Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Nimeongelea aketiye katika KITI Cha enzi, wewe unanirudisha msalabani,

Nikuulize wapi imeandikwa kwamba Yesu ndiye Mungu aketiye katika KITI Cha enzi ningekujibu.

Karibu.
Ufunuo wa Yohana 1:1

Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana.

Huo 👆 ni mstari wa biblia, hapo kwenye "Ufunuo wa Yesu kristo aliyepewa na Mungu"
Bado tu huoni kuwa Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu ambae yuko chini ya Mungu na kupokea maagizo kutoka kwa Mungu ?
 
Nimeuliza tofauti ya wewe na mwakasege kuhusu nafsi .. sikusema ujaeleza ...wewe unasema hivi mwakasege anasema vile ...(kumbuka imeandikwa ufalme ulio farakana hauta simamq) kama mafundisho au imani zenu zinapingana vipi mnaweza kuwa wote ni sahihi🤣🤣
Jikite kwenye mada,

Maswali nje ya mada hayajibiwi hapa.
 
Kuhusu majengo yaliyopo Mbinguni soma kitabu Cha ufunuo,

Hadi vipimo vya mji Ule mpya vimeandikwa.

Kuhusu farasi weupe imeandikwa ndani ya BIBLIA Yesu atakuja amepanda farasi mweupe,

Kuhusu kuzimu kule makazi ya shetani waliolaaniwa, hata wakitembea Kwa mguu ni sawa tu.
Kati ya kupanda farasi mweupe na Tesla car kiukweli kabisa nachagua Tesla, farasi unafika kiuno kiko hoi huku wife anakusubiri.
 
Nimeongelea aketiye katika KITI Cha enzi, wewe unanirudisha msalabani,

Nikuulize wapi imeandikwa kwamba Yesu ndiye Mungu aketiye katika KITI Cha enzi ningekujibu.

Karibu.
MUNGU NA YESU NA ROHO MTAKATIFU NI KITU KIMOJA KWA KUWA NI NAFSI MOJA ...
1) MUNGU NI NAFSI YA MUNGU
2) YESU NI NAFSI YA MUNGU NDANI YA MWILI WA MWANADAMU USIO NA NAFSI YA MWANADAMU
3) ROHO MTAKATIFU NI NAFSI YA MUNGU NDANI YA MWILI WA MWANADAMU WENYE NAFSI YA BINADAMU ...YAANI NAFSI MBILI NDANI YA MWILI MMOJA ...Kwa fafanuzi hii ni kweli aketiye kwenye kiti cha enzi ndiyo huyo huyo nafsi ya kristo ambaye ndiyo mungu ...hii ndiyo injili ya kweli yenye uwezo wa kujibu kila swali hata maswali ya waislamu kuhusu yesu yanajibika kwa asilimia 100 kwenye fafanuzi hii ya kweli na thabiti.
 
Nitajibu kuhusu lugha,

Lugha za duniani ni za huku, Mbinguni kuna lugha yake.

Roho Haina limit katika utambuzi, inajua yote.

Ukienda Mbinguni, hutafundishwa lugha chuoni, utaelewa na kuongea automatically.
"Roho haina limit katika utambuzi", inakuwaje hapa duniani roho tunazo(that's what we're being told) lakini tuna limit katika utambuzi.
 
Salaam, Shalom!!

Akifundisha katika semina jijini Mbeya Jana tarehe 26 January,Mwalimu Christopher Mwakasege amerudia kauli aliyowahi kuitoa kabla.

Amesema, asubuhi, walipokuwa katika bible study ya familia asubuhi ya jumapili hiyo, Mkewe alimuuliza swali kuwa ikitokea ametokewa na YESU atamtambuaje?

Mwalimu Christopher Mwakasege akamjibu Kwa kumkumbusha juu ya siku aliyotoka ndani ya MWILI wake na kwenda Mbinguni, alipofika Mbinguni, alikutana na Nabii Musa yule Nabii wa kale, na alimtambua, akaongeza kusema, Ukiwa katika mwili wa kiroho, huhitaji kutambulishwa sababu Roho inajua yote na kutambua yote yajayo na yaliyokwisha pita.

..... Mwisho wa kunukuu....

