Mwl. Nyerere: Unaweza kumtingisha Waziri Mkuu nchi isitikisike lakini huwezi kumtingisha Rais

Mwl. Nyerere: Unaweza kumtingisha Waziri Mkuu nchi isitikisike lakini huwezi kumtingisha Rais

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mwl. Nyerere alikuwa na busara sana kulipotokea hamkani ya Malechela kutomshauri vema Rais Mwinyi, Nyerere alionya akasema unaweza kumtingisha Waziri mkuu nchi isitikisike lakini huwezi kumtingisha Rais nchi ikaacha kutikisika.

Maana yake ni nini? Mwl. alitambua nguvu ya Rais na mamlaka yake kwa ustawi wa taifa letu. Hivyo basi ni vema tuache tetesi za mitandaoni na tubaki kumuombea mema ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ustawi wa taifa letu.

Superbug.
rais 1.PNG
rais 2.PNG
rais 3.PNG
rais 4.PNG
 
Alinyofolewa Lowassa na nchi ilienda vema ila Rais wa nchi sio Jambo la kulishabikia kwa pupa, habari za vigogo tuzipuuze kwa wakati huu ndugu zangu tuungane tuwe kitu kimoja just imagine Leo spika Ndugai kapanda miti Kongwa vipi kesho uzushi huu ikionekana sio kweli mtaficha wapi nyuso zenu?
 
Yaani mtu mmoja akitingishika watu milioni 52 wanatingishika? Ni mfumo dhaifu sana.
Sijui haya yanatoka wapi.

Kwa nini "itingishike" na kwa vipi?

Watu hawatapata milo yao ya siku kama kawaida yao?

Jaribu uone litakavyopita kama upepo, na maisha yataendelea kama kawaida, na pengine bora zaidi.

Kuna viongozi wa "kutikisa taifa" siyo dizaini ya huyu.

Huku ni kutisha watu tu.
 
Mnatuchanganya mjue nyie, mara tusikie mzima wa afya na anapiga kazi zake, mara tusikie yupo Nairobi, mara tusikie yupo Bahari Ya Hindi akieelekea India, mara tusikie amesharudisha "USAJILI WAKE" kwa Sir, mara mtuambie tumuombee dua wakati yeye mwenyewe "HAJATUAMBIA TUMUOMBEE".

Acha tusubiri, akituambia tumuombee basi tutamuombea. Akikausha basi fresh, no sho, fair play, na si tutakausha tu.
 
Labda una upungufu wa media nyumbani kwako kweli hujawahi kumsikia mh Rais Magufuli akisema anaomba tumuombee hasa kwakuwa sera zake zinachukiwa na wasiolitakia mema taifa? Rejea phrase yake juu ya Vita ya kiuchumi. Pengine aliforecast shubiri hii ndio maana alisema Mara nyingi mniombee.
 
Labda unaupungufu wa media nyumbani kwako kweli hujawahi kumsikia mh rais Magufuli akisema anaomba tumuombee hasa kwakuwa sera zake zinachukiwa na wasiolitakia mema taifa? Rejea phrase yake juu ya Vita ya kiuchumi. Pengine aliforecast shubiri hii ndio maana alisema Mara nyingi mniombee.
Si ndio hapo bana.

Kumuombea mtu sio lazima awe mgonjwa,

Unamwombea tu hata kama mzima wa afya, basi wamwombea afya yake iwe imara kwa kiasi kile kile au zaidi kabisa.
 
Back
Top Bottom