Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Naona unatumia nguvu nyingi sana kuwa nyuma ya huyo dada, hakuna lugha ya kejeli hapo ni wazi kabisa kaachwa na nyumba kama maelezo ya mtoa mada yanavyoeleza, kama asingekuwa na nyumba angesema hapa kwamba ananiambia niuze nyumba ambayo hata si yake au hatukuwa na nyumba
Pole kwa kuelewa tofauti hajaniachia nyumba nimejenga mwenyewe
 
1: mzazi mwenzio watoto wake wanasona shule zipi?
2: kama una taka usaidiwe usiombe ada ya mtoto, wewe omba matumizi ya kumlea mtoto, swala la ada litaongelewa wakati kesi ikisikilizwa.
3: huko unakoishi tafuta wakili akuandikie hayo maombi peleka mahakamani atatumiwa summons, summons hiyo usipeleke wewe wala kuipeleka kwa mwenyekiti, apeleke process server wa mahakama ili akikataa kupokea kuwepo kiapo kama ushahidi. Taratibu nyingine utajuzwa huko mahakamani.

Nb wakati mnaachana mliachana kienyeji au? Maana kama mlifata sheria tunategemea mahakama iliweka utaratibu wa malezi ya mtoto including shule.

Hao wanaokushauri uza nyumba achana nao, mida hii wanatoka bar.hawawazi baada ya kuuza mtaishi wapi na mtoto.
Wanataka waishi kwenye miti kama ndege

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa kuelewa tofauti hajaniachia nyumba nimejenga mwenyewe
Kwenye keyboard una kauli ya upole na upendo...ungeitumia hii kwa mumeo sidhani kama angekimbia aache mwanae.
Ila endelea kupambania kile unachoamini ni haki yako.

Huwa mnanishangazaga sana nyie akina mama....mtoto akiwa mdogo kama hivi ni wa baba na anatakiwa awajibike, ila akishakua na kujiweza anakuwa wa kwako na unaanza kumweleza mabaya yote ya baba bila kuweka zuri hata moja.
Wanawake Mungu anawaona.
 
Poleni sana watoto wanaona siyo wajinga

Baba simamia wajibu wako mtoto hata alishwe kitu gani akija kukua anatengenisha pumba na mchele anajua kilicho sahihi.

Hakuna mtoto atapokea negativity Kwa baba aliyemsimamia kikamilifu.
 
Asante kwa faraja! Nyumba nimehangaika mwenyewe na siku zote namsomesha mwenyewe ila nimekwama tu kabisa ada safari hii yaani nimehangaika mpaka nikaona ngoja nirudi kwa mwenzangu anisaidie sasa ndiyo kunijibu hana hela au niuze nyumba ni kanijibu maneno ya kuudhi tu ili niumie
Hiyo nyumba ni ya kwakoo?
 
Wanawakee mnakuwaga na maneno sana mkiachana , sasa hv mnatafuta huruma za watu.
Mimi nilitengana na mzazi mwenzangu mwaka 2019,aliniambia waz waz kuwa hana mpango na mimi na wala hataki mia yangu kwani mtoto atahudumiwa na babake mpya.Tenaakataka kubadili mpaka majina ya mtoto ili ampe huyo msengerema mwenzake.
Sasa hivi analalama sana kwa marafiki na jamaa zangu kuwa sihudumii mtoto.
ndio walivyo hao viumbe, Wana jeuri Sana mdomoni
 
Na mimi nilikua ni mmojawapo kuwa niliamua kupambana tu nilee mwenyewe ila sasa hali imekua ngumu sana naona nitashindwa ndiyo nikaamua nimshirikishe lakini mwenzangu naona hataki anataka kunikomoa tu kwahiyo naona nimpeleke mahakaman ili awe analipia huko na matumizi kabisa
We mgumu kuelewa, mtoto ana miaka Tisa, jamaa atamchukua akaenae Kama wewe umeshindwa kumlea Hali ngumu, kwa umri huo anaruhusiwa kukaa na baba yake kwanza
 
Nitafurahi kama akimchukua nimekua nikijaribu hilo pia anakataa anasema mke wake ana mtoto haweza kwanini sitoboi?
Hawezi kumlipia hiyo Ada wakati elimu serikali inatoa bure, na hela ya matumizi atahamriwa na mahakama akupe elfu thelasini kwa mwezi
 
najaribu kuimagine ungepata sponsor mzuri halafu baba mtoto awe anamhitaji mtoto wake.... nahisi angekula matusi sio ya dunia hii, wanawake mna matatizo sana.
Sawasawa mkuu hapo kilichopo ni hicho sponsor kakimbia au kafulia ndo kakumbuka kuna baba wa mtoto.
 
