Ngoja nimalizie kisa changu hapa japokuwa kipo on progress
Kuna binti nilikutana naye sehemu, actually nilimchukulia kama heat and run, so kisa kinaanza hivi
Tulifahamiana ndani ya miezi miwili, na ndani ya miezi hiyo miwili nilikutana naye kama mara3 hivi, japo mambo yetu ya ukubwani ilikuwa mara2 na sikuwa na ukaribu kihivyo, kosa langu nilimleta kwangu mara moja akawa amepajua, katika huo mwezi siku moja nililala naye ..tukaja kukutana baada ya week 3 (kutokana na ubusy wa shughuli zangu)
Baada ya week3 ilikuwa siku ya jumapili nipo church akapiga sana simu ili aje kwangu nikawa sipokei maana nikiwa church huwa namute simu ..baada ya ibada nilikuta mised call kama 21 za binti huyo
Ikabidi nimpigie nikamuuliza shida ni ipi..akasema anataka kuja kwangu kuniona...mimi siku hiyo sikuwa na mzuka wa kukutana naye ila kwakuwa aliomba sana kuja kwangu nikasema ok.. aje...
Alivyokuja wala hakusema kama ana ujauzito maana ningeomba tupime (hapo tulikuwa na 3 weeks bila kuonana)
Basi bana ..jumapili hiyo akaja kwangu...tukafanya ya kufanya...asubuhi ya juma3 nikataka kwenda kwenye mishe zangu...akasema ana mimba yangu...yaani mimba kaipata usiku huo (mimi nikamkatalia) nikasema tupime akagoma katakata...kuna jirani ni rafiki yangu nikamshirikisha ..tukamwambie apime tukiwa wote akagoma pamoja na vipimo kuwepo akasema na hatoki ndani maana kashaharibu ujana wake
Basi nikaamua kupoa kwa muda ila nikasema kama umegoma kupima atoke ndani ya nyumba yangu akagoma
Kwa shida saana after 1 week 2 days ndio akakubari kutoka ila akadai ana mimba ila kupima hataki
Nikafanikiwa kumtoa kwa nguvu akatoka...akawa anaendelea kusisitizi ana mimba...baada ya mwezi ndio akasema nimpime akakubari..nikampeleka hotel tukapima .
Mimba ikawa imo...
To me, siamini kama huyo ni mtoto wangu japo alishazaliwa..impact yake simu kama zote za kuomba.matumizi...mara anataka ajengewe nyumba
Scenario ya kujitegesha kwangu na ndani ya saa 4 kutangaza ana mimba yangu imenifanya nisiamini mazingira ya mtoto huyo kupatikana (asije kuwa na kadi tano)
Ndio nipo njiani kufanyq DNA ya siri bila yeye kujua
Nimeleta kisa kwenye uzi huu maana vinafana na chako na bado ni tukio ambalo lipo active..wadau mnaweza nipa maoni
Akina dada wa sawa ni hatariqq anakutegeshea na mazingira ya mimba yanakuwa na uncertainity/utata nyingi/mwingi