My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana

My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana

Part two
Nawarudisha nyuma kidogo;

Mahusiano mengi ni win-win condition, kuna nyakati yule binti aliwahi kuniomba vitu viwili, moja aliomba mtaji wa biashara na kingine aliniomba nikipata nafasi sio mbaya nimjengee hata vyumba viwili ili ikitokea lolote basi mtoto apate sehemu ya kulala.

Baada ya tafakari, nikaona badala ya kumpa mtaji wa biashara Wacha nimjengee hiyo nyumba aliyokuwa ameniomba.

Nikanunua kiwanja Kibaha kwa Mathias kutoka kampuni moja iliyokuwa inajihusisha na uuzaji na ununuzi wa Viwanja

Baada ya kukamilisha kununua kile kiwanja, huku wale jamaa wanahangaikia kunitengenezea Hati, nikamwaga tofali then nikaanza kuinua vyumba vitatu.

Nikaanza kujenga taratibu huku nahesabu miezi ya huyo mtoto azaliwe.

Nyumba ilipofika usawa wa Lentor, si ndiyo nikakuta hizi kadi nyingine nne za huyu mtoto.
.….............. ................ .................
Alipotoka mazoezini, nikamweleza ukweli kuwa Mimi na yeye basi, nilikuwa natafuta ushahidi bahati nzuri nimeupata. Nikamwonesha zile Kadi zake nne za wale Wanaume wengine zenye majina ya mtoto wake

Kusema kweli nilijizuia sana kumfanya jambo baya siku Ile, nahisi Mungu alinisaidia vinginevyo huenda kwa Umri huu ningekuwa natumikia adhabu ya kuua.

Kuna mambo kadhaa yakawa yananijia kichwani, moja nitarudishaje gharama zangu

Pili nilipanga niwapoteze Mama na Mtoto wake, Kuna mpango niliporudi nyumbani niliupanga, ila baadaye huruma ilinijia nikamwacha aendelee na mambo yake

Muhimu nimeshajitoa kwenye ule mtego.

Kwa hasira, nilitafuta dalali, nikauza lile gofu pale Kibaha ili kufidia gharama nilizotumia japo kidogo, uzuri wake Hati ilitoka kwa jina langu

Baada ya tukio lile, simu zilipigwa nyingi kuomba tukae tuzungumze ili kumaliza tofauti.

Kwenye biashara hakuna mtu anatamani apoteze wateja, Mimi nilikuwa mteja wake miongoni mwa wateja wake wengine watano(5) tuliokuwa na Kadi zenye majina ya mtoto wake.

Mtu umemkuta na Kadi tano za mtoto, anataka mkae muyajenge, hivi mnajenga kitu gani hapo

To be honest lile jambo lilinigharimu sana, pamoja na usumbufu wa simu zake kupitia namba tofauti tofauti

Wakati ule simu zilikuwa hazina option ya kumfungia mtu asikupate (kama ilivyo sasa) iwapo umechoka usumbufu wake, hivyo nikawa nikikuta namba ngeni inapiga simu, nikawa sipokei hadi inakata.

Baada ya kutafakari kwa kina, nikatafuta Kozi Fulani nje ya Nchi ya miezi 3 nikaenda kupoteza muda kule ili kuondoa usumbufu wake.

Maana niliona ningeendelea kusalia Nchini wakati ule, ningemtumia watu wamwondoe bure yeye na Mwanae, maana uwezo na nafasi ya kufanya vile nilikuwa nao.

Kufika kule nikasajili namba nyingine niliyokuwa naitumia Whatsapp, na Ile aliyokuwa ananipata kawaida ikawa haipatikani.
.......................................

Huu mchezo kwasasa umekuwa mwingi miongoni mwa Wanawake wengi hapa Nchini

Japo nguvu za giza zimekuwa zinatumika sana kufanikisha hili, Mimi sijaandika kuhusu hili ili kufupisha hadithi

Kuna familia zimeingia kwenye migogoro kwasababu ya jambo hili

Kuna Wanaume wamechanganyikiwa na kuvurugwa kisa kikiwa hiki hiki Cha kulea mtoto mwenye Baba wengi

Kuna Wanaume ndoa zimevunjika kwasababu hii pia.

Kuna Wanaume wameacha kutunza familia zao kwa kutekwa na huu upande wa pili

Nimeandika kwa ufupi ili Ujumbe uweze kueleweka.

Nimemaliza ✍️


CHAI.
MWAKA GANI HUO AMBAO SIMU ZILIKUWA HAZINA BLOCKING ILA ZINA WHATSAPP? UONGO WAKO WA KIJINGA OPTION YA KU BLOCK NUMBERS IPO TOKA MIAKA YA 2000s wewe unasema haikuwepo. Ila miezi mitatu ukaenda nje ukawa una Whatsapp. Unaona wote makebo kama wewe?
 
