Mzazi: Mnyama wa ajabu aitwaye upendo wa kweli

ephen_

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2022
Posts
21,002
Reaction score
77,708
Nyuma ya mtoto aliye imara kuna mzazi aliyepambana kimyakimya.

Naona wazazi ni watu wanaotakiwa kuheshimiwa sana. Si kwa sababu tu wanatulea, bali kwa sababu ya uzito wa jukumu walilobeba tangu siku ya kwanza tulipoingia duniani. Uzazi sio tu tendo la kuleta kiumbe hai, bali ni safari ya maisha inayojaa sadaka, upendo usio na masharti, na maumivu yasiyoonyeshwa hadharani.

Ukiwa mzazi unakua na ule upendo ulioandikwa kwenye biblia UPENDO WA AGAPE ule usiochoka, usiotegemea malipo, na usiohitaji sababu. Ni upendo unaokusukuma kukesha usiku mzima mtoto akilia, kukubali kula chakula kilichopoa kwa sababu mtoto alihitaji kushiba kwanza. Ni upendo unaosamehe bila kusema, hata pale mtoto anapokosea kwa makusudi.

Mtoto hata akikosea, baada ya muda mzazi anasahau na kumsamehe hata asipoomba msamaha.
Unajikuta bado unamtafutia maisha bora, unamkubali, unampenda.

Mzazi anapotazama macho ya mtoto wake, anaona wajibu. Ushamleta mtu duniani; unakua na moyo wa kuhakikisha yupo salama kiakili, kimwili apate mahitaji yote. Lakini hiyo siyo mwisho. Bado uhakikishe anakua mtu mwema kwenye jamii. Kama ni mvulana, aje kuwa mwanaume kamili mwenye maadili, heshima, upendo na kujitegemea.

Kama ni msichana, aje kuwa mwanamke kamili mwenye utu, heshima, upendo na kujitambua.
Bado uhakikishe anakua imara kupambana na changamoto za dunia hii.

Ni majukumu mengi, ya kimwili na ya kiroho. Na mara nyingi, mzazi huyafanya yote haya kwa kimya.
Hakuna anayejua kilio cha usiku, hofu ya kesho, na maumivu ya kuona mtoto wako akiteseka.

Ila sasa naona wazazi hua wanapitia mawazo ya kimyakimya. Haya ni mawazo yanayokuja kimya kimya, yakitafuna nafsi kama
"je nitamlea vema? Nitamfikisha alikokusudiwa? Atanielewa? Atanikumbuka?

Siku zote mzazi hutaka mema tu kwa mtoto wake. Unamtunza,
Unamsihi,
Unamwombea.

Lakini kuna wakati anachagua njia tofauti, au dunia inambadilisha. Na hapo ndipo mzazi huumia sana. Maumivu ya mzazi hayapimwi kwa macho ni maumivu ya ndani ya moyo, ya nafsi. Lakini bado yuko tayari kumpokea, kumsamehe, kumpa nafasi ya pili.

Kwa kweli, mzazi ni kiumbe wa kipekee. Anabeba uzito mkubwa moyoni, lakini anaonesha tabasamu usoni. Anapambana kwa ajili ya mtu mwingine kila siku, bila malipo ya moja kwa moja. Na ndiyo maana, mzazi anastahili siyo tu heshima bali shukrani ya maisha yote.

Kwa hiyo, tukumbuke kuwasikiliza wazazi, Kuwaheshimu na Kuwapenda.
 
Ukisha kuwa mzazi ndio unaelewa uzito wa wajibu wa mzazi.
Kwa sababu ya majukumu ya uzazi ngumu tena kumkumbuka mzazi wako inavyo paswa kuwa .
Huwa inauma sana lakini kiujumla maisha si kwa ajili ya furaha ila masumbuko na adha na maudhi na mateso na uchungu mwingi.
 
Umesema sahihi kabisa kwa asilimia kubwa.

Lakini wapo wazazi exceptional wanaowatoa watoto kafara, wanaowauza watoto wao kwa mahari bila kufuata mioyo ya mabinti zao, wao wanachojali ni Pesa.

Wapo wazazi wamezaa watoto kujipatia kipato, hawa Afrika ni wengi Sana.
Kupata vibarua n.k.
 
Malipo ya mzazi wako utayalipa kwa watoto wako.

Kwa familia maskini, kijana yupo kwenye hatari ya kuingia kwenye mgogoro wa nafsi wengine mpaka kufikia kupata Depression kwa kuona wazazi wao wanazeeka bila kuwatendea hata jema moja kama sehemu ya kuwashukuru.

Huku maisha magumu, huku familia yako huimudu, kule wazazi kuwapa shukrani. Hatari Sana
 
Umesema sahihi kabisa kwa asilimia kubwa.

Lakini wapo wazazi exceptional wanaowatoa watoto kafara, wanaowauza watoto wao kwa mahari bila kufuata mioyo ya mabinti zao, wao wanachojali ni Pesa.

Wapo wazazi wamezaa watoto kujipatia kipato, hawa Afrika ni wengi Sana.
Kupata vibarua n.k.
Hili andiko nimejiandikia mimi binafsi.
Sijui kuhusu hao wazazi unaowaongelea lakini.
 
Hili andiko nimejiandikia mimi binafsi. Sijui kuhusu hao wazazi unaowaongelea lakini.

