KERO Mzani wa magari wa Njiro, Arusha ni mbovu na fedha zinakusanywa kimazoea

KERO Mzani wa magari wa Njiro, Arusha ni mbovu na fedha zinakusanywa kimazoea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakuu,

Hapa Arusha kuna mzani moja wa Jiji iliyopo maeneo ya Njiro, baada tu ya roundabout ya Impala.

Mzani huu naufahamu huu mwaka wa tatu. Kila gari kubwa linalopita hapa linatozwa kati ya 5,000 hadi 10,000, lakini la kushangaza ni kwamba mzani haugfanyi kazi, yaani ni mbovu, ila fedha zinakusanywa kimazoea.

Ukishalipia, basi kupima gari sio shughuli yao tena. Kuna hadi watu wa jiji wanakagua risiti za malipo, lakini huduma ya kupima gari hakuna kabisa.

Huu ni ufisadi uliotukuka. Mamlaka husika zijitafakari, na TAKUKURU iingilie kati suala hili. Malipo yawe na mrejesho wa huduma stahiki.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom