Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Umeanza kuamini hivo before au after kujitegemea?
Mimi nimetaka kuslim since niko kidato cha pili lakini sikuwahi fanya hivyo kwasababu nilijua home hakuna anayeweza kunielewa.
Nlipoendelea kukua nikaenda chuo hata kuslim nikaachana na habari hiyo nikawa mtu wa kusoma maandiko mengi ya imani mbalimbali iwe hindu, mabudha, usilamu, chochote tu. Since then nimekuwa hivyo. Siamini katika madhehebu ila naamini Mungu yupo and I pray in my own way.
Nlipomaliza chuo sikuwahi rudi ishi na wazazi so mpaka leo hakuna anayejua naamini nini au kama nimebadilika.
Kuna muda huwa naenda kansani labda kwa mika 7 iliyopita nmeenda kama mara 3 au 4 ila kwa matukio ya ibada za kumwaga marehemu n.k.
Personally, nikiamua kuwa mfuasi wa dhehebu kwa sasa, nadhani ninaweza kuslim
 
Mkuu wewe huamini uwepo wa Mungu, au huamini njia zinazotumika kumfuata huyo Mungu!?

Unakuaje hudhani wakati wakati huakini kama yupo!!

Mtakuja kukosana tu ni kheri ukahama hapo kwenu.
Siamini, ila najaribu kufikiria kwa kitu anacholazimisha nikiamini...mbona kitu chenyewe hakipendi mtu alazimishwe kukiamini?
 
Hivi ulianzisha uzi kuomba ushauri au kubishana na watu wenye mtizamo tofauti na wako juu ya jambo ulilouliza...!? Nilidhani unalinganisha unachoambiwa na mtazamo wako kuona kipi ni sahihi
Sijaomba kuhubiriwa.
Ushauri ulio ndani ya mada nasikiliza, ila hizi porojo nyingine za kutaka niamini mambo ya Mungu naweka pembeni.
 
Poor you!
Nimekuhurumia,baada ya mda utakuja kugundua mama yako alikua sahihi ila nasikitika utakuja kugundua when it is too late,
Social media hizo zinawaharibu,nna hakika we snap chat na tiktok haukosi kwenye simu yako,basi tuseme nini sasa!
Mungu amtunze bimkubwa wako aishi ashuhudie yajayo!
Sina tiktok wala snapchat. ila najua nyie kanisani ndio huwa mnazitumia sana.
 
So akikukwambia kwa kukuimiza uende disco...utazame TV kutwa ...umleta bwana ako home ulale naye ....uwe unywe pombe ...n.k...je nako utaona kakulazimisha au kaingilia Uhuru wako!?
Akinihimiza hajanlazimisha au kuingilia uhuru wangu, ila akianza kusema ukiwa chini ya paa langu LAZIMA uende disco, utazame Tv kutwa na ulete bwana wako home ulale naye...atakuwa ameingilia uhuru wangu.
 
Sasa kama imani yangu haimhusu...nikiwa siamini Mungu naenda kanisani kufanyaje?
Unaenda kutekeleza amri yake.
Na hiyo itaonyesha kuwa unatii mamlaka ya hapo NYUMBANI.

Sio kila kitu ukiambiwa ufanye lazima uamini au ukikubali. Vinginevyo hujui maana ya sheria au Amri.

Serikali ikikuambia ulipe Kodi, Hilo suala halina mjadala, kwamba unaamini au huamini, unaafiki au hauafiki. Hapo ni utekelezaji tuu.

Serikali ya NYUMBANI pia haiangalii watoto mnaamini au mnakuvali nini. Inachotaka ni utekelezaji, Basi.

Hiyo ndio shida ya Kukosa malezi ya Baba.
Mama Yako yupo vizuri Ila mtoto ndio cherema
 
Nenda kanisani mfurahishe bimkubwa halafu siku ukitoka kwake endelea kuamini unachoamini mfano shetani nk.

Kila mtu atakufa na kuzikwa kivyake haya mambo ya kulazimisha imani ni primitive!

Ni ajabu misaada ya kuendesha shughuli za makanisa inatoka ulaya ambako sote tuko huku ni wapagani, makanisa ni kumbi za kufanyia sherehe za kijamii!!

Ukimtoa mtu bongo yuko kanisani ukiwa umemfunga macho uje umtue kanisani hapa ulaya ataanguka na kufa hapo hapo hataamini kwa kuona kanisa zima tunafanya sherehe za kitaa tunacheza muziki na kunywa pombe na baadae tukimaliza tumelewa tutaondoka na atasali peke yake!!

Kuna vitu vya kanisa ni majaribu na inatakiwa kuamini kwa hiari mf

1. Stori ya Yesu kufa na kufufuka na kupaa ni puzzle maana kwenye maisha yetu ya Buza kitaa hiyo haipo! Mtu akifa kafa na binadamu hana mabawa ya kuruka kwenda juu angani kama ndege tena muvi inaonesha eti Yesu anaruka juu sote tunaona hizi ni kamba kabisa mchana kweupe kwa mtazamo wetu masela wa huku Buza, mama yetu alikufa miaka 20 long fucking hakuamka tena that day hadi leo ni huzuni tupu.

2. Yesu kufa kwa ajili yetu ni puzzle maana binadamu by nature ni selfish hakuna mtu wa kuhangaika na shida za watu kibao dunia nzima wasio ndugu zake. Hizi ni kamba pia huku Buza masela wananiunga mikono na miguu!

3. Yesu ni Mungu ni puzzle kubwa sana maana Mungu anaumba sasa haiwezekani Mungu (Yesu) akaumba binadamu halafu binadamu wakamuua Mungu aliewaumba (Yesu) msalabani, hizi ni kamba pia huku Buza kitaa supu ya makongoro na mataputapu!

