Inasikitisha,inaumiza sana,inashangaza sana. Mimi najua ipo lakin nilijua ipo sana kwa wanafunzi na wanachuo (wenye umri mdogo),wasioolewa (baadhi) na ni wengi tu nawafahamu wala hawajifichi na wanaenjoy kupita maelezo na huo uhusiano wao, ila kwa mtu aliyeolewa hii ndiyo nimeisikia kwanza.
Lakin naamini kila jambo lina sababu zake.
Huyu dada kuna jambo limemsukuma mpaka aka fall in love na mwanamke mwenzie.
Na hizo sababu ndizo zilizomfanya atambue utofauti kati ya mumewe na huyu mwanamke mwenzie.
Ila kabla hajachukua uamuzi wowote ajiulize maswali haya.
1- je yupo tayari kutengwa na walimwengu kuanzia wazazi wake,mtoto wake,ndugu na rafiki kwa ajili ya kuendelea na huo usagwaji na huyo mwanamke mwenzie??.
2- yupo tayari kuikabili aibu hiyo mbele ya mtoto,mume,wazazi wake pindi uchafu huo ukijulikana??
3- na je ikijakutokea wakakorofishana na huyo mwanamke (msagaji) itakuwaje??, manake hapo afahamu kuwa muda huo tayari atakuwa ametengwa na mtoto,wazazi,marafiki,ndugu na mumewe.
4-angekuwa yeye anaachwa na mumewe ksb mumewe kapata mwanaume mwingine anayemridhisha zaid angejisikiaje??.
angalizo, asimwambie mumewe anaweza kumdhuru tena vibaya sana, kama alijaribu kumtania tu (japo nyuma ya pazia ilikuwa kweli) alikuwa mbogo je akimwambia kweli si atamwua kabisa??.
Huyo ni shetani tu anamjaribu anataka kuivunja tu ndoa yake,,"mwanamke mjinga anaibomoa ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe....................."
mungu kupitia maombi, wanasaikolojia ndiyo wanaweza kumsaidia huyo mwanamke kuachan na huo uchafu.
Mpe pole sana sana, ni majaribu tu ila naamini atayashinda.
wanaume kuweni wepesi kusifia uzuri wa wake/wapenzi wenu,wapendeni,watunzeni,wadekezeni,wajalini,wakuneni vizuri jamvini, ili kupunguza usagaji na uswagaji katika jamii, pia wanawake hii siyo njia sahihi ya kujitimizia haja zenu za jamvini,moto hauzimwi kwa kuumwagia petroli, shetani asizitawale akili zenu.