😂😂😂

Usiombe ukaolewa na kupata Wakwe wenye sifa hizo.
Utabadili mtazamo, pale unafungwa usizae na mama mkwe kumkomesha kijana wake anayetekeleza wajibu wake kama mumeo.

Au watoto wako kusumbuliwa,

Au Mumeo kumkatalia binti yenu kuolewa na kijana anayempenda baada ya kuchukua pesa za wenyewe.
 
Nyuma ya mtoto aliye imara kuna mzazi aliyepambana kimyakimya.

Naona wazazi ni watu wanaotakiwa kuheshimiwa sana. Si kwa sababu tu wanatulea, bali kwa sababu ya uzito wa jukumu walilobeba tangu siku ya kwanza tulipoingia duniani. Uzazi sio tu tendo la kuleta kiumbe hai, bali ni safari ya maisha inayojaa sadaka, upendo usio na masharti, na maumivu yasiyoonyeshwa hadharani.

Ukiwa mzazi unakua na ule upendo ulioandikwa kwenye biblia UPENDO WA AGAPE ule usiochoka, usiotegemea malipo, na usiohitaji sababu. Ni upendo unaokusukuma kukesha usiku mzima mtoto akilia, kukubali kula chakula kilichopoa kwa sababu mtoto alihitaji kushiba kwanza. Ni upendo unaosamehe bila kusema, hata pale mtoto anapokosea kwa makusudi.

Mtoto hata akikosea, baada ya muda mzazi anasahau na kumsamehe hata asipoomba msamaha.
Unajikuta bado unamtafutia maisha bora, unamkubali, unampenda.

Mzazi anapotazama macho ya mtoto wake, anaona wajibu. Ushamleta mtu duniani; unakua na moyo wa kuhakikisha yupo salama kiakili, kimwili apate mahitaji yote. Lakini hiyo siyo mwisho. Bado uhakikishe anakua mtu mwema kwenye jamii. Kama ni mvulana, aje kuwa mwanaume kamili mwenye maadili, heshima, upendo na kujitegemea.

Kama ni msichana, aje kuwa mwanamke kamili mwenye utu, heshima, upendo na kujitambua.
Bado uhakikishe anakua imara kupambana na changamoto za dunia hii.

Ni majukumu mengi, ya kimwili na ya kiroho. Na mara nyingi, mzazi huyafanya yote haya kwa kimya.
Hakuna anayejua kilio cha usiku, hofu ya kesho, na maumivu ya kuona mtoto wako akiteseka.

Ila sasa naona wazazi hua wanapitia mawazo ya kimyakimya. Haya ni mawazo yanayokuja kimya kimya, yakitafuna nafsi kama
"je nitamlea vema? Nitamfikisha alikokusudiwa? Atanielewa? Atanikumbuka?

Siku zote mzazi hutaka mema tu kwa mtoto wake. Unamtunza,
Unamsihi,
Unamwombea.

Lakini kuna wakati anachagua njia tofauti, au dunia inambadilisha. Na hapo ndipo mzazi huumia sana. Maumivu ya mzazi hayapimwi kwa macho ni maumivu ya ndani ya moyo, ya nafsi. Lakini bado yuko tayari kumpokea, kumsamehe, kumpa nafasi ya pili.

Kwa kweli, mzazi ni kiumbe wa kipekee. Anabeba uzito mkubwa moyoni, lakini anaonesha tabasamu usoni. Anapambana kwa ajili ya mtu mwingine kila siku, bila malipo ya moja kwa moja. Na ndiyo maana, mzazi anastahili siyo tu heshima bali shukrani ya maisha yote.

Kwa hiyo, tukumbuke kuwasikiliza wazazi, Kuwaheshimu na Kuwapenda.
Mkuu leo nimetoka kulipa ada za wanangu na pesa zilivyopotea nikawakumbuka wazazi wangu walivyojitoa kuhakikisha tunatimiza ndoto zetu. Hata kama juhudi zao hazikutufikisha kwenye marajio yetu 100% ila kumbukumbu zinaonyesha jitihada walizowekeza kwa wakati huo.

Wakati mwingine uzazi ni uwajibikaji usiohitaji malipo wala pongezi ndio maana wengi wetu huwa hatujui vikwazo walivyopitia wazazi wetu kutufikisha hapa tulipo. Ila tukitenga muda wa kukaa na wazazi chini na kujaribu kuwadadisi masahibu yao katika harakati za malezi, tutagundua kweli wazazi ni miungu wetu hapa duniani.
 
Amri inasema...

WAHESHIMU..! Baba na Mama upate HERI na Miaka/Maisha Mema/Mengi DUNIANI.

Uwekezaji ni mmoja tuu, KUWAHESHIMU.

JE HESHIMA ni nini...!???

Kibwagizo cha wimbo....

Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote, ushauri wao umeniletea mafanikio mema, sasa naishi, na watu vizuri eehh... sasa naishi, na watu vizuri eeeh eeehhhh...☺.
 
😂😂😂

Usiombe ukaolewa na kupata Wakwe wenye sifa hizo.
Utabadili mtazamo, pale unafungwa usizae na mama mkwe kumkomesha kijana wake anayetekeleza wajibu wake kama mumeo.

Au watoto wako kusumbuliwa,

Au Mumeo kumkatalia binti yenu kuolewa na kijana anayempenda baada ya kuchukua pesa za wenyewe.
Huyo ameshapoteza sifa ya kua mzazi.
 
Back
Top Bottom