wanapewa miili mipya wakati kumbe ukifa tu na kuingia mbinguni unapewa mwili mpya?
Hao ni watakaofufuliwa wakati Ule wa dhiki kuu.

Watapewa miili mipya Ili wakaungane na WATAKATIFU wenzao ambao tayari wako Mbinguni.

BIBLIA ni coded na ukiisoma bila msaada wa Roho mtakatifu hutaona ikipingana, lakini ukiisoma kana gazeti, mkanganyiko ni mwingi sana.
 
Hivi mbinguni usafiri wa kufika huko ni farasi tu au kuna aina nyingine ya usafiri?
Hao farasi wa kupeleka watu mbinguni ni hawahawa wa duniani au wanatoka hukohuko mbinguni kuja kubeba binadamu huku duniani?
 
Ni kweli mbingu ipo lakini hakuna binadam hapa duniani aliwahi fika kule na kurudi kama hawa matapeli wanavyotuhadaa
 
I and the FATHER tu umoja.

Umewahi soma andiko Hilo?

Yesu pia amejitambulisha kama " Mimi NIKO" utambulisho alijitambulisha Mungu Kwa Musa.

Ningependa nikujibu Kwa undani zaidi, naomba nipate muda.
 
Ni kweli mbingu ipo lakini hakuna binadam hapa duniani aliwahi fika kule na kurudi kama hawa matapeli wanavyotuhadaa
Mbinguni huendi kibinadamu.

Ukijua mtu ni ROHO,

Binadamu ni WA udongo.

Ukijua mtu ni nani, hutoshangaa Roho kwenda Mbinguni wakati mwili upo duniani USINGIZI.
 
Zuma riidi ni Pepo katika form ya mwanadamu,

Fuatilia hata Kuzaliwa kwake, kulikuwa tofauti mamaye ameeleza vyema,

Kuhusu majengo marefu hata kuzimu kavu, yapo.

Lakini pia Mbingu ni halisi IPO.
Hebu fafanua kidogo hapo kuhusu majengo marefu ya mbinguni na kuzimu?
Na kuzimu pia wanatumia farasi kama mbinguni? Manake hawa wa mbinguni wanatueleza mambo ya farasi weupe wanaong'aaπŸ€”πŸ€”. So probably hii technology ya skyscrapers engineers and architects wameitoa either mbinguni au kuzimu.
 
I and the FATHER tu umoja.

Umewahi soma andiko Hilo?

Yesu pia amejitambulisha kama " Mimi NIKO" utambulisho alijitambulisha Mungu Kwa Musa.

Ningependa nikujibu Kwa undani zaidi, naomba nipate muda.
Forget about blaa blaa zote nilizo ziandika then nijibu sentensi za mwisho kwamba "Mbinguni tuta mkuta Mungu,Yesu na Malaika ? Au tutamkuta Mungu na malaika ?
 
Petro hakuwahi kumwona Musa Wala Elia before,

Lakini walipomtokea Yesu, aliwatambua vizuri.

Ndipo ujue, Roho hujua yote, Ukiwa na macho ya Roho, ukamwona Yesu, utajua bila kutambulishwa kuwa huyu ni Yesu.
Hizo ni Alfu lela ulela ndiomana mtu yeyote akijisikia kusema katokewa na mtu anasema..!! Tutamuamini vipi hapo ndo zinapoanza blah blah kilikwenda kikarudi..!!
 
Kuhusu majengo yaliyopo Mbinguni soma kitabu Cha ufunuo,

Hadi vipimo vya mji Ule mpya vimeandikwa.

Kuhusu farasi weupe imeandikwa ndani ya BIBLIA Yesu atakuja amepanda farasi mweupe,

Kuhusu kuzimu kule makazi ya shetani waliolaaniwa, hata wakitembea Kwa mguu ni sawa tu.
 
Swali no 2.

Zamani kabla ya kufufuka Kwa Yesu, WATAKATIFU walikuwa wakifa wanasubiri Mahali paliitwa Paradiso, Mahali pema peponi,

Baada ya Yesu kufufuka, WATAKATIFU huenda mbingu ya kwanza live, na hawahukumiwi tena, maana hayupo wa kuwahukumu.
Kakudanganya mpumbavu gani wewe jamaa 😁😁😁 bila shaka wewe ni mmojawapo wa wapuuzi wa madhehebu ya dini ....nitajie upo dhehebu gani nikuonyeshe upumbavu wa dhehebu lako ....
 
Hizo ni Alfu lela ulela ndiomana mtu yeyote akijisikia kusema katokewa na mtu anasema..!! Tutamuamini vipi hapo ndo zinapoanza blah blah kilikwenda kikarudi..!!
Hutakiwi kuniamini Mimi,

Soma Bible ujue nilichoandika limeandikwa ndani ya BIBLIA au la.

Sasa amini neno la Mungu, ukiliamini ndipo utajua niliyoona pia ni kweli
 
Kakudanganya mpumbavu gani wewe jamaa 😁😁😁 bila shaka wewe ni mmojawapo wa papuuzi wa madhehebu ya dini ....nitajie upo dhehebu gani nikuonyeshe upumbavu wa dhehebu lako ....
Watafute watu wa dini na madhehebu uwaulize swali hilo,

Mimi ni Roho, namwabudu Mungu katika Roho na Kweli.
 
Nitajibu kuhusu lugha,

Lugha za duniani ni za huku, Mbinguni kuna lugha yake.

Roho Haina limit katika utambuzi, inajua yote.

Ukienda Mbinguni, hutafundishwa lugha chuoni, utaelewa na kuongea automatically.
Hayo maswali ambayo haujayajibu ni kwamba hayana majibu yake.
I'm eager to learn.
 
Hutakiwi kuniamini Mimi,

Soma Bible ujue nilichoandika limeandikwa ndani ya BIBLIA au la.

Sasa amini neno la Mungu, ukiliamini ndipo utajua niliyoona pia ni kweli
Bible ni kitabu kilichoandikwa na watu na chenye mapungufu..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…