Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Wewe inakuuma nini mtu mzima kufuata imani anayoitaka??
Kesho utaanza kusikia anafanya meditation,oo Mungu Ni energy,ukifa utazaliwa panya ndio hao watu waliomezeshwa falsafa za kishetani
 
Siamini, ila najaribu kufikiria kwa kitu anacholazimisha nikiamini...mbona kitu chenyewe hakipendi mtu alazimishwe kukiamini?
Huyo ni mzazi mkuu, yani ukitaka akuelewe mtazozana sana.

Hata huyo housegirl hana kosa kabisa ni vile yeye anaamini ni sahihi.
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Watoto wa dizaini yako ni mzigo sana kwa wazazi,umelilea toto vizuri,likishakuwa tena bado liko kwenye himaya yako linaanza kuleta ujuaji,kifupi wewe ni mzigo na pasua kichwa...
 
Uongo mkubwa, kesi za ajabu ajabu za ulawiti zimepatikana kwa ma ustadh na mapadri.
Na wengi wao wanaomkana Muumba wao miongoni mwao ndio wanaofanya maovu na uzinzi na ufiraji na kulawitiwa
 
Kwa nini hawezi?
Maana sio mmeenda kupata vielimu vya kukariri mpaka mnatokwa na akili
Hilo ni jambo la kimila na kiutamaduni ni taboo.
Sijajua kuhusu Tz maana mimi sio mwanasheria, ila nchi nyingi zinakataza kisheria incest.

Logic behind ni kuwa ukiruhusu incest unapunguza variations kwenye genetic pool, kwahyo kukitokea trait mbaya inakuwa dominant kwenye familia/ukoo.
Mfano ikitokea Asthma au ugonjwa wa akili unakuwa dominant kwasababu mnaoana ninyi kwa ninyi.

Kwahyo kiutamaduni ni immoral, na kisheria hairuhusiwi.
 
Haha amwaminiye Mungu ni nabii[emoji23][emoji23][emoji23]
Hali unayopitia ni ule ujana wa maji ya moto.
Kuna saa utazitafuta sana habari ya Mungu.
Namkumbuka babangu ulivyokuaga jeuri kupitiliza lkn ulifika wakati alimtafuta Mungu kwa udi na uvumba.

Wewe vimba tu siku ukitupiwa kajini kadogo kakuhangaeishe weee aash kanisa utalisaka mwenyewe[emoji23][emoji23]
Embu naonba unitupie hilo jini, ntakulipa
 
Nini kinachomfanya mama yako afurahi kwa kukuona tu umefika kanisani kwake?? Kuna tofauti gani na mlevi anayekunywa bia na kusikia raha??
Dah umeniharibia siku. Sikutegemea kusoma uzi wa kipumbavu kama huu. Miaka 24 ni mdogo na ubaya zaidi bado unaishi kwenu. Unajisikiaje unavyoona mama yako ananung'unika kwama hamfuati maelekezo yake? Wengi wetu huku town hatuendi kanisani ila tukifika nyumbani ili kumfurahisha mama ile siku ya ibada unabeba na biblia kabisa. Baada ya ibada lazima umsubiri asalimiane na watu wake kisha mrudi wote nyumbani. Mama akikunung'unikia ni mwanzo wa kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima. Uache upumbavu wewe. Kama hutaki usumbufu hama hapo kajitegemee.
 
Mimi sijui Kama Mungu yupo au hayupo...siajema yupo au hayupo.

Nachosema ni kuwa hawa Mungu (Allah & yahweh) wanaoelezewa kwenye vitabu vya dini ya kikristo/uislam hawapo.
Hakuna ushahidi kama wapo.
Kama unao uweke hapa.

Ni sawa na mimi nikuambie kuwa kuna binadamu mwenye mabawa.
Sasa wewe tayari unajua binadamu yukoje na mabawa yakoje kwhayo kupiga picha binadamu mwenye mabawa sio shida...Shida itakuja kwenye kuniamini mimi kuwa huyo binadamu yupo.
Sio jukumu lako kutoa ushahidi kuwa huyo binadamu hayupo.
Bali ni jukumu langu mimi niliyekuambia kuwa yupo binadamu wa hivyo kukupa ushahidi usio na shaka.

