Ni wanaume wachache sana baada ya ndoa kuvunjika huwa wakisikia Ex wake anataabika au ana maradhi mabaya na anateseka kwa namna yoyote ataweza kujikausha na asipatwe na uchungu.Sababu kubwa ni kuwa,ni mtu ambaye mlizoeana sana,mliishi kama ndugu ila tu ushetani flani unaingia hapo kati unasababisha ndoa kuvunjika.Kuingilia kati hutaweza,kujikausha hutaweza,na kama atapata jambo baya zaidi bado itakusumbua sana.Ushauri wangu kama utaweza kupata nafasi ya kuongea naye,msikilize na umpe matumaini na si kuwa tenganisha,hii itamfanya ajione kuwa unampenda na kumjali,ingawa huwezi kutatua tatizo lake zaidi ya kumppa faraja.na kama ni swala lakuachana na huyo mwanaume iwe ni maamuzi yake binafsi na isiwe kutokana na ushawishi wako...