GE2025 My side: Hali jinsi ilivyokuwa tarehe 29. Maandamano, usaliti, uhalifu na mauaji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Kaka Mkubwa

Na mimi nikupe uzoefu wangu kwenye mambo ya kisiasa kila ninapoandika nimegundua watu wanachotaka uandike mambo kwa kuonyesha upande uliopo(upande wao) wakati mimi kama muandishi na mwanafasihi ninaandika kulingana na hali ninayoiona(mimi).

Mfano nikiandika mambo kuikosoa serikali wapo watu wataniponda. Nikiandika kuponda wapinzani wataniponda pia.

Nikiandika kilichopo kwenye jamii bila kukaa upande wowote yaani kuonyesha hisia zangu au maslahi yangu binafsi ninaandamwa vilivyo.

Nimegundua siasa hawataki watu Neutro wanataka aidha uwe upande wao au uwe adui yao.

Wakati mimi nataka watu wawe kitu kimoja. Unaona tofauti na hali ngumu ninayopitia?
 
Nje ya mada,


Mkuu una kipaji cha uandishi,hongera kwa hilo,
Nimesoma mada yote mpaka nikawa najihisi nipo kwenye tukio husika,

Big up sana Mkuu.

Mungu ni mwema sana.
Nashukuru na naamini Mungu hakukosea kunipatia kwani nitakitumia vilivyo watu wapate ladha, elimu, burudani, vichekesho, vioja, falsafa, na kila kitu chenye kujenga
 
Andiko refu blah blah nyiingiii kumaliza miti tu na karatasi....

Bila kukana ule ujinga uliandika mwanzo we nawe ni mat#$&k yako
 
Ulituambia unaweza vuka morogoro road ukiwa umefumba macho

Tukakwambia tulia mda wetu unakuja, mkaishia kutuua kwa risasi
 
Waandamanaji walikuwepo mkuu.
Nimeshuhudia kwa macho yangu lakini waliharibiwa na wahalifu ambao kimsingi wao ndio waliwapa ujasiri wa kuingia barabarani.

Lakini kila mtu alikuwa na lengo na maslahi yake hapa ndipo mkwamo ulikuwepo
Unaonekana ulikuwa undercover/askari kanzu wa kuwachomesha waandamanaji, maana kila tukio ulilishuhudia.
 
Ni kweli hakukuwa na waandamanaji waliobeba mabango.
Lakini ni kweli pia walikuwepo waandamanaji wa amani na dhati kabisa waliokuwapo eneo la tukio.

Sina sababu ya kudanganya.
You can skin me but kwenye hili I will remain with my stance. Maandamano halali hufuata taratibu. Serikali ilkataa Maandamano siku ya uchaguzi. Kwa hiyo hata hao unaosema walikuwa wanandamana bila mabango na hawakufanya uharibifu na wizi nao walikuwa ni sehemu ya uhalifu.

Tukianza kukaidi maelekezo ya viongozi wetu tunajenga taifa la hovyo na la hatari
 
Waliofanya uhalifu pamoja na waliochochea waandae mawakili wabobevu kwa sababu kesi za ugaidi zinawahusu. Watu wengi wataozea jela kwa kuponzwa na Mange.
 
Hata haohao wachache bila ule uharifu polisi hawakua na shida nao kabisa, watu wamekaa makundi makundi tangu kunakucha.

Shida ni wale wezi na waharibifu.
Na kama ulivyoandika wezi walipomaliza shughuli waliingia mitini wakajifungia, wakisubiri waende sehemu nyingine ambayo ulinzi mdogo wakiwashe wabebe mali wakatulie.

Wale sasa ambao wako varandani, mtaani kwao na majumbani wakiamini wako salama, ndio wakawa wahanga wa risasi.

Wale wanaoratibu maandamano, wawaase wafuasi wao juu ya uharibu wanaoufanya.
Vifo vinauma na hasara zisizo na msingi zinauma pia.
 
I have much respect kwako mtibeli, but siwezi soma makala ndefu kiasi hicho. Ungefanya summarize ungeeleweka. Tukiacha na maandamano na vurugu, unazungumziaje kura alizopata mh rais Dr Samia Suluhu Hassan?
Tunaambiwa alipata kura zaidi ya 31+ millions. Na ni sawa na % 98.
Hapa nilipokuwepo, jimbo zima la kilombero ninauhakika kwa 100000% kwamba Samia hakupata kura 4000. Walitangaza zaidi ya kura 40,000.

Kifupi tumepigwa Angani na ardhini. Tumepigwa barabarani kwenye maandamano na tumepigwa kwenye sanduku la kura.
 
I have much respect kwako mtibeli, but siwezi soma makala ndefu kiasi hicho. Ungefanya summarize ungeeleweka.
Hii haikuwa makala mkuu ilikuwa kama ripoti na simulizi ya nilichoshuhudia

Tukiacha na maandamano na vurugu, unazungumziaje kura alizopata mh rais Dr Samia Suluhu Hassan?
Tunaambiwa alipata kura zaidi ya 31+ millions. Na ni sawa na % 98.

Kama nitakuwa mkweli ni kwamba hayo matokeo ni uongo mtupu. Hilo mtu yeyote hata angejizima data vipi anajua matokeo yale ni uongo.

Hapa nilipokuwepo, jimbo zima la kilombero ninauhakika kwa 100000% kwamba Samia hakupata kura 4000. Walitangaza zaidi ya kura 40,000.

Kifupi tumepigwa Angani na ardhini. Tumepigwa barabarani kwenye maandamano na tumepigwa kwenye sanduku la kura.

Ilikuwa zaidi ya uhuni, umafia na uchafuzi.
 

Nataka nikufahamishe kuwa maandamano kwa kiasi kikubwa hasa ukanda wa Morogoro road yalichochewa na vijana ambao harakaharaka ungewaona kama watumiaji wa mihadarati.
Sitaingia sana huko lakini watu wa kawaida, kama walokole, wasabato au watu wa dini dini ile shughuli wasingeweza

Baada ya moto kukolea ndio makundi mengine mpaka watu wa kawaida walijitosa kuingia kwenye mchezo.

Hofu yangu ni kuwa, jambo kama hili litafutiwe dawa lisitokee tena.

Kwani ikitokea limetokea kuna watu watapasuka vibaya hasa watu maarufu na wanaojulikana.
 
Waliofanya uhalifu pamoja na waliochochea waandae mawakili wabobevu kwa sababu kesi za ugaidi zinawahusu. Watu wengi wataozea jela kwa kuponzwa na Mange.

Hakuna kitu kama hicho.
Hapo busara ndio muhimu zaidi kuliko ulichoshauri kwa hali iliyopo
 

Unahoja lakini waandamanaji nao wanahoja.
Viongozi wasiposikiliza baadhi ya wananchi kwenye mambo nyeti unategemea jambo gani?
Mfano mambo ya wasiojulikana na utekaji tangu kuanza mpaka leo nini kimefanyika?
 
Unaonekana ulikuwa undercover/askari kanzu wa kuwachomesha waandamanaji, maana kila tukio ulilishuhudia.

Undercover ningekuja kuandika hapa?
Tumia akili yako vyema Mkuu.

Sijashuhudia kila kitu. Mji wa Dar ni mkubwa sana. Yapo maeneo mengi sana sijashuhudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…