4. PUZZLE ni kama Yesu ni sehemu moja ya Mungu (Mungu Mwana) basi alipokufa msalabani Israel sehemu mbili za kukamilisha Mungu wa utatu nazo pia zilikufa (Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu nao walikufa maana Mungu Mwana alikufa au Yesu) meaning dunia haina Mungu tangu ile siku Yesu aliuwawa! NDO maana viongozi ni watesi sana wanaweka matozo, tunarundikwa kama nyanya kwenye mabasi ya mwendokasi, wanakata umeme huku Buza tu Masaki upo, wanatufungia barabara kila siku na kututesa na joto na foleni. Mungu Baba atatulipia maana Mungu mwana alikufa msalabani

5. Biblia imeandikwa miaka mingi baada ya Yesu kufa na imeandikwa na watu ambao hatuwajui na hatuna uhakika waliyoyaandika waliyatoa wapi hivyo tuna hiari kuamini au kutoamini maneno ya Biblia hivyo ina maana si lazima kwenda kanisani kusoma maneno ya watu!

Je unawezaje kumsema na kumchukia mtoto mtukutu kuwa ana pepo na masheitwani kwa matendo yake mabaya kama huwezi kutuonesha hayo mapepo tukayaona kwa macho yetu sasa kwanini uchukie kama hatukubali imani yako? Kwanza stori mapepo kama stori zingine ziliandikwa na watu na mi mnisaidie kuelewa namna ya kujua kama walisema kweli au la?
 
Alafu kitu kingine usichokijua ni kuwa Kitendo cha kufuata sheria za Iran au Saudia ukiwa katika nchi hizo unakuwa muislam indirect way. Licha ya kuwa huendi msikitini. Kwa sababu dini nikufuata sheria na taratibu zilizoanishwa katika vitabu.

Dini inasema muumini lazima kuswali.
Kuna nchi inalazimisha watu kuswali?
Mbona upeo wenu 'wasomi' ni mdogo hivi?
 
Mimi nimetaka kuslim since niko kidato cha pili lakini sikuwahi fanya hivyo kwasababu nilijua home hakuna anayeweza kunielewa.
Nlipoendelea kukua nikaenda chuo hata kuslim nikaachana na habari hiyo nikawa mtu wa kusoma maandiko mengi ya imani mbalimbali iwe hindu, mabudha, usilamu, chochote tu. Since then nimekuwa hivyo. Siamini katika madhehebu ila naamini Mungu yupo and I pray in my own way.
Nlipomaliza chuo sikuwahi rudi ishi na wazazi so mpaka leo hakuna anayejua naamini nini au kama nimebadilika.
Kuna muda huwa naenda kansani labda kwa mika 7 iliyopita nmeenda kama mara 3 au 4 ila kwa matukio ya ibada za kumwaga marehemu n.k.
Personally, nikiamua kuwa mfuasi wa dhehebu kwa sasa, nadhani ninaweza kuslim
Okay, got you.
 
Unaenda kutekeleza amri yake.
Na hiyo itaonyesha kuwa unatii mamlaka ya hapo NYUMBANI.

Sio kila kitu ukiambiwa ufanye lazima uamini au ukikubali. Vinginevyo hujui maana ya sheria au Amri.

Serikali ikikuambia ulipe Kodi, Hilo suala halina mjadala, kwamba unaamini au huamini, unaafiki au hauafiki. Hapo ni utekelezaji tuu.

Serikali ya NYUMBANI pia haiangalii watoto mnaamini au mnakuvali nini. Inachotaka ni utekelezaji, Basi.

Hiyo ndio shida ya Kukosa malezi ya Baba.
Mama Yako yupo vizuri Ila mtoto ndio cherema
Wewe dini tu ndio imekuathiri mpaka ufikirie hivyo.
Kulipa kodi ni jambo la kiimani?
Kwenda kanisani ni jambo la kiimani, ni useless kwenda kanisani pasipo kuamini Mungu. Even a toddler can understand this.
 
Kumbe mungu ni mbaguzi.
Hii umetoa kwenye kifungu gani?

Kuweka Protocol ni ubaguzi?😂😂😂
Ati Una degree😀
Mbona Mama Yako akikulisha hapo NYUMBANI hauiti ubaguzi?
Wewe upo chini ya wazazi, mzazi kapewa mamlaka ya kukulea, kukulisha, kukupa malazi n.k.
Mzazi akukupa chakula husema anaingilia Uhuru wako.
Akikuvisha hausemi anaingilia Uhuru wako.
Alipokuwa anakusomesha haukusema anaingilia Uhuru wako.

Anakuambia uende Kanisani Ari ndio anaingilia uhuru wako? Yaani kuna watu wapumbavu kweli.

Uhuru unaoutaka hauwezi kuipata ukiwa chini ya wazazi. Protocol haipo hivyo.

Na sio tuu wazazi hata siku ukiolewa, unakuwa chini ya Mumeo. Yeye ndio ataamua wapi uende kuabudu. Suala la kuamini utajua mwenyewe akilini na moyoni mwako.

Suleiman aliwahi kusema; Mpumbavu hata umtwange kwenye kinu upumbavu wake hautamtoka.
 
Nenda kanisani mfurahishe bimkubwa halafu siku ukitoka kwake endelea kuamini unachoamini mfano shetani nk.

Kila mtu atakufa na kuzikwa kivyake haya mambo ya kulazimisha imani ni primitive!

Ni ajabu misaada ya kuendesha shughuli za makanisa inatoka ulaya ambako sote tuko huku ni wapagani, makanisa ni kumbi za kufanyia sherehe za kijamii!!
Sawa Zuga nmekupata, wacha niendelee kuzuga
 
Back
Top Bottom