Unaona ulivyocherema[emoji23]

Kwa hiyo mtoto alelewe na Baba WA kambo wakati Baba yake mzazi yupo sivyo,

Wanawake macherema Kama ninyi mnatakiwa Mungu awape wanaume dizaini yangu ili akili ziwakae.

Mahakamani au ustawi wa jamii, usifikiri kuna watu wajinga wajinga Kama wewe.

Hoja mwanaume atazozitoa
1. Mtoto anamiaka 9 hivyo anaweza kuishi na Baba. Hata sheria zinaeleza.
2. Mpaka tunafika hapa Mama yake(wewe) ameonyesha Hana uwezo wa kuendelea kumtunza Mtoto kutokana na mahitaji ya mtoto kuongezeka. Hivyo naiomba Mahakama au Ustawi Kwa ruhusa yenu mniruhusu nimchukue mwanangu nimlee mwenyewe. Atakuwa anaenda kumsalimia Mama yake.
Pia sitamuomba Mama yake pesa yoyote ya kumuangalia mtoto.

3. Kutokana na matukio ya ulawiti kushika Kasi, mtoto wangu nahofia kulelewa na Baba WA kambo. Wote tunajua dunia imebadilika.

4. Nafikiri mtoto nikimlee itamrahisishia Mama na taifa letu kupata mtoto Bora kwani nitamuandaa kama wenzake kufanya shughuli ndogondogo za Ujuzi
Watoto wenzake waliopo pale NYUMBANI kila mmoja anamradi wake anaousimamia, kuna anayefuga kuku, mwingine Bata mzinga, hivyo wanajenga Ujuzi hata pesa ya matumizi siwapi wanazitolea kwenye miradi Yao.
Mtoto wangu huyu Naye atakuwa kama wenzake tena hiyo pesa anaweza msaidia hata mama yake.

5. Mtoto nikimlea Mimi wala hatutarudi tena hapa ustawi wa jamii au mahakamani kuwasumbueni. Kwani mahitaji yake na haki zake zitalindwa Kwa ukaribu zaidi kuliko akiwa mbali nami.

6. Mama yake Hana kazi inayomtosheleza kumhudumia huyu mtoto.

7. Mama yake anakosa fursa ya kuolewa na kutukanwa kuwa ni single mother kisa mtoto wangu. Ni bora nimchukue mwanangu ili kumpunguzia adha na masimango kutoka Kwa jamii.
Ndugu Hakimu, au afisa ustawi sote tunajua ilivyongumu Kwa Mwanaume kuoa single mother, ndio maana Kwa kumsaidia mwenzangu ili apate mtu mwingine nimeonelea mahakama iniruhusu nimlee mwanangu

8. Tunawapa mzigo watu wasiohusika.
Kwa nini mtoto wangu awe mzigo Kwa Baba yake wa kambo ilhali Mimi nipo, pesa kuigawanya ni ngumu ndio maana naomba mwanangu ajumuike huku na apunguze mzigo Kwa Baba WA kambo. Wote tunajua maisha ni magumu
Na Hii ndo Atakachokutana nacho huko anakoshauriwa aende
 
1: mzazi mwenzio watoto wake wanasona shule zipi?
2: kama una taka usaidiwe usiombe ada ya mtoto, wewe omba matumizi ya kumlea mtoto, swala la ada litaongelewa wakati kesi ikisikilizwa.
3: huko unakoishi tafuta wakili akuandikie hayo maombi peleka mahakamani atatumiwa summons, summons hiyo usipeleke wewe wala kuipeleka kwa mwenyekiti, apeleke process server wa mahakama ili akikataa kupokea kuwepo kiapo kama ushahidi. Taratibu nyingine utajuzwa huko mahakamani.

Nb wakati mnaachana mliachana kienyeji au? Maana kama mlifata sheria tunategemea mahakama iliweka utaratibu wa malezi ya mtoto including shule.

