Part two
Nawarudisha nyuma kidogo;
Mahusiano mengi ni win-win condition, kuna nyakati yule binti aliwahi kuniomba vitu viwili, moja aliomba mtaji wa biashara na kingine aliniomba nikipata nafasi sio mbaya nimjengee hata vyumba viwili ili ikitokea lolote basi mtoto apate sehemu ya kulala.
Baada ya tafakari, nikaona badala ya kumpa mtaji wa biashara Wacha nimjengee hiyo nyumba aliyokuwa ameniomba.
Nikanunua kiwanja Kibaha kwa Mathias kutoka kampuni moja iliyokuwa inajihusisha na uuzaji na ununuzi wa Viwanja
Baada ya kukamilisha kununua kile kiwanja, huku wale jamaa wanahangaikia kunitengenezea Hati, nikamwaga tofali then nikaanza kuinua vyumba vitatu.
Nikaanza kujenga taratibu huku nahesabu miezi ya huyo mtoto azaliwe.
Nyumba ilipofika usawa wa Lentor, si ndiyo nikakuta hizi kadi nyingine nne za huyu mtoto.
.….............. ................ .................
Alipotoka mazoezini, nikamweleza ukweli kuwa Mimi na yeye basi, nilikuwa natafuta ushahidi bahati nzuri nimeupata. Nikamwonesha zile Kadi zake nne za wale Wanaume wengine zenye majina ya mtoto wake
Kusema kweli nilijizuia sana kumfanya jambo baya siku Ile, nahisi Mungu alinisaidia vinginevyo huenda kwa Umri huu ningekuwa natumikia adhabu ya kuua.
Kuna mambo kadhaa yakawa yananijia kichwani, moja nitarudishaje gharama zangu
Pili nilipanga niwapoteze Mama na Mtoto wake, Kuna mpango niliporudi nyumbani niliupanga, ila baadaye huruma ilinijia nikamwacha aendelee na mambo yake
Muhimu nimeshajitoa kwenye ule mtego.
Kwa hasira, nilitafuta dalali, nikauza lile gofu pale Kibaha ili kufidia gharama nilizotumia japo kidogo, uzuri wake Hati ilitoka kwa jina langu
Baada ya tukio lile, simu zilipigwa nyingi kuomba tukae tuzungumze ili kumaliza tofauti.
Kwenye biashara hakuna mtu anatamani apoteze wateja, Mimi nilikuwa mteja wake miongoni mwa wateja wake wengine watano(5) tuliokuwa na Kadi zenye majina ya mtoto wake.
Mtu umemkuta na Kadi tano za mtoto, anataka mkae muyajenge, hivi mnajenga kitu gani hapo
To be honest lile jambo lilinigharimu sana, pamoja na usumbufu wa simu zake kupitia namba tofauti tofauti
Wakati ule simu zilikuwa hazina option ya kumfungia mtu asikupate (kama ilivyo sasa) iwapo umechoka usumbufu wake, hivyo nikawa nikikuta namba ngeni inapiga simu, nikawa sipokei hadi inakata.
Baada ya kutafakari kwa kina, nikatafuta Kozi Fulani nje ya Nchi ya miezi 3 nikaenda kupoteza muda kule ili kuondoa usumbufu wake.
Maana niliona ningeendelea kusalia Nchini wakati ule, ningemtumia watu wamwondoe bure yeye na Mwanae, maana uwezo na nafasi ya kufanya vile nilikuwa nao.
Kufika kule nikasajili namba nyingine niliyokuwa naitumia Whatsapp, na Ile aliyokuwa ananipata kawaida ikawa haipatikani.
.......................................
Huu mchezo kwasasa umekuwa mwingi miongoni mwa Wanawake wengi hapa Nchini
Japo nguvu za giza zimekuwa zinatumika sana kufanikisha hili, Mimi sijaandika kuhusu hili ili kufupisha hadithi
Kuna familia zimeingia kwenye migogoro kwasababu ya jambo hili
Kuna Wanaume wamechanganyikiwa na kuvurugwa kisa kikiwa hiki hiki Cha kulea mtoto mwenye Baba wengi
Kuna Wanaume ndoa zimevunjika kwasababu hii pia.
Kuna Wanaume wameacha kutunza familia zao kwa kutekwa na huu upande wa pili
Nimeandika kwa ufupi ili Ujumbe uweze kueleweka.
Nimemaliza ✍️