Kwa miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na mahusiana na mwanamke ambaye tulitokea kupata mtoto mmoja.Kutokana na saabu mbalimbali ikiwamo hali ngumu ya kiuchumi na changamoto nyingine za kimahusiano.Uhusiano wetu ulivunjika na Mwanamke akampeleka mtoto kwa BIBI yake na kisha akaolewa na yule bwana ambaye alikuwa sababu ya uhusiano wetu kuvunjika pamoja na madhaifu yetu.
Hata hivyo watu waliokuwa wanafahamu kuhusu uhusiano wetu walijaribu kuturudisha pamoja lakini mwanamke huyu alikataa kata kata kwa sababu mbalimbali.
Sababu ya kuandika uzi na kutaka ushauri wenu.NIFANYE NINI?
Kwa mujibu wa taarifa nilizopata huyu EX wife anapitia kipindi kigumu sana kwani uhusiano aliopo sasa ni very abusive(KIPIGO,MANYANYASO etc) Mateso anayopata ni ma,kubwa ila pamoja na hayo bado hatoki katika uhusiano(Binafsi nafikiri ni kwa sababu ya Majuto na kufikiri kwamba anastahili adhabu anayopata kwa sababu ya aliyofanya nyuma)
Pamoja na hayo yote nimejisikia kuumia sana baada ya kupata taarifa hizo ingawa sina ushahidi.Kuna uwezekano wa kumuona na kuzungumza naye ingawa binafsi nachelea kufanya hivyo hasa kutokana na mamao aliyonifanyia na pia kuepuka kuvuruga uhusiano wangu wa sasa.Baada ya kuachana naye alininyima access ya mtoto na hivyo taarifa za Mtoto nazipata kupitia kwa mdogo wake ambaye huwa ana namba yangu.
Tangu nipate habari hii nimeumia sana,nimetumia muda mwingi kusali ni kumuoma Mungu amsaidi lakini bado nakuwa na msongo wa mawazo kwa sababu yake.Hali imeathiri sana mambo yangu mengine.Nashindwa kuelewa ni kwa nini inakuwa hivi.JE NIFANYEJE ILI NIMTOE KATIKA UHUSIANO HUU IWAPO NI ABUSIVE.Je kwa nini nimekuwa na maumivu makali kwa sababu ya mateso yake?Je ni kwamba ninampenda au ni mimi tu nina matatizo yangu.
Tupeane ushauri juu ya nini naweza kufanya ili kuepuka msongo na mambo mengine ambyo naweza fanya katika hali kama hii.