Mzani wa ubaya ndani ya CHADEMA umeelemea upande wa Lissu!

Lisu aliona ndani ya CDM hakuna tena anayeaminika

Sasa ameamua kusimama pekee yake na anakwenda kushinda

Naimani Lisu ni mmoja ya watu wanaojua mengi sana ya nchi hii kuliko yoyote ...
Hata mimi ananizidi kilaza Lisu?
 
Mkuu, CHADEMA wamejitanabahisha kama chama chenye msimamo mkali dhidi ya ufisadi na kukosekana kwa maadili ndani ya serikali na makada wake kama Lissu, Wenje, Lema na wengineo wakiwa firebrands (vichomi) kabisa katika kupambana na serikali kuhusu tuhuma mbalimbali za kifisadi.

Kwa mazingira hayo, kitendo cha kada muhimu Wenje kuwa na "dili" na huyo Abduli bila kuchukuliwa hatua yoyote tena akikubaliwa kugombea umakamu mwenyekiti wa chama, ni kielelezo tosha kuwa kutakuwa na MATATIZO MAKUBWA SANA ndani ya CHADEMA. Kama Wenje ni "mtu wa Mbowe" huu ni msiba.

Nashindwa kupata picha. Wenje aliwezaje kumfuata Abduli na kisha kumpeleka kwa Lissu eti "amsaidie" kupata malipo yake (ya halali) serikalini?!! Alitoa wapi huo ujasiri? Lissu ninayemfahamu ni bora azikose hizo hela kuliko kuweka dili na mafisadi wanaohujumu taifa wakati huu. Mtikila alipokea hela za Rostam na kufifia. Sioni Lissu akiruhusu hali hiyo.

Mkuu, kwa andiko lako hili umeshusha hadhi uongozi mzima wa CHADEMA!

Unakubali tukubaliane kuwa CHADEMA si chama makini cha upinzania tena bali A BIG POLITICAL HOAX?
 
Mkuu kwanza nakubali kitendo kilichoelezewa na wenje hakina picha nzuri sana kwa jamii inayolilia usawa, ilitakiwa upatikanaji wa haki usiwe kwa kujuana na kona kona nyingi hivi(hata hivyo uhalisia ni kwamba tuko mbali sana na mfumo huo wa kupata haki/stahiki). Jambo ambalo mimi haliniingii akilini huu ulikuwa ni ufisadi au hongo ya kimfumo ndani ya CHADEMA.

Kitu ambacho nakiona kwa CHADEMA kuna kuchokeshwa au kuchoshwa (fatigue) na jinsi wamefanya siasa za harakati kwa muda mrefu bila mafanikio au kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa raia kwa aina hiyo ya siasa, hapo ndipo yakaja mambo ya maridhiano na hata kutumia njia zile wengine wanazozitumia kupata haki zao ikiwemo hiyo ya kumuangukia Rais.

Mkuu fikiria umedhulimiwa kiwanja, umepigwa dana dana kuipata haki yako idara ya ardhi na kesi mahakamani imekuwa mzunguko usioisha, halafu kuna Makonda ambaye huyakubali mambo yake mengi na unajua sio msafi lakini unajua ukimueleza kwa sababu zake za kisiasa atakusaidia kutatua shida yako na utapata haki yako, utafanyaje?!
 
Mkuu uko sawa lisu alipata madhara sana baada ya lile shambulio hali imepelekea ubongo kuwa na matatizo. Leo anasema hivi kesho vile yaani kwa ufupi jamaa hajielewi. Mbowe asikubali kuachia hicho kitu ni hatari sana.
 
Kwa mahakama zetu hizi ambazo kila wakati zinakuwa remoted by ule mhimili uliojichimbia chini zaidi sijui kama angeweza kupata haki yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…