Naungana na Mwalimu Christopher Mwakasege juu ya UKWELI wa jambo hili, mbingu IPO na ni halisi, Mimi pia nimewahi kwenda Nchi nzuri sana, mfano wa uzuri wa Nchi Ile hauelezeki, mji huo hakuna jua Wala mwezi, IPO Nuru nzuri sana ambayo macho hayachoki kuitazama,

Nimewahi kuandika pia juu kupewa taarifa juu ya ujio wa Yesu kulinyakua Kanisa Kwa kumwona Yesu akiwa na jeshi la Malaika, amepanda farasi mweupe wakienda Kwa Kasi mawinguni.

Ndipo tujue yafuatayo.

1. Mbingu ni halisi Si hadithi.

2. WATAKATIFU wote wapo Mbinguni, wakifa hawakai kaburini.

3. Mungu yupo na ni MMOJA, na Jina la Mungu huyo mmoja tulilopewa WANADAMU liwezalo kuokoa ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH.

Mungu awabariki.
Nilipaswa niwe marehemu kitambo sana. Lakini Mungu ananiweka hai kwa upendo wake. Mtu mwenyewe nina milima ya dhambi. Kimsingi sina haki mbele zake za kumshawishi niendelee kuvinjari duniani.

Naunga mkono ushuhuda wa Mwakasege. Mwaka 84 nimewahi kupelekwa mbinguni katika roho. Taswira zile sijawahi kuzisahau ni kama nilienda jana. Mwaka 1987 nilishuhudia uwepo wa Yesu hapa duniani. Alikuja kututembelea familia na wote walimuona. Mimi nilimtambua na kuwajulisha. Familia walikubali yule mtu wa Mungu hakuwa wa kawaida na features zake na miujiza kila mtu aliiona.....

Kuna vitu vinatokea maishani naviona kabla na huwa nasema vinatokea. Mambo mazuri au hatari.

Nimeiona Tanzania ipo gizani miaka mitatu iliyopita na nilisema kisha wote tumeona yanayojiri....

Kuna watu wanajifitini baada ya kutufitini wakidhani watasimama milele
 
Ufunuo wa Yohana 1:1

Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana.

Huo 👆 ni mstari wa biblia, hapo kwenye "Ufunuo wa Yesu kristo aliyepewa na Mungu"
Bado tu huoni kuwa Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu ambae yuko chini ya Mungu na kupokea maagizo kutoka kwa Mungu ?
Umekosea YESU KRISTO NI VITU VIWILI ni MWILI *mwanawa adamu) na NAFSI ambayo ndiyo mungu ...kilichokufa msalabani na kufufuka siku ya 3 ni mwili siyo nafsi ya kristo ndiyo maana msalabani yesu anamwambia yule mtu kuwa 👉 leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi sasa ujiulizi yesu aliyekufa na kufufuka siku ya 3 ni nani na huyo ambaye leo hii anakuwa peponi ni nani? Tumieni akili ...NAFSI YA YESU NDIYO MUNGU HIVYO HAIWEZI KUFA HATA SEKUNDE MOJA ...baada ya siku ya tatu nafsi ya mungu ikaulejea mwili wa kristo ndiyo maana ya kufufuka siku ya 3 ...hivyo ukisikia neno "MWANA"maana yake ni mwili wa kristo na ukisikia neno "BABA"maana yake nafsi ya kristo ambayo ndiyo Mungu
 
Kuna Uzi nimeandika kuhusu mbingu na layers zake.

Mbingu ya kwanza hakuna jua Wala mwezi,

Huko Nuru inayotumika ni Mungu mwenyewe,

Soma maandiko uelewe, hutauliza maswali ya kitoto.
Kwahiyo mungu ni umeme? 😹
Rabb ebu acha utani basi, kwahiyo mwakasege alienda kwenye mwanga akaniambia ndo mbinguni na wewe unakubaliana nae kabisaa.!??
 
"Roho haina limit katika utambuzi", inakuwaje hapa duniani roho tunazo(that's what we're being told) lakini tuna limit katika utambuzi.
Ni sababu ya kuishi ndani ya MWILI.

Ndio maana USINGIZIni Roho hupata nafasi .
 
