Mzazi mwenzangu anadai atabadili cheti cha mtoto cha kuzaliwa atoe jina langu kwa kuwa ananichukia

Mzazi mwenzangu anadai atabadili cheti cha mtoto cha kuzaliwa atoe jina langu kwa kuwa ananichukia

Hujaelewa swali yote hayo nayajua hapa mimi nataka watu wenye uelewa kuhusu jambo kama hili watoe maoni yao na kuhusu kuacha aje akutafute unaweza kuacha tu lakini hapa kinacho angaliwa ni kwa namna gani mtu anaweza kuzuia au ni kwanini hii iwezekane je mamlaka za vyeti haziko makini au shida ni nini
Kubadili jina kuna process ndefu mno sidhani kama ataweza kirahisi.

Ni mikwara tu hiyo maana kufuatilia Deedpol sio jambo rahisi anaweza kuishia njiani.
 
Kubadili jina kuna process ndefu mno sidhani kama ataweza kirahisi.

Ni mikwara tu hiyo maana kufuatilia Deedpol sio jambo rahisi anaweza kuishia njiani.
Asante kwa mchango wako watu wengi watajifunza kupitia wewe
 
Hata usimjali... muache abadilishe, tafuta walipo kimya kimya na hakikisha mtoto anakutambua na uwe na mpango mkakati wa kumtimizia mahitaji kadiri ya uwezo wako mwanao (KAMA UNA UHAKIKA NI WAKO)
 
Hata usimjali... muache abadilishe, tafuta walipo kimya kimya na hakikisha mtoto anakutambua na uwe na mpango mkakati wa kumtimizia mahitaji kadiri ya uwezo wako mwanao (KAMA UNA UHAKIKA NI WAKO)
Ushauri mzuri sana nashukuru kwa mchango wako.
 
Ufafanuzi kuhusu cheti cha mwanzo, mifumo yetu bado haipo computerized. Mwanamke anaweza kwenda Rita akadai amepoteza cheti cha kuzaliwa cha mtoto, ataambiwa utaratibu wa kufuata police report etc, atajaza fomu upya akifika sehemu ya majina atabadili jina la mwisho aondoe lako aweke atakalojisikia yeye, wakiwa makini watamuuliza na atatoa sababu na watamkubalia na atapata cheti kipya ndani ya siku 7, na wasipokuwa makini kumuuliza bado atapata cheti kipya ndani ya siku 7. Hakuna sheria inayomzuia mama kubadilisha jina la mtoto na kubadilisha cheti. Inaruhusiwa. Tena kama hajaandikishwa shule ni rahisi zaidi. Pia kisheria hata ukiwa mtu mzima unaruhusiwa kubadilisha jina mojawapo kwenye process ni kwenda kuapa mahakamani, ila watu wanakwepaga usumbufu sababu ya jina kusambaa kwenye vyeti,vitambulisho nk. USHAURI:, Kama hutaki mama wa mwanao abadili jina lake njia rahisi ni moja tu, tuma ela ya matumizi kila mwezi hata kama ni ndogo, hata akiolewa na mtu mwingine hawezi kubadili, vinginevyo awe na asili ya ushetani.
Umemalizia vizuri sana mkuu. ukiona mwanamke kafikia hatua hiyo ujue jamaa hajishughukishi na mtoto
 
Kubadili jina kuna process ndefu mno sidhani kama ataweza kirahisi.

Ni mikwara tu hiyo maana kufuatilia Deedpol sio jambo rahisi anaweza kuishia njiani.
Ni rahisi sana unui tu
 
Unamuhudumia mtoto? Kama ndio kamshtaki ustawi, tafuta polisi, huko alipo atapatikana atapewa utaratibu maalum wa malezi ya mtoto wenu.
 
Hii ni stori ya upande mmoja. Mwanamke from no where unahudumia mtoto ipasavyo anataka kubadili jina la ubini wa baba yake?!!

Siwezi kusema chochote na hii stori yako.
 
Back
Top Bottom