CHAI.
MWAKA GANI HUO AMBAO SIMU ZILIKUWA HAZINA BLOCKING ILA ZINA WHATSAPP? UONGO WAKO WA KIJINGA OPTION YA KU BLOCK NUMBERS IPO TOKA MIAKA YA 2000s wewe unasema haikuwepo. Ila miezi mitatu ukaenda nje ukawa una Whatsapp. Unaona wote makebo kama wewe?
Ningekuwa nataka kutaja exactly ni lini tukio limetokea nisingesema ni tukio la mwaka 47

Nimeandika hivyo kwa lengo maalumu

Hata hivyo nimechagua kufikisha ujumbe kuhusu uwepo wa matukio ya hivyo, kama umechagua kuona chai katikati ya maelezo yangu badala ya Ujumbe

Basi tafuta maandazi ya Barhresa ukanywe hiyo chai
 
Ningekuwa nataka kutaja exactly ni lini tukio limetokea nisingesema ni tukio la mwaka 47

Nimeandika hivyo kwa lengo maalumu

Hata hivyo nimechagua kufikisha ujumbe kuhusu uwepo wa matukio ya hivyo, kama umechagua kuona chai katikati ya maelezo yangu badala ya Ujumbe

Basi tafuta maandazi ya Barhresa ukanywe hiyo chai

Chai ya Mwarobaini na alovera ambayo haijamenywa maganda.
 
Ni rahisi sana kuchambua tukio lililotokea na kuona makosa lakini ungekutana na situation kama hiyo si ajabu na wewe ungefanya makosa ya kijinga zaidi ya hayo.
Umesema sahihi Mkuu, na inawezekana muda huu kuna mwenzetu mwingine anapitia hayo niliyopitia.

Na usipokuwa na busara, maiti ya Mama na Mtoto inaweza kuokotwa
 
Namimi na kisa kama hiki natafuta njia ya DNA
Kama unataka kufanya DNA, chukua sampuli za mtoto iwe nywele ama hata jasho la nguo zake then nenda ukapime nje ya Nchi

Kama utapima Tanzania, huwezi kupata matokeo sahihi
 
whatsapp imeanza mwaka gani
Kwa Tanzania ilianza miaka ya 2009 kuelekea 2010

Japo sikutaka kusema ni tukio la mwaka gani exactly ili kuficha baadhi ya taarifa

Ndiyo maana nikasema tukio la mwaka 47 😎
 
Kwa Tanzania ilianza miaka ya 2009 kuelekea 2010

Japo sikutaka kusema ni tukio la mwaka gani exactly ili kuficha baadhi ya taarifa

Ndiyo maana nikasema tukio la mwaka 47 😎
nimekupata vyema mkuu wala haina tabu, uzi lazima uwe na wadhamini
 
Pole sana mkuu..... wanaume tunapitia mengi sana... !
Na kujitoa kwenye huu mtego sio rahisi

Unaweza kuhudumia mtoto ukasema ni wako, kumbe Kuna Mwanaume mwenzio sehemu naye anamuhudumia mtoto huyo huyo huku akijua ni wake pia

Kwasasa hayo matukio yamekuwa mengi sana

Japo changamoto kubwa naiona kwa Wizara ya afya kushindwa kuweka mifumo sahihi ya kudhibiti Kadi za Kliniki za Mtoto

Mtoto mmoja anakuwa na Kadi 5 za Kiliniki zikiwa na majina tofauti za Mtoto na Baba anayehudumia
 
Ndio ukajibu maswali ya mwaka 47 hukoo😂🏃🏽‍♀️
Maswali magumu kweli kweli, nahisi kwa kuwa nimezeeka nimeanza kupoteza kumbukumbu za hayo matukio ya mwaka 47 🤪
 
nimekupata vyema mkuu wala haina tabu, uzi lazima uwe na wadhamini
Vijana wana maswali mengi hadi Babu yao napoteza appetite ya kujibu 🙌

Hata hivyo nitakomaa nayo, muhimu mwaka 47 nilikwepo 🤗
 
Maswali magumu kweli kweli, nahisi kwa kuwa nimezeeka nimeanza kupoteza kumbukumbu za hayo matukio ya mwaka 47 🤪
Leo kumbukumbu zitarudi kwa jinsi ulivyobananishwa huko😂

Mi nashukuru tu umenipa mbinu nawaza nianzie wapi sasa😎
 
Leo kumbukumbu zitarudi kwa jinsi ulivyobananishwa huko😂

Mi nashukuru tu umenipa mbinu nawaza nianzie wapi sasa😎
Kweli Vijana hawataki amani kabisa na Wazee 🙌

Binafsi sikushauri ufanye hayo, Ukikutana na Mwanaume mwingine anaweza kuwaua wewe na mtoto ili kufidia hasara za malezi alizotoa kwako

Mimi ilibaki kidogo tu niwape Vijana kazi ya kwenda kusafisha
 
The only shimo a man will enter akiwa one man army ni kaburi tu mengine lazima we share. Sijui mmenielewa?
Kuchapiwa ni siri ya ndani, lakini sio uingie gharama za kutunza Mama na Mtoto ili hali sio damu yako
 
Hebu acha basi kwahiyo babu msaliti na mtoa mimba ndo malaika,, hapo walikutana shetani na shetani mwenzie ndo hivyo kazeeka saiv ni malaika
Mahi hatukatai babu msaliti ila mwanamke mwenzetu kazidi bhana. Wanaume watano?? Na unaweza kukuta wote sio baba wa huyo mtoto..!!

Babu moto anawapelekea si jogoo la shamba hilo 😹😹😹
Humu kwenyewe kazifumua za kutoshaaa 🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️
 
Ogopa mwanamke mshirikina, huyu huenda alikuwa muongo, malaya na mshirikina.
Mzee mwenzangu, kweli Uzee dawa, mengi sijayaandika ili kuendelea kuhifadhi privacy tu..

Ila ukiingia pale suala la kuwekwa kwenye chupa ni dakika 0 tu

Na kutoka huko ni hadi Yesu arudi
 
Back
Top Bottom