Ni kweli wapo watakaookolewa kwenye dhiki kuu na ni wengi ila kama maandiko yanavyoonyesha kwenye kitabu cha ufunuo kuokoka kipindi hicho itakuwa ni kwa shida sana maana imagine huwezi kuuza wala kununua ina maana hakutokuwa na ajira kwa urahisi kwa watakaokoka hasa ile miaka 3.5 ya mwisho then hata kama ukitaka kufanya biashara si rahisi maana haupo linked na global antichrist digital financila system.

Halafu heri ni wale watakaokuwa wamenyakuliwa na ndio ambao wataingia karamuni mwa Yesu miaka 7, wanarudi duniani na miili ya utukufu kumpiga vibaya sana mpinga kristo na majeshi yake na kutawala dunia na miili hiyo ya utukufu.
Ndiyo maana ni vizuri sana kwa mwamini kukesha kwa maana ya kuwa tayari wakati wowote maana aliyeokoka na akaukosa unyakuo ni hatari sana kwake.
mbona maandiko yanasema Yesu alisharudi na tupo naye ?
Huyo unayemsubiri wewe ni yupi?
1 Yohana 5:20
 
Kumbe huyu Mwakasege nae ni tapeli tu kama kina Mwamposa..
 
Tofauti Mohammad alikuwa ni mtume na hakuna mtume baada yake hawa wengine ni wahuni ...
Hiyo ni kutokana na Imani yako, kwa hawa wa makanisa ya dotcom mitume wapo kibao. Nyie mlipigwa lock kiaina na vitabu vya Imani zenu na kuna wengine Jesus ndiyo kila kitu yaani bila yeye haufiki huko aliko Mungu.
Ukija kwa Buddhists, Hindu, Bohra na denominations nyingine pia unakutana na mengine bado zipo zile za kale Africa kabla ya ujio wa Waarabu na Wazungu.
 
Kwann Yesu/Mungu anakua Portrayed kama Mzungu tu? Sisi watu weusi tuseme nini?
Mungu ni Mungu,

Usichanganye mambo ya RANGI za WANADAMU, wakati asili ya mtu ni Adam.
 
Umekosea YESU KRISTO NI VITU VIWILI ni MWILI *mwanawa adamu) na NAFSI ambayo ndiyo mungu ...kilichokufa msalabani na kufufuka siku ya 3 ni mwili siyo nafsi ya kristo ndiyo maana msalabani yesu anamwambia yule mtu kuwa 👉 leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi sasa ujiulizi yesu aliyekufa na kufufuka siku ya 3 ni nani na huyo ambaye leo hii anakuwa peponi ni nani? Tumieni akili ...NAFSI YA YESU NDIYO MUNGU HIVYO HAIWEZI KUFA HATA SEKUNDE MOJA ...baada ya siku ya tatu nafsi ya mungu ikaulejea mwili wa kristo ndiyo maana ya kufufuka siku ya 3 ...hivyo ukisikia neno "MWANA"maana yake ni mwili wa kristo na ukisikia neno "BABA"maana yake nafsi ya kristo ambayo ndiyo Mungu
Eheee..sawa, MWANA ni mwili wa KRISTO na BABA ni nafsi ya KRISTO ambayo ndiyo MUNGU.

Kwa hiyo nafsi ya Yesu iliipa maagizo mwili ya Yesu alafu mwili wa Yesu (mwana) ukampa malaika maono akamwoneshe Yohana, what hell is this ?

Any way tuachane na habari ya nafsi maana nafsi hata mimi na wewe tunayo.

Kwanza ni NAFSI ni kitu kingine na wewe ulicho kielezea hapo ni ROHO siyo NAFSI.

NAFSI ni Muunganiko wa mwili na ROHO.

"Mungu akampulizia puani Adam pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai" hivyo nafsi ni muunganiko wa roho na mwili pamoja ndiyo nafsi, ila vikitengana kimoja kinakuwa mwili kimoja kina kuwa roho.

Cha msingi nilichotaka kukuuliza ni Je, mbinguni watakatifu watamwona Mungu na Yesu kama vitu viwili tofauti au watakiona kimoja tu kwa sababu ni kile kile kilijibadilisha form (umbo) ?
 
Back
Top Bottom