Habari za wakati huu.
Nipo hapa baada ya kupata wakati mgumu kuelewa watanzania ni watu wa namna gani ndio maana nimekuja na mada hii.
Kuna kitu huwa tunaelezwa ambacho ni uzalendo.Kwa tafsiri yangu ambayo inaweza isiwe universal.Uzalendo(patriotism) ni mapenzi ambayo mtu anakuwa nayo kwa taifa lake.Mtu huyu ataitwa mzalendo na atalipenda taifa lake kwa kuheshimu sheria na taratibu za taifa husika,tamaduni,historia na mambo yote katika taifa husika ambayo yamekubalika na watu wote.
Kwa Tanzania hili jambo ni tofauti.Watu wanachanganya mapenzi kwa viongozi wa taifa na uzalendo.Mtu akiwa sio mfuasi wa kiongozi husika katika taifa anaokena sio mzalendo(hii ni shida kubwa).Kiongozi utawala wake unakuwa na ukomo lakini taifa linabaki.Sasa ni kwanini watu mnachagua ku-pledge loyalty kwa viongozi na sio taifa?
Mwaka 2013 nikiwa katika mafunzo ya kijeshi 824 KJ tulifundishwa somo la uzalendo.Somo lilikusudia kutufunza kupenda taifa letu(nashukuru Mungu kuna kitu nilijifunza).Serikali ilikuwa inatenga bajeti nzuri kiasi kwamba tulikuwa tunahudumiwa vizuri,ikiwa pamoja na kupatiwa posho za kujikimu.Ni gharama kubwa zinatumika.Hizi ni kodi za watanzania.Lakini je,mbona neno uzalendo linatumika vibaya hapa kwetu?kuna sababu gani ya kutenga tena hizi bajeti kupeleka vijana mafunzo ya JKT wakajifunze uzalendo wa kupenda viongozi na sio taifa?
Tutafakari kwa pamoja hapa.Mapenzi kwa viongozi hayakatazwi lakini mahaba yakizidi tunapoteza taifa.Mapenzi kwa taifa ndio ya kweli na ndio ujenzi wa taifa letu.
Asante na siku njema