Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

But as for those who disbelieve, for them is fire of hell; it taketh not complete effect upon them so that they can die, nor is its torment lightened for them. Thus We punish every ingrate.

35:36
Ongezea fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
 
Kama wewe ni me nenda kaangalie wanawake, kama ni ke kaangalie wanaume. Pia kaangalie mitindo ya mavazi na kadhalika.
Kwa kufanya hivi utakuwa umemlidhisha mzazi na ku-enjoy.
 
Eti "nikajua vingi". WakanaMungu bhana. Hujajua kitu kuhusu Uislam bado.

Halafu ndio utakuta mtu kama wewe anasema nimesoma dini zote hakuna kitu sijui. Jamani.

Nyinyi watu ni wajinga halafu mna kibri mno.
Okay sijajua uislam mkuu...it seems uislam ni very complicated subject..binadamu wa kawaida hawezi kuelewa kirahisi.

And if that's so, then kwann mungu aliucomplicate ili wachache waelewe?

Btw, huna jipya la kuniambia kuhusi uislam.
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Kwanini usihamie tu kwako ujitegemee, umri wako tayari
 
Ujue wacha Mungu wengi kwa kawaida na hasa wazazi hupenda kuona nyumnba nzima mkienda Kanisani kiusali, hivyo kama kuna mtu ndani ya nyumba hiyohiyo haendi kusali hujiona kama vile wanaishi na shetani na hivyo ndio maana Mama yako anaumia na kukwazika unapoonekana kutopenda kusali!
Pia kumbuka mzazi atabaki mzazi mpaka kufa kwako hivyo hata kama umejiona umeshaelimika usiwe mbishi kwake au kuwa mtu wa kupingana naye, utajibebea laana zisizo za lazima!
Kwavile bado upo chini yake kama jinsi alivokukumbusha basi endelea kumtii vinginevyo utamkatisha tamaa hata kukupambania katika mambo mbalimbali ili ufanikiwe kimaisha, usikute tangu uko chuo huwa anafunga kufanya sala na maombi kwa ajili hivyo ukimuonyesha kitu cha namna hiyo hakika utakuwa unamuumiza sana!
Bora nenda kanisani hata kwa kumfurahisha yeye tu ila usikaidi completely!
Got you.
 
Wewe ndio una tatizo,tena sio dogo ni kubwa,kama unahisi dini imeletwa na wazungu kwa maana nyingine unasema hakuna Mungu,...kifupi unajiweka kwenye hatari kubwa ktk maisha yako,umri wako ni mdogo sana, mama yako yuko sahihi na ameona mengi ndio maana anakurudisha kwenye njia sahihi,ukikana wosia wake unajiweka kwenye hatari sababu ni kukataa shauri za wazazi na kufuata njia zao wenyewe,tubu hiyo dhambi,mwambie Mungu aondoe hiyo roho ya uasi inayokudanganya kua hakuna Mungu.

Mungu yupo,kama huamini kua Mungu yupo nenda hospital na mochwali ukaone watu walikufa ndio utajua yuko Mungu, usipogeuka hiyo njia unayotaka kuifuata UTAANGAMIA na iko siku utamkumbuka mama yako na maneno aliyokua akikwambia.
 
Kumbe uoga wa kifo ndio unafanya uamini mungu yupo.

Na dini zilianzishwa ili kuwafariji watu wasiogope kifo
 
Kuna mama huwa namuona anaenda kusali kila jumapili na lazima aende na watoto wake kanisani hata katikati ya wiki ila ni mbaguzi sana kwa watoto wasio wa kwake anaoishi nao.
Ujue wacha Mungu wengi kwa kawaida na hasa wazazi hupenda kuona nyumnba nzima mkienda Kanisani kiusali, hivyo kama kuna mtu ndani ya nyumba hiyohiyo haendi kusali hujiona kama vile wanaishi na shetani na hivyo ndio maana Mama yako anaumia na kukwazika unapoonekana kutopenda kusali!
Pia kumbuka mzazi atabaki mzazi mpaka kufa kwako hivyo hata kama umejiona umeshaelimika usiwe mbishi kwake au kuwa mtu wa kupingana naye, utajibebea laana zisizo za lazima!
Kwavile bado upo chini yake kama jinsi alivokukumbusha basi endelea kumtii vinginevyo utamkatisha tamaa hata kukupambania katika mambo mbalimbali ili ufanikiwe kimaisha, usikute tangu uko chuo huwa anafunga kufanya sala na maombi kwa ajili hivyo ukimuonyesha kitu cha namna hiyo hakika utakuwa unamuumiza sana!
Bora nenda kanisani hata kwa kumfurahisha yeye tu ila usikaidi completely!
 
Ongezea fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
And who doth greater wrong than he who is reminded of the revelations of his Lord, then turneth from them. Lo! We shall requite the guilty.

32:22
 
And who doth greater wrong than he who is reminded of the revelations of his Lord, then turneth from them. Lo! We shall requite the guilty.

32:22
Ongezea tena fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakuwahi kukujua, hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
 
Okay sijajua uislam mkuu...it seems uislam ni very complicated subject..binadamu wa kawaida hawezi kuelewa kirahisi.

And if that's so, then kwann mungu aliucomplicate ili wachache waelewe?

Btw, huna jipya la kuniambia kuhusi uislam.
Uislam sio complicated.

Ila wewe hujui kuhusu Uislam. Wewe kutoujua Uislam hakuufanyi Uislam kuwa complicated. Ni wewe ndio haujui. Kama wengine tunavyokuwa hatujui kitu fulani lakini tunakijua tukitafuta Ilmu yake kwa taratibu zake.

Sina jipya la kukuambia kuhusu Uislam? Aisee wewe kweli hujui na hujui kama hujui.
 
Baba yangu ukishabarikiwa utajua na imani Yako na alikuwa mtumsishi wa kanisa .
 
Uislam sio complicated.

Ila wewe hujui kuhusu Uislam. Wewe kutoujua Uislam hakuufanyi Uislam kuwa complicated. Ni wewe ndio haujui. Kama wengine tunavyokuwa hatujui kitu fulani lakini tunakijua tukitafuta Ilmu yake kwa taratibu zake.

Sina jipya la kukuambia kuhusu Uislam? Aisee wewe kweli hujui na hujui kama hujui.
Okay, enlighten me....Nini sijui kwenye uislam?
 
Back
Top Bottom