Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Kuna ushauri nimepata humu wa kukusanya ushahidi wa mali za baba mtoto wangu na huo ndiyo niupeleke mahakaman ili alipe kulingana na uwezo wake ,sina lengo nitajirike kupitia child support lakini nataka kama mzazi nimekwama na yeye asaidie wakati mwingine kuwa postive ni vizuri
  • Siku ukitumia akili zako bila kushikiwa naakina Joyce Kiria utapata mafanikio.
  • Wanaume si maduwanzi kiasi hicho! Ukitumia mbinu hiyo unapotezwa asubuhi sana!
  • Kuna mwenzako huku mtaani kwa ujinga kama huo mtoto hajasajiliwa mtihani wa taifa.
 
Wanawake wanamatatizo Sana Mimi wangu alinipokonya mtoto na kashfa kibao kwamba Mimi maskini siwezi mtunza mwanae na nikimuhitaji masharti kibao lakini Leo hii ananitafuta nitoe maela kwa mtoto[emoji1787] na Mimi namkazia tuone yeye si alisema yupo vizuri atamtunza mwenyewe na anauwezo minipozangu tu namtazama kama nacheki derby ya kariakooo
[emoji38][emoji38][emoji38]kwamba wewe ni maskini
 
Wanawakee mnakuwaga na maneno sana mkiachana , sasa hv mnatafuta huruma za watu.
Mimi nilitengana na mzazi mwenzangu mwaka 2019,aliniambia waz waz kuwa hana mpango na mimi na wala hataki mia yangu kwani mtoto atahudumiwa na babake mpya.Tenaakataka kubadili mpaka majina ya mtoto ili ampe huyo msengerema mwenzake.
Sasa hivi analalama sana kwa marafiki na jamaa zangu kuwa sihudumii mtoto.
Wengi wako hivyo,
yakibuma huko wanarudi kutia huruma
 
Kuna ushauri nimepata humu wa kukusanya ushahidi wa mali za baba mtoto wangu na huo ndiyo niupeleke mahakaman ili alipe kulingana na uwezo wake ,sina lengo nitajirike kupitia child support lakini nataka kama mzazi nimekwama na yeye asaidie wakati mwingine kuwa postive ni vizuri
Utaharibu zaidi,
Kesi za hivi wasiliana na wazee (wazazi) wake, ukienda mahakaman umetangaza vita
 
Na akienda mahakamani sheria inasema mtoto kuanzia miaka saba anaweza kaa na baba yake,hvo utaambiwa kama umeshindwa kukaa nae mpeleke kwa baba yake.
 
Hawa viumbe ni kuishi nao kwa akili sana kwa kifupi najiona kabisa nakwenda kuitwa baba jina ( sio muwajibikaji kwa haya yanayotokea ).Ukikua mwanangu utakuja nikumbuka na utanitafuta .
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
Ukome inaonekana mwanzoni ulimuacha uyo mume kwa dharau ukijua utaweza mambo yote peke yako.
 
Kiufupi wanawake wanapenda sana show off ,mie mzazi mwezangu kamuhamisha mtoto darasa la NNE kumpeleka shule ya kiingereza baada ya miezi 8 kamrudisha kule kule kwa serikali

Ugomvi wetu mkubwa mie nitoe hela ya kusoma huko alikotaka yeye kwa vile nilijua huu ni mtego nikagoma

Kiufupi hakuna mwanaume asiyependa kulea mwanae ila viburi na maneno ya mama zao pamoja na kuwalisha sumu ,ukifikikia hela unayotoa unampa mamake unaghaili kabisa

Malezi bora ya mtoto wa nje yanategemea mawasiliano bora ya mama na baba sio unitukane afu uniambie nitume hela ya mtoto

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa yani hakuna mwanaume Ambaye hataki kulea mtoto lakini shida ni mama zao miyeyusho sana
 
Single mothers hata umpe mshahara mzima hakosi cha kulalamika. Utasikia anakusemelea kwa ndugu eti kaka yenu akipiga simu kuongea na mtoto anaongea dakika moja tu anakata. Yani wanajifanya wanayaweza alaf wakienda huko wakakuta ndivyo sivyo wanaanza kulia lia
 
Mnhhh....nyumba kuachiwa na ada ya mtoto ni vitu tofauti...umeamua tu kuwa mbishi...kisa mnadhani huyo mama anafaidi sana kwa mtoto kukaa nae..men are soo selfish at times..sijui kwa vile hamzai?
Sorry to say this.. huna akili na acha kumpotosha mwenzio.
 
Mtoa mada, kwakuwa mtoto ana miaka 7+ na endapo Baba atamchukua mtoto wake. Umewaza mstakabali wa hiyo nyumba aliyoacha Baba mtoto
 
Kuna mwingine nae alishauriwa vibaya na wenzake, jamaa anampa 100k kwa mwezi, kampangia chumba ili mtoto apate pa kulala. Yule mwanamke akaona haitoshi bora aende ustawi wa jamii ili matunzo yaongezwe as aliona jamaa anapesa so ana wajibu wa kumhudumia yeye na mtoto, poor that girl.

Kafika ustawi akaulizwa unapewa kiasi gani, kasema 100k, malazi ya mtoto analipa baba yake. Akaulizwa unajishughukisha na nini kajibu hana kazi kwa sasa, kaambiwa TAFUTA KAZI. Jamaa kwa hasira akasema nina uwezo wa kutoa 50k kila mwezi na sina uwezo tena wa kulipia chumba. Ikapita hivyo, bidada akaambiwa arudishe mtoto kwa bibi ili hiyo 50k iwe inatumwa huko kila mwezi.

Watu mnadhani huko ustawi ni roller coaster sio.?
Halafu kingine kujazia nyama, wadada wengi wanadhani ustawi kunabase upande mmoja. Ila siku hizi hao ustawi wanajionea vituko vya wadada, mambo yamebadilika wengi wanaangukia pua.
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
Fanya kazi kwa bidii, mhudumie mtoto ako wewe mwenyewe.
Usimsumbue wala kugombana nae kweny simu.
Akipiga simu ongea vzuri na usilalamike
Jipende na upendeze.
Ataanza kukufuatilia alaf badae atataka kujua mbona siku hzi upigizani makelele, hulalamiki utamwambia umechagua furaha.
Hapo atakua kwenye mabano atataka ajue hiyo furaha ni nin.
Mengine utajiongeza siwez sema kila kitu
 
Back
Top Bottom