⚠️ Babu Tale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz afunguka kilichotokea walipoenda nyumbani kwa Diddy katikati ya tuhuma nyingi na kesi mbalimbali zinazomkabili Diddy nchini Marekani akihusishwa na uhalifu wa king0no anaodaiwa kuufanya kwa watu mbalimbali wanawake kwa wanaume
Babu Tale akizungumza na Rick Media amesema walienda kweli nyumbani kwa Diddy wakiwa na producer maarufu Swizz Beatz ambaye ni mume wa mwanamuziki Alicia Keys ila Swizz Beatz alikuwa akiwalinda Babu Tale na Diamond ingawa hawakukujua kwanini anawalinda ila ndio wamejua sasa baada ya Diddy kukumbwa na msala huo mzito wa uhalifu wa kingOno
“Sisi tulienda kama tulivyotoa taarifa hapo awali na tulitoka salama, jana ndiyo nimejua kwamba Swizz Beatz alikuwa akitulinda kinoma, kwanza tulipofika tulikaa nje. Diddy akatangulia chumbani juu anaangalia movie wafanyakazi wake wawili wakaja kutuchukua kwenda kula, baada ya muda akawatuma twende chumbani kwa Diddy tukaangalie movie lakini Swizz akawa mkali na tukaondoka bila kuaga kwahiyo sisi tukawa tunajua kuwa brother (Swizz Beatz) ametubania, kumbe alikuwa anatulinda,” amesema Babu Tale Babu
Kabla, Diamond alipoulizwa alisema si kila kitu kuhusu walipoenda kwa Dddy ni cha kuongelewa katika vyombo vya habari, kufuatia minong'ono na habari za Diddy kuendelea kuhusishwa na watu mbalimbali hasa maarufu ndio Babu Tale nae amehojiwa na kuongea
.............................................................................
Kwa contents mbalimbali YouTube follow channel ya Edson Mshishile 👇👇
MSHISHILE FILMS ni Channel ya EDSON MSHISHILE ambayo inajihusisha na uandaaji wa Filamu fupi, Vichekesho na Filamu ndefu. Hivyo kama mdau wa Filamu usiache ku-Subscribe na kubonyeza alama ya kengere ili kuendelea kupata Filamu mbalimbali kutoka katika channel hii.ð¤ð¤ðð...
www.youtube.com