Nikishindwa kukupa huo ushahidi, madai yangu unapaswa uyapuuze lakini hautasema kuwa binadamu wa hivyo hayupo, lakini utasema "Sina ushahidi kuwa binadamu wa hivyo yupo, kwa hiyo siamini yupo...Siku nikipata ushahidi nitaamini yupo"


Ndoivyo sasa kwa Mungu...Kwa hizi dini mbili hawa Mungu wao (Allah au Jehova) anatakiwa awe Na uwezo wote, ujuzi wote na awepo kila mahali.
Sasa bado sijapata ushahidi wa uwepo wake.
Ahsanteeeeeeeeeh!!!
 
Mrembo She Quoted you nasikitika sana kuona unalazimishwa kusali ikiwa hupendi kufanya hivyo.

Mrembo hii ni Africa ukweli ni kuwa una haki ya kuamua usali au usisali ila shida ni hizi akili za wazazi wetu mapopoma wanaohisi kuwa hata ukishakuwa mtu mzima lazima akuendeshe ilimradi yeye inambidi kuwa mshauri tu .

Sasa hiko hivi hapo kwenu ili kuitunza amani kubali tu kwenda huko kanisani ila nenda kujipumzisha poteza muda kama wao watakavyo hii ni kutokana na kuwa huna kwako bado.

Ila ukipata kwako ishi utakavyo ila kuhusu kukulazimisha kusali sikubaliani na mama yako ila ndiyo hivyo sasa upo kwake tii ili maisha yaende.

Ila nje ya mada vipi utaki kuolewa ?[emoji3] Maana yuko mwamba hapa yeye na mambo ya kanisani ni mbingu na ardhi .

Ikiwa uko ready yuko pale anakusubiri pm ukuambie jambo[emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante, wewe ndio uko positive na ushauri wako ni wa maana...Nikuulize kitu, wewe unaamini Katika dini gani?

Kuhusu kuolewa, sina mpango nao kwasasa
 
Una miaka 24 na unaishi kwa wazazi halafu hautaki kufuata masharti yao.

Kama unaona hauwezi kuwasikiliza unapaswa uhame ukaanze maisha yako. Umri unakuruhusu na wala hawatakuuliza ukiondoka. Wewe wape taarifa tu kuwa unahamia kwako.

Ukiendelea kuishi hapo kwao wanakuona mtoto na lazima wakupangie masharti.
Nilishawaambia kuhama wakakataa.
 
Mzazi yupo sawa sababu we ni mtoto wake hataki uharibikiwe na kingine bado unaishi chini ya wazazi wako unatakiwa ufate kile wanachokwambia

Kijana mdogo ushaona dini uliyozaliwa ndani yake uiamini

Acha kujipa usahihi na mzazi wako mzazi huwa hakosei hata siku moja
Wazazi huwa wanakosea mkuu wao si malaika.

Na pia suala la binti kuamini au kutoamini ni lake binafsi kati yake na Mungu, ila kwakuwa anakaa nyumbani hapo ndipo ugumu unakoanzia.
 
Huyo ni mzazi mkuu, yani ukitaka akuelewe mtazozana sana.

Hata huyo housegirl hana kosa kabisa ni vile yeye anaamini ni sahihi.
Mmh sawa, sikuile nilitaka kumpasha na kumchenjia pale sebuleni...ila nikaona mama yupo haitokuwa sawa.
 
Asante, wewe ndio uko positive na ushauri wako ni wa maana...Nikuulize kitu, wewe unaamini Katika dini gani?

Kuhusu kuolewa, sina mpango nao kwasasa
Mimi ni islamic mrembo ila maamuzi ya niswali au nisiswali najaribu kuyaweka kuwa private sio niingiliwe na binadamu yeyote.

Japo kipindi hiko nimewahi kulazimishwa fulani kwa jina la" Da'hwa " ila Mnyazi ni mwema vita nilivishinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom