Mzazi alomfikisha Mahakaman Mwl Madrasa Kwa kosa la kuchapa watoto, akemewe popote pale anapoonekana na ikiwezekana Jamii imchukulie hatua

Kwani madrasa kunafundishwa nini hasa? Labda tuanzie hapo!
 
100% Fact
 
Kusema kweli ukipata elimu ya dini (Islamic),ni jambo jema sana,, tatizo tu ni waalimu wachache sana wa madrasa waliojifunza pia saikolojia,kitu ambacho ni mhimu kwa mwalimu yoyote yule.
Mi nakumbuka hadi leo,jinsi mwl wangu fulani wa madrasa alivokuwa akitoa adhabu yakukuchapa viboko uku umeshika masikio, ilikuwa inaumiza kwa kweli hata kisaikolojia,sijui kama mmeelewa hiyo adhabu,yaani unainama unapitisha mikono kati ya mapaja kwa nyuma ili ushike masikio, inamaana makalio yanakua juu,mboko ikipigwa sasa inaingia kisawasawa,mungu anisamehe hadi leo uwa namuona msikitini huyo mwalimu,kwasasa aumwa pia huwa naishia kumsalimia tu,lkn moyoni namchukia,hii hali hainitoki.
Nilisoma hadi karibia kiwango cha kati,lkn uenda ningekuwa mbali,dizaini ya walimu hawa ilichangia kiasi fulani kutia ugumu katika elimu hizi,ni hiyo historia yangu kwa ufupi.
 
Umelewa alkasusu bila shaka!
 
hizo fimbo ndio zilikufanya mpaka ukafika kiwango cha kati. Mtume MUHAMMAD (s.a.w) mwenyewe alibanwa mbavu na malaika Jibril (Gabriel) a.s pale alipoletewa ufunuo kwa mara ya kwanza na kuambiwa SOMA! akajibu siwezi kusoma...akaminywa mbavu hizi mpaka zikakaribia kukutana...akaambiwa tena SOMA! akaminywa kama mara tatu ndio akaambiwa tena SOMA kwa jina la Mola wako aliyekuumba...Akaweza kusoma.

Ila wewe leo hii unataka elimu ilukae tu kimayai mayai utadhani unakopi na kupaste vitu vyenye flash disk
 
Hivi nyie mnaoona alichofanyiwa Mwl ni sawa, mna akili TIMAMU kweli??.

Mnataka Taifa liwe na kizazi Cha aina gan? Kizazi ambacho kitaona kuonywa ni makosa ?.

Dini humstaharibisha MTU, Mmejaa Ukristo wa ajabu ajabu ,Ukiristo usokua maadili .


BIBLIA inaonya kutomnyima mtoto fimbo
 
Unaifahamu sheria ya viboko?
 
Mtaani kwetu wengi ni waislamu
Watoto wanatoka shule saa 11 au 12 wanakula wanaenda madrasa kurudi saa 4 usiku. Kesho tena wanaamka saa 11 ili saa 12 wawe shule.
Utakuwa unakaa uswahilini sanaa
 
Mtaani kwetu wengi ni waislamu
Watoto wanatoka shule saa 11 au 12 wanakula wanaenda madrasa kurudi saa 4 usiku. Kesho tena wanaamka saa 11 ili saa 12 wawe shule.
Uko kwenu wamezidisha madrasa nyingi mwisho saa mbili baada ya swala watoto wanarudi nyumbani
 

Simaanishi hivyo mkuu,sawa adhabu itolewe,lkn iwe kulingana na uzito wa kosa,,itakuwaje uchapwe viboko kwa kushikishwa masikio,kwa kosa lakuchelewa kuingia darasani!!!sio kwamba umetoroka darasani au umemtukana mwalimu au umepigana!!
 
Hata Biblia katika kitabu cha methali inahimiza kuwachapa watoto ili kuwaokoa na tabia mbovu

Methali 23:13-14

"Usiache kumrudi mtoto;
ukimchapa kiboko hatakufa.

Ukimtandika kiboko,
utayaokoa maisha yake na kuzimu"
 
Simaanishi hivyo mkuu,sawa adhabu itolewe,lkn iwe kulingana na uzito wa kosa,,itakuwaje uchapwe viboko kwa kushikishwa masikio,kwa kosa lakuchelewa kuingia darasani!!!sio kwamba umetoroka darasani au umemtukana mwalimu au umepigana!!
Hata klabu za mpira mchezaji akichelewa mazoezini hupewa adhabu na kutozwa faini. Chelewa kazini halafu uone bosi wako kama atakuchekea.

Mwalimu anapokuchapa unaona kama anakuonea ila haya masomo ni kwa ajili ya kukuandaa na maisha yako ya baadae. Masuala ya uchelewaji ni hulka zetu watanzania kwasababu ya tabia hii kutokukemewa kwa watoto matokeo yake wanakua nayo tabia hii hata katika maisha yao ya kila siku
 
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaihisha mamaye” (Methali 29:15).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…