Hao wanaokushauri uza nyumba achana nao, mida hii wanatoka bar.hawawazi baada ya kuuza mtaishi wapi na mtoto.
Hatujaachana na talaka, alikataa kinipa talaka japo yeye ndiye aliyeniacha, sasahiv mara nyingi anapiga simu turudiane na kuwapigia hadi wazazi wangu lakini mimi naona inatosha ndiyo maana nadai tu anisaidie mtoto kutunza
Mtoto wake bado hajaanza shule huko aliko na hata yeye pia amejenga
Asante sana kwa ushauri nimeuzingatia
 
Unaona ulivyocherema[emoji23]

Kwa hiyo mtoto alelewe na Baba WA kambo wakati Baba yake mzazi yupo sivyo,

Wanawake macherema Kama ninyi mnatakiwa Mungu awape wanaume dizaini yangu ili akili ziwakae.

Mahakamani au ustawi wa jamii, usifikiri kuna watu wajinga wajinga Kama wewe.

Hoja mwanaume atazozitoa
1. Mtoto anamiaka 9 hivyo anaweza kuishi na Baba. Hata sheria zinaeleza.
2. Mpaka tunafika hapa Mama yake(wewe) ameonyesha Hana uwezo wa kuendelea kumtunza Mtoto kutokana na mahitaji ya mtoto kuongezeka. Hivyo naiomba Mahakama au Ustawi Kwa ruhusa yenu mniruhusu nimchukue mwanangu nimlee mwenyewe. Atakuwa anaenda kumsalimia Mama yake.
Pia sitamuomba Mama yake pesa yoyote ya kumuangalia mtoto.

3. Kutokana na matukio ya ulawiti kushika Kasi, mtoto wangu nahofia kulelewa na Baba WA kambo. Wote tunajua dunia imebadilika.

4. Nafikiri mtoto nikimlee itamrahisishia Mama na taifa letu kupata mtoto Bora kwani nitamuandaa kama wenzake kufanya shughuli ndogondogo za Ujuzi
Watoto wenzake waliopo pale NYUMBANI kila mmoja anamradi wake anaousimamia, kuna anayefuga kuku, mwingine Bata mzinga, hivyo wanajenga Ujuzi hata pesa ya matumizi siwapi wanazitolea kwenye miradi Yao.
Mtoto wangu huyu Naye atakuwa kama wenzake tena hiyo pesa anaweza msaidia hata mama yake.

5. Mtoto nikimlea Mimi wala hatutarudi tena hapa ustawi wa jamii au mahakamani kuwasumbueni. Kwani mahitaji yake na haki zake zitalindwa Kwa ukaribu zaidi kuliko akiwa mbali nami.

6. Mama yake Hana kazi inayomtosheleza kumhudumia huyu mtoto.

7. Mama yake anakosa fursa ya kuolewa na kutukanwa kuwa ni single mother kisa mtoto wangu. Ni bora nimchukue mwanangu ili kumpunguzia adha na masimango kutoka Kwa jamii.
Ndugu Hakimu, au afisa ustawi sote tunajua ilivyongumu Kwa Mwanaume kuoa single mother, ndio maana Kwa kumsaidia mwenzangu ili apate mtu mwingine nimeonelea mahakama iniruhusu nimlee mwanangu

8. Tunawapa mzigo watu wasiohusika.
Kwa nini mtoto wangu awe mzigo Kwa Baba yake wa kambo ilhali Mimi nipo, pesa kuigawanya ni ngumu ndio maana naomba mwanangu ajumuike huku na apunguze mzigo Kwa Baba WA kambo. Wote tunajua maisha ni magumu
Nimeshamwambia mara nyingi sana aje amchukue aishi naye ila hatak,kwahiyo akienda kusema hivyo mahakanan sitakua na pingamizi,
 
Hawezi kumlipia hiyo Ada wakati elimu serikali inatoa bure, na hela ya matumizi atahamriwa na mahakama akupe elfu thelasini kwa mwezi
Angalau atakua amesaidia! Kama wewe ni hakimu au unajua sheria asante kwa huu ufafanuz
 
Kwenye keyboard una kauli ya upole na upendo...ungeitumia hii kwa mumeo sidhani kama angekimbia aache mwanae.
Ila endelea kupambania kile unachoamini ni haki yako.

Huwa mnanishangazaga sana nyie akina mama....mtoto akiwa mdogo kama hivi ni wa baba na anatakiwa awajibike, ila akishakua na kujiweza anakuwa wa kwako na unaanza kumweleza mabaya yote ya baba bila kuweka zuri hata moja.
Wanawake Mungu anawaona.
Umekurupuka,tulia usome uelewe
 
Back
Top Bottom