We ni mwanaume, lakini una moyo wa kike. Mtu ambaye ametaka mwenyewe kuachana na wewe, na kwenda kwa mwingine, ambaye pamoja na manyanyaso yote lakini bado hataki kuondoka kwenye mahusiano hayo, then wewe ndio umuonee huruma kuliko yeye mwenyewe kujionea huruma?
Nikwambie tu, hiyo ni difence mechanism inakufanya ujisikie unamuonea huruma, but in reality bado unampenda na huelewi imekuwaje pamoja na wema na mapenzi yote uliyompau, but amekuacha na kwenda kwa huyo anayemnyanyasa.
Acha kumfikiria, angalia maisha yako na familia yako, usipokuwa makini unaweza kujikuta unashindwa kukaa na mkeo, huku huyo unayesema ananyanyasika akiendelea kudumu kwenye ndoa yake.