Mahondaw
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 75,495
- 185,562
Kweli kabisa.Unafanya vizuri mjukuu, mambo ya kugonganisha magari sio mazuri zamaa hizi
Kweli kabisa.Unafanya vizuri mjukuu, mambo ya kugonganisha magari sio mazuri zamaa hizi
Kesi yake sio ndogoOmba mwongozo kwa smart 😜🏃♂️🏃♂️
Weee sio kwenye kushea papa babu!Mkwe anaonekana Mzungu, atatoa mwongozo tu 😂
Aliyewaroga wanaume keshakufa kitambo babuu hamuwezi kutulia hata iwejeUkiweza kujua hilo, Mume atatulia kama maji mtungini
Waache waliwe pesa zaoPart two
Nawarudisha nyuma kidogo;
Mahusiano mengi ni win-win condition, kuna nyakati yule binti aliwahi kuniomba vitu viwili, moja aliomba mtaji wa biashara na kingine aliniomba nikipata nafasi sio mbaya nimjengee hata vyumba viwili ili ikitokea lolote basi mtoto apate sehemu ya kulala.
Baada ya tafakari, nikaona badala ya kumpa mtaji wa biashara Wacha nimjengee hiyo nyumba aliyokuwa ameniomba.
Nikanunua kiwanja Kibaha kwa Mathias kutoka kampuni moja iliyokuwa inajihusisha na uuzaji na ununuzi wa Viwanja
Baada ya kukamilisha kununua kile kiwanja, huku wale jamaa wanahangaikia kunitengenezea Hati, nikamwaga tofali then nikaanza kuinua vyumba vitatu.
Nikaanza kujenga taratibu huku nahesabu miezi ya huyo mtoto azaliwe.
Nyumba ilipofika usawa wa Lentor, si ndiyo nikakuta hizi kadi nyingine nne za huyu mtoto.
.….............. ................ .................
Alipotoka mazoezini, nikamweleza ukweli kuwa Mimi na yeye basi, nilikuwa natafuta ushahidi bahati nzuri nimeupata. Nikamwonesha zile Kadi zake nne za wale Wanaume wengine zenye majina ya mtoto wake
Kusema kweli nilijizuia sana kumfanya jambo baya siku Ile, nahisi Mungu alinisaidia vinginevyo huenda kwa Umri huu ningekuwa natumikia adhabu ya kuua.
Kuna mambo kadhaa yakawa yananijia kichwani, moja nitarudishaje gharama zangu
Pili nilipanga niwapoteze Mama na Mtoto wake, Kuna mpango niliporudi nyumbani niliupanga, ila baadaye huruma ilinijia nikamwacha aendelee na mambo yake
Muhimu nimeshajitoa kwenye ule mtego.
Kwa hasira, nilitafuta dalali, nikauza lile gofu pale Kibaha ili kufidia gharama nilizotumia japo kidogo, uzuri wake Hati ilitoka kwa jina langu
Baada ya tukio lile, simu zilipigwa nyingi kuomba tukae tuzungumze ili kumaliza tofauti.
Kwenye biashara hakuna mtu anatamani apoteze wateja, Mimi nilikuwa mteja wake miongoni mwa wateja wake wengine watano(5) tuliokuwa na Kadi zenye majina ya mtoto wake.
Mtu umemkuta na Kadi tano za mtoto, anataka mkae muyajenge, hivi mnajenga kitu gani hapo
To be honest lile jambo lilinigharimu sana, pamoja na usumbufu wa simu zake kupitia namba tofauti tofauti
Wakati ule simu zilikuwa hazina option ya kumfungia mtu asikupate (kama ilivyo sasa) iwapo umechoka usumbufu wake, hivyo nikawa nikikuta namba ngeni inapiga simu, nikawa sipokei hadi inakata.
Baada ya kutafakari kwa kina, nikatafuta Kozi Fulani nje ya Nchi ya miezi 3 nikaenda kupoteza muda kule ili kuondoa usumbufu wake.
Maana niliona ningeendelea kusalia Nchini wakati ule, ningemtumia watu wamwondoe bure yeye na Mwanae, maana uwezo na nafasi ya kufanya vile nilikuwa nao.
Kufika kule nikasajili namba nyingine niliyokuwa naitumia Whatsapp, na Ile aliyokuwa ananipata kawaida ikawa haipatikani.
.......................................
Huu mchezo kwasasa umekuwa mwingi miongoni mwa Wanawake wengi hapa Nchini
Japo nguvu za giza zimekuwa zinatumika sana kufanikisha hili, Mimi sijaandika kuhusu hili ili kufupisha hadithi
Kuna familia zimeingia kwenye migogoro kwasababu ya jambo hili
Kuna Wanaume wamechanganyikiwa na kuvurugwa kisa kikiwa hiki hiki Cha kulea mtoto mwenye Baba wengi
Kuna Wanaume ndoa zimevunjika kwasababu hii pia.
Kuna Wanaume wameacha kutunza familia zao kwa kutekwa na huu upande wa pili
Nimeandika kwa ufupi ili Ujumbe uweze kueleweka.
Nimemaliza ✍️
Babu kwani miaka yenu ya 50, haya mambo yalikuwepo kumbe 😒😒😒.??Part one
Najua haya maandishi tunayoandika humu yataishi na kusomwa humu hata baada ya sisi kuondoka Duniani miaka 50 ama 100 ijayo. Hivyo yanalengo la wengine waweze kujifunza.
Wewe Mwanaume, kama halijakutokea leo, basi kesho linaweza kukutokea maana kwa utafiti wangu mdogo, huu mchezo umeshamiri sana miongoni mwa Wanawake wengi miaka hii.
