BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,860
Mzazi ana Jukumu muhimu sana katika Kumlea na Kumkuza Binadamu bora wa kizazi cha baadaye. Kupitia Malezi hayo, Mzazi anapaswa kumsaidia Mtoto Kukua na kuwa mwenye Afya Njema, Furaha na Anayejiamini.
Tafiti mbalimbali zinaonesha baadhi ya Watu wazima waliopitia Unyanyasaji wa aina yoyote katika Umri wa Utoto na hawakupata msaada wa kuziondoa Kumbukumbu hizo, wengi wao huishia kuwa na Tabia zisizofaa au kushindwa kukabiliana na Changamoto za Kimaisha
Makosa ambayo Wazazi hufanya kwenye Malezi na kusababisha Watoto kuishi na Kumbukumbu za Matukio Mabaya (Trauma) kwenye maisha yao
1. Kupuuza mafanikio ya Mtoto wako na kutomsifia anapofanya vizuri
2. Kumkosoa kwa kila kitu anachojaribu kufanya au kuonesha na kumhukumu kwa kila kosa
3. Kumlinganisha Mtoto wako na Marafiki, Ndugu zake au Watoto wa Majirani kila wakati anapokosea
4. Kuonesha wazi una upendeleo kwa ndugu zake wengine na sio yeye
5. Kutamka maneno ya ukali kama 'Ninakulisha, Ninakutunza hapa ndani na ninalipa gharama juu yako lakini hakuna chochote cha maana unafanya'
6. Kulazimisha Mtoto wako atimize Ndoto au matakwa yako ambayo haukuwahi kuyatimiza wakati wako
7. Kutumia muda mchache sana ukiwa na Mtoto wako au kujitenga nao kabisa na kutowaonesha upendo