Mzalendo ni mtu gani na uzalendo ni nini?(Patriotic vs Patriotism)

Seth saint

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2020
Posts
2,262
Reaction score
5,885
Habari za wakati huu.

Nipo hapa baada ya kupata wakati mgumu kuelewa watanzania ni watu wa namna gani ndio maana nimekuja na mada hii.

Kuna kitu huwa tunaelezwa ambacho ni uzalendo.Kwa tafsiri yangu ambayo inaweza isiwe universal.Uzalendo(patriotism) ni mapenzi ambayo mtu anakuwa nayo kwa taifa lake.Mtu huyu ataitwa mzalendo na atalipenda taifa lake kwa kuheshimu sheria na taratibu za taifa husika,tamaduni,historia na mambo yote katika taifa husika ambayo yamekubalika na watu wote.

Kwa Tanzania hili jambo ni tofauti.Watu wanachanganya mapenzi kwa viongozi wa taifa na uzalendo.Mtu akiwa sio mfuasi wa kiongozi husika katika taifa anaokena sio mzalendo(hii ni shida kubwa).Kiongozi utawala wake unakuwa na ukomo lakini taifa linabaki.Sasa ni kwanini watu mnachagua ku-pledge loyalty kwa viongozi na sio taifa?

Mwaka 2013 nikiwa katika mafunzo ya kijeshi 824 KJ tulifundishwa somo la uzalendo.Somo lilikusudia kutufunza kupenda taifa letu(nashukuru Mungu kuna kitu nilijifunza).Serikali ilikuwa inatenga bajeti nzuri kiasi kwamba tulikuwa tunahudumiwa vizuri,ikiwa pamoja na kupatiwa posho za kujikimu.Ni gharama kubwa zinatumika.Hizi ni kodi za watanzania.Lakini je,mbona neno uzalendo linatumika vibaya hapa kwetu?kuna sababu gani ya kutenga tena hizi bajeti kupeleka vijana mafunzo ya JKT wakajifunze uzalendo wa kupenda viongozi na sio taifa?

Tutafakari kwa pamoja hapa.Mapenzi kwa viongozi hayakatazwi lakini mahaba yakizidi tunapoteza taifa.Mapenzi kwa taifa ndio ya kweli na ndio ujenzi wa taifa letu.

Asante na siku njema
 
Mtu mwenye akili nzuri hawezi kuwa mzalendo.

Wale wanaoshikwa akili ndio wanauwezekano mkubwa wa kuwa wazalendo. Wenye akili iliyotulia hadi wakipende kitu lazima wawe na maslahi nacho wala si kushawishiwa na wengine.
 
Kwahiyo kiongozi tuzamishe taifa sio?

Maslahi binafsi sikatai lakini hapa tunaangalia picha kubwa.Kama ideology za ubinafsi zikaingia maana yake ni kwamba unaruhusu mwenye nacho akandamize asiye kuwa nacho.Hii itabariki mauaji na utekaji kitu kinachoweza kuleta class struggle
 
Hoja yangu ni kwamba, ili uwale mzalendo lazima uwe mtu uliyepandikiziwa imani fulani kuhusu nchi yako. Na mara nyingi watu wengi ambao wako smart huwa hawakubali kupandikiziwa tu imani fulani, wao sio watu wa kuamini tu bali ni watu wanaipenda logic Ili kukubaliana na jambo.

Hata hivyo, watanzania ambao ni wazalendo ni wachache sana. Kinachofanya kwa kiasi fulani mambo yaende ni kwamba watu wanabanwa na sheria.
 
Shida kubwa sana hii.Hili taifa linaweza kuzama muda wote wote.Kama idadi ya watu ambao ni loyal kwa hili taifa ni ndogo sana basi ni kazi kweli kweli, maana pakitokea msukumo wa nje ni kwamba tumeisha wote sasa.
 
We ulitaka iweje mkuu. Uzalendo kwako ni nini?
 
Uzalendo nimeeleza kwa tafsiri yangu ambayo inaweza kuwa tofauti na wengine lakini kuna vitu muhimu lazima vionekane ukiongelea uzalendo navyo ni:Kuheshimu sheria na taratibu za nchi,utamaduni,historia ya taifa,watu na rasilimali za taifa.Mengine yanaweza kuongezekana lakini hayo ni mambo ya msingi sana
 
Mfia dini,
mzalendo,
shabiki lialia wa soka,
mbaguzi wa rangi.

Wote hawa ☝️ nawaweka katika kundi la watu wanaopaswa kuwahishwa Mirembe kwa msaada zaidi.
 
Mzalendo ni mtu tofauti na shabiki wa soka na mbaguzi wa rangi kiongozi.Kuhusu wafia dini sitaweka neno maana wanadai imani ndiyo inawaongoza lakini huku kwingine reasoning ni nguzo kuu
 
Uzalendo nimeeleza kwa tafsiri yangu ambayo inaweza kuwa tofauti na wengine lakini kuna vitu muhimu lazima vionekane ukiongelea uzalendo navyo ni:Kuheshimu sheria na taratibu za nchi,utamaduni,historia ya taifa,watu na rasilimali za taifa.Mengine yanaweza kuongezekana lakini hayo ni mambo ya msingi sana
Kuheshimu sheria na taratibu za nchi ndicho kitu pekee kinachofanya kuwe na kaunafuu kidogo . Hakuna uzalendo kabisa.
 
Hapa JF unakanywa na waliokuwa CCM
Screenshot_20260726-212613.png
 
Mzalendo ni mtu tofauti na shabiki wa soka na mbaguzi wa rangi kiongozi.Kuhusu wafia dini sitaweka neno maana wanadai imani ndiyo inawaongoza lakini huku kwingine reasoning ni nguzo kuu
Mzalendo kwa maneno machache yukoje? Hebu mfafanue kwa maneno machache sana.
 
Uzalendo ni kulitumikia taifa lako kwa moyo wako wote na kuwa tayari kulifia.
Kuna wengibe wanafikiri uzalendo ni kuvaa tai ya bendera ya taifa au kwenda ikulu na kuimba nyimbo za kuwasigia uongozi.
 
Back
Top Bottom