Binafsi lilinitokea miaka mingi iliyopita, kwa kuwa umri wangu umesogea sana, basi nitasema lilinitokea mwaka 47 😎
Iko hivi;
Niliingia kwenye mahusiano ya siri na mrembo mmoja miaka mingi iliyopita, nikiwa tayari kwenye Ndoa
Miaka ile kulikuwa na uhamasishaji wa upimaji wa HIV sana, kwani rate ya maambukizi ilikuwa kubwa, hivyo nami nilifanya mpango tukacheki afya kabla ya kuanza mahusiano
Baada ya miezi 6 hivi ya mahusiano ya siri, kuna siku kama nne mfululizo hivi mwenzangu alikuwa anaforce sana tuonane, of course tulikuwa tunaishi mikoa tofauti
Sikuwa tayari kuonana naye, hivyo nikamdanganya sikuwa na hela ya nauli hivyo ningependa anitembelee mwezi unaofuata
Ajabu alisafiri kwa nauli yake, akaja tukaonana
Baada ya wiki tatu hivi akanijulisha hazioni siku zake
Nilizipinga sana hizi taarifa, kwani tangu mwanzoni mwa mahusiano yetu, nilimweleza sitarajii kupata naye mtoto/watoto hivyo asiniletee habari zake.
Tukaingia kwenye mivutano then baadaye nikaamuru aitoe ile mimba, nikamtumia kiasi cha pesa ili aitoe
Alikula ile pesa na ujauzito hakutoa, kwahiyo ni kama aliamua kufanya kusudi (alikuwa na mipango yake na Ile mimba).
Mahusiano yaliendelea lakini sio kama awali, mivutano ilikuwa mingi na kisa kikiwa Ile mimba aliyobeba.
Wakati haya yanaendelea, nilikuwa nimempangia nyumba na by that time nilimlipia Kodi ya miezi 8 kwenye mji aliokuwa anaishi huku nikiendelea kumtumia hela ya matumizi
Yule Binti aliamua kutumia mimba yake kuni-blackmail, kwamba atafanya kila mbinu hadi Bibi yenu ajue kwamba ana ujauzito wangu.
Hivyo nikawa naendelea kumtunza huku napanga mipango ya kumchomoa Ile mimba kimya kimya, lakini bila mafanikio
Miezi 9 sio mingi, akajifungua mtoto wa kiume mweupe hatari, wakati huo Mimi Baba wa Mchongo ni mweusi kama lami.
Nikasafiri kwenda kuwaona Mama na huyo mtoto nikimbebea zawadi lukuki
Baada ya kumwona mtoto, ugomvi ukaanza upya, nikamwambia huyu mtoto amtafute Baba yake Mzazi sio Mimi
Mtoto hafanani na yeyote upande wetu, nimemkagua mara mbili mbili alama zetu, hana hata moja
Yaani nimekaa pale lakini akili hainipi kabisa, kichwa kinawaza hili mara lile...
Nikiwa nimepanga safari kurudi kwa Bibi yenu kesho yake, jioni moja aliniomba atoke kwaajili ya mazoezi mepesi hivyo Mimi nilibaki pale nyumbani na yule mtoto....
Mungu sio Athumani, wakati nipo pale nyumbani wakati napekua rimoti ya TV kwenye droo ya Meza na mtoto amelala kwenye sofa si nikakuta bahasha ya A4 ndani ikiwa na bahasha nyingine ndogo nne
Kukagua zile bahasha, nikakuta zina makadi ya Kliniki yenye majina ya yule mtoto tofauti kwa Baba wengine manne.
Kumbe mtoto ana Baba wengine wanne, Mimi nakuwa watano 🙌
Itaendelea sehemu ya Pili
Part Two: My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana
Mjikute tu... Tena wazeee ndo mnpenda chini balaa miaka hiiMbona sisi wazee wenu tumetulia lakini 😉
Kuna aina ya pisi unaweza uka I retain kama itakua na utulivu heshima Ile ile ya mwanzo hata kama unajua kabisa ilipigwa!!Jambo la kushea Wanaume wengi hatuwezagi kuvumilia sijui kwanini
Yaani hata uwe na mchuchu mkali vipi, ukisikia kuna wengine wanaichapa, mara zote hujiondoa taratibu
Wanasema kuanza upya sio ujingaKuna aina ya pisi unaweza uka I retain kama itakua na utulivu heshima Ile ile ya mwanzo hata kama unajua kabisa ilipigwa!!
Cha ajabu hawa viumbe ukijua TU mambo Yao ya Siri wanakubadilikia ili wewe ndio uonekane unabembelezea mahusiano,yaani wanatafuta ushindi ili kificha aibu yao wanaweza fanya lolote hata kukusingizia vitu vya kijinga jinga vile havina kichwa Wala miguu!!
Hata vya kudhalilisha kabisa!!
Na wakiona kama uliwekeza sana kwao na familia ndio hukuonyesha kiburi zaidi yaani aiseh!wanafikiri huna pa kwenda na unaweza nyanyasika kama Mzee wa miaka 70 kumbe kijana kabisa wa 36,38 Hadi 40!!
Unaingia mzigoni TU,akidai tuvitu vitu hasa manyumba haya ili apate pesa kwa mgongo wa "mali kwa ajili ya watoto" unasepa TU aiseh!
Ni bora ukaanza upya ukiwa na furaha kuliko kulia Lia ndani ya familia Yako mwenyewe uliyoijenga!!
Madem wengi ukishajua TU Siri zao,aiseh utapigwa sarakasi za kufa MTU Hadi utaomba poooh!!