KERO Mzazi Atoa Sehemu ya Mchango, Lakini Mtoto Anyimwa Chakula Shuleni

KERO Mzazi Atoa Sehemu ya Mchango, Lakini Mtoto Anyimwa Chakula Shuleni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Weatired

New Member
Joined
Sep 21, 2026
Posts
1
Reaction score
2
Serikali inahimiza utoaji wa chakula shuleni ili kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya kupata chakula. Lakini kuna baadhi ya walimu na kamati za shule ambao wanashindwa kuratibu jambo hili kwa haki.

Kwa mfano, utaratibu unaweza kuwa mwanafunzi anatakiwa kuchangia jumla ya madumu 15 kwa mwaka, mahindi madumu moja na fedha Shilingi 10,000. Sasa inakuwaje mzazi ambaye ameshatoa robo tatu au nusu ya mchango wake, mtoto wake ananyimwa chakula?

Namaanisha, kwa mfano, kwa muhula mmoja mahitaji ni madumu 7.5. Mzazi ameshatoa madumu 4, fedha badala ya Shilingi 5,000 kwa nusu muhula ametoa Shilingi 3,000, pamoja na mahindi nusu dumu. Kwa nini mtoto huyo anyimwe chakula?

Tuseme mzazi, kutokana na changamoto za maisha, ameshindwa kukamilisha mchango wote katika kipindi cha Julai hadi Septemba, lakini tayari ameshatoa kiasi fulani. Mtoto akinyimwa chakula hadi mwezi wa Septemba, halafu akapewa kuanzia mwezi wa Septemba na shule ikafungwa mwezi wa Desemba, je, si mtoto huyo atakuwa amepoteza sehemu ya haki yake ya chakula ambayo mzazi wake alikuwa tayari ameshachangia?

Kama mzazi ametoa robo ya mchango, hesabu ni rahisi. Kama nusu ya mchango inahusisha miezi sita, basi mtoto apewe chakula kwa miezi mitatu kulingana na mchango uliotolewa. Baada ya hapo, mzazi akumbushwe kukamilisha mahitaji yaliyobaki ili mtoto aendelee kupata chakula.

Kwa nini isiwe rahisi hivyo ikiwa kuna uratibu mzuri?

Kumnyima mtoto chakula wakati unajua mzazi wake tayari ameshatoa sehemu ya mchango ni jambo lisilo sahihi na linaweza kumuathiri mtoto ambaye hana kosa lolote.

Walimu wakuu na kamati za shule, tafadhali fanyeni hesabu na uratibu wa michango kwa haki. Lengo ni kuhakikisha mtoto anapata chakula kulingana na mchango uliotolewa, huku mzazi akiendelea kukumbushwa kukamilisha sehemu iliyobaki.

Inadaiwa hali hii inatokea katika Shule ya Msingi Lipupuma, Mshangano Kati, na Sekondari ya Luhila, Manispaa ya Songea, Mtaa wa Mshangano.

Wazazi wanahitaji utaratibu wa haki, uwazi na unaomlinda mtoto.
 
Katika vitu ambavyo ni vya kuepuka ni hivyo. mzazi hutakiwi kwa namna yoyote kufanya mwanao akose vitu muhimu
kama ni michango ya shule sijui chakula jipangie utaratibu maalumu ili mtoto asikose huduma.

Mtoto kukosa huduma za msingi au kuwa nje ya utaratibu kutamfanya ajiunge au apate vishawishi visivyo vya lazima.
 
